Header Ads

UGONJWA HATARI WA UTI :ATHARI KINGA NA MATIBABU YA UGONJWA WA UTI.



Asilimia kubwa ya Watanzania hawaujui vizuri ugonjwa wa UTI. Kumekwepo na maelezo kutoka kwa watu mbali mbali na wakati mwingine hata kwa wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huu lakini bado watu wengi wanakanganyika na ukweli halisi.Leo nitajaribu kutoa maelezo walau kwa kina ili jamii iujue ugonjwa huu kinagaubaga.

Kwanza kabisa kirefu cha cha herufi UTI ni URINARY TRACT INFECTION ikimaanisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.

Msomaji anapaswa kujua njia ya mkojo ni ipi, inaanzia wapi na inaishia wapi. Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke. Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS.Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu.Wanawake wanakua na urethra fupi 4cm kulinganisha na wanaume 25cm hivo kupelekea kupata UTI kwa urahisi.

Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS. Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayokwenda kwenye figo mbili. Mirija hii inaitwa URRETERS na ikishaambukizwa inajulikana kama URRETITIS.Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani KIDNEYS na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.


Hivyo sababu huambatana na chanzo cha tatizo katika mojawapo ya sehemu husika, Mfano:
1. Ugonjwa wa sukari hufanya kiwango cha sukari kuwa kikubwa kwenye damu kwa vile mafigo kazi yake ni kuchuja damu hivyo ni kusema sukari huingia kwa wingi kiasi cha kusababisha vidudu bakteria kuzaliana kwa wingi kwenye mafigo au kibofu cha mkojo.

2. Madawa /sumu huchubua utando wa njia ya mkojo na kusababisha bacteria kuzaliana

3. Matatizo ya vijiwe kwenye figo/ mirija ya mkojo, kibofu, hufanya msongomano wa mkojo na Vijidudu huzaliana.

4. Maradhi ya Tunda Prostate gland huvimba na kufunga njia ya mkojo matokeo yake kuuzuia na kuuweka mkojo mda mrefu kwenye kibofu mpaka bacteria kuzaliana.
5. Tendo la ndoa, sexual intercouse unapata vijidudu moja kwa moja kutoka kwa mwanamke mwenye uambukizo

6. Kujichua, tendo hili mara nyingi watu hutumia mafuta au sabuni ambazo huwa zina kemikali zinazopenya kwenye mrija wa mkojo huwasha na kusababisha vidonda ambayo bacteria hukua na kazaliana

7. Usafi, aidha kwa kujikamua sana baada kukojoa, kutawaza maji machafu kutokuwa na hali ya unadhifu, huko chini kuna vijidudu ambavyo huishi baina ya njia ya haja kubwa na makorodani kutokana na hali ya ujoto humea vizuri na hupata nafasi ya kukuingia kwenye mirija kama utakuwa huna tabia ya kuwapunguza kwa usafi.
Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi.Lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana nazo ni maumivu wakati wa kukojoa na pengine kutoka uchafu au usaha kwenye njia ya mkojo.Hizi ni dalili za UTI kulingana na aina ya maambukizi.Kama nilivotangulia kusema awali zipo aina tatu za UTI urethritis(maambukizi kwenye mrija wa mkojo),cystitis (maambukizi kwenye kibofu) na pyelonephritis(maambukizi kwenye figo)

WASILIANA NASI NAMBA 0762701427

No comments:

Powered by Blogger.