Header Ads

RANGI YA UTE AU UCHAFU UNAOTOKA ILI KULINDA MAENEO YA UKE

Tokeo la picha la kutokwa na ute mweupe mzito ukeni

Ni kawaida kushangaa endapo kama rangi au uchafu unatoka mara kwa mara ukeni kuwa ni wa kawaida au unahitaji kuchunguzwa. Uchafu utokao ukeni unaweza kuwa na rangi nyingi, na viashiria mbalimbali ili kuonyesha kuwa mwili una afya.
Katika makala hii tunaenda kujifunza ili tujue je, ute unalinda maeneo ya uke unakuwa na rangi gani?


Je, Uchafu Unaotoka Ukeni Huwa Ni Kitu Gani?

Uchafu utokao ukeni huwa ni majimaji fulani yanayotengenezwa kutoka kwenye tezi ndogo zinazokuwa ukeni na kwenye mlango wa kizazi. Maji maji haya huvuja kutoka ukeni kila siku ili kuondoa seli zilizochoka pamoja na mabaki, ili kuufanya uke pamoja na njia ya mfumo wa uzazi uwe katika hali yenye afya nzuri.Kiwango cha uchafu unaotoka ukeni kinaweza kutofautiana kwa kila mwanamke. Rangi, uzito, na kiwango vinaweza pia kubadirika kila baada ya siku, kutegemeana na mazingira ya mwanamke anapokuwa hedhini:


  • Siku ya 1-5

Mwanzoni mwa mzunguko wa hedhi, uchafu unaotoka ukeni mara nyingi huwa mwekundu au wenye damudamu, kadiri mwili unavyotumia nguvu kuliondoa gamba laini linalokuwa juu ya ukuta wa mfuko wa kizazi.

  • Siku ya 6-14

Kipindi cha hedhi kinachofuata, mwanamke anaweza kuona damu kidogo ikitoka ukeni kuliko kawaida. Yai linapoanza kukua na kukomaa, basi ute utelezi unaokuwa kwenye mlango wa kizazi utabadirika na kuwa wenye rangi ya kijivu au mweupe au wa njano. Unaweza ukawa mzito.


  • Siku ya 14-25


Siku chache baada ya yai kupevuka, ute utelezi hubadirika na kuwa mwepesi wenye kuteleza, kama ute wa yai la kuku vile. Baada ya yai kupevuka, ute hubadirika na kuwa wenye rangi ya kijivu, mweupe au wa njano, na wenye kunata.



  • Siku ya 25-28:

Ute utelezi unaokuwa kwenye shingo ya kizazi hubadirika na kuwa mwepesi, na mwanamke anaweza kuuona kidogo tu, kabla hajaingia kwenye kipindi kingine cha hedhi.


  1. Uchafu Wenye Rangi Nyekundu


Uchafu huu mwekundu unaweza kutofautiana, kwani unaweza kuwa wenye rangi yenye kung’aaa au nyekundu sana. Uchafu mwekundu huwa ni matokeo ya damu ya hedhi kuanza kutoka.
Damu ya hedhi hutokea, kwa wastani, kwa kila mzunguko wa siku 28, ingawa kiwango cha kati huwa ni siku 21 na 35. Hedhi huwa ni ya siku 3-5.
 NUKUU: Mwanamke yeyote anayepata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja, anapaswa afike hospitali mapema ili kumuona daktari. Ingawa kuna visababishi vingi hafifu vya kumfanya mwanamke apate hedhi mara mbili kwa mwezi, lakini navyo vinaweza wakati mwingine kuwa viashiria vya matatizo mabaya baadaye.
Mwanamke yeyote aliyefikia hali ya kukoma hedhi na kutokuona hedhi kwa takribani mwaka mmoja, anapaswa amuone daktari mapema ikiwa kama anapatwa na hali ya kutokwa na damu ukeni. Hii yaweza kuwa ni dalili ya salatani.

  1. Uchafu Mweupe


Uchafu mweupe unaweza kuongezeka, unaweza ukawa kama maziwa vile au wa njanonjano kwa mbali. Endapo mwanamke hatakuwa na dalili zingine, basi uchafu mweupe unaweza kuwa kiashiria kabisa cha kilainishio kizuri chenye afya ukeni mwake. Utakuta uke wake uko katika hali nzuri hata anapokutana kimapenzi na mwezni wake hakutakuwa na shida yoyote zaidi ya kufurahia tendo la ndoa.NUKUU: Hata hivyo, endapo kama uchafu mweupe utakuwa mzito kama maziwa mtindi vile na kuwa na harufu mbaya, basi hii yaweza kuwa dalili za maambukizi. Muhusika anapaswa afike hospitali haraka bila kuchelewa ili kumuona daktari wa vipimo.
Uchafu mweupe wenye kunata, na wenye harufu mbaya mara nyingi huwa ni wenye maambukizi ya fangasi, ambao pia unaweza kusababisha muwasho ukeni.


  1. Uchafu Wenye Rangi Ya Njano Na Ukijani


Kama uchafu una rangi ya njano njano, inaweza isiashirie tatizo kwako. Hali hii hasa inaweza ikasababishwa kubadirika kutokana na vyakula unavyotumia.Uchafu ambao ni wa njano kabisa, unjano wenye ukijani, au kijani yenyewe, mara nyingi huwa ni dalili za bakteria au maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Jitahidi kumuonda daktari mapema endapo kama uchafu ni mzito na wenye harufu mbaya.

  1. Uchafu Wenye Rangi Ya Pink


Uchafu unaweza kuwa wenye rangi ya pinki kwa mbali au kabisa. Mara nyingi huwa unakuwa na damudamu kidogo. Uchafu wenye rangi ya pinki kwa kawaida  hujitokeza huku ukiwa na matone ya damu damu kabla ya kipindi cha hedhi kuwadia. Hata hivyo, inaweza pia kuwa ishara ya damu kutoka pale yai linapojipachika kwenye ukuta wa tumbo la uzazi ujauzito unapoingia.
0765203999

No comments:

Powered by Blogger.