Header Ads

Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume

Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume

Uzazi wa mpango ni jumla ya vitu vingi sana
Uzazi wa mpango hauhusu kuzuia kupata ujauzito tu bali hata kupangilia idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi wa mpango..
Wanandoa wengi wamekua wakitamani kupata jinsia flani za watoto ili wapate watoto wachache.
Hata hivyo wakati mwingine inatokea wanapata watoto wa jinsia moja tu ya kike na hivyo hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika yaani mtoto wa kiume.
Zipo familia ambazo hufikia hadi kugombana na kutengana kwa sababu hii.
Baadhi ya kabila na koo za watu upande wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa inapotokea mama anazaa watoto wa kike tu.
Kwenye makala hii naenda kumaliza kitendawili hiki kwa kukueleza njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi.
Endelea kusoma  …
Kisayansi mbegu zinazotoa mtoto wa kiume zinaitwa XY.
Mbegu hizi zinapotoka kwa mwanaume huenda kwa mwendo wa kasi sanakwenda kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke lakini shida kubwa ni kuwa mbegu hizi XY hufa haraka SANA zikiwa njiani.
Wakati mbegu zinazotoa mtoto wa kike zinaitwa XX.
Mbegu hizi husafiri taratibu na huchelewa kufika ndani ya mfuko wa uzazi. Kwakuwa mbegu hizi yaani XX huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.
Kwahiyo namna pekee ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume ni kuhakikisha mbegu za kiume XY zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla hazijafa  ….
Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume:
1. Shiriki tendo la ndoa siku mayai ya mkeo yanapokua yameshuka

Siku yai linapokuwa limeshuka
Unaposhiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka (ovulation day) mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike na kuunda ujauzito.
Kwa kawaida huwa ni siku ya 14 kabla ya kuona damu ya mwezi unaofuata na siyo baada ya kuona siku zako.
Ikiwa wewe mwanamke huifahamu siku yai linapokuwa limeshuka basi tumia ishara ya kuongezeka kwa joto mwilini mwako.
Pima joto la mwili wako. Nunua kifaa cha kupimia joto (thermometer) na ujipime joto la mwili wako kila siku asubuhi.
Siku ukipima ukaona joto limeongezeka kidogo basi ujue yai limeshuka (ovulation day) na hiyo ndio siku hasa ya kutafuta mtoto wa kiume.
Pia angalia maji maji ya uke. Shika maji maji ya uke wako na kwa kawaida siku yai likiwa limeshuka utaona maji ya uke kuwa ni mazito na yanavutika kama maji ya mayai mabichi.
2. Mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako
Mwanaume unatakiwa uongeze wingi wa mbegu zako (sperm count). Hili linawezekana hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati ukisubiri mke aanze kuona yai linashuka (ovulation day).
Pia hakikisha hauvai nguo za kubana sana na usikae mazingira ya joto sana.
Kwa kawaida korodani zinatengeneza mbegu nyingi zaidi wakati wa hali ya ubaridi kuliko kwenye  joto hivyo mwanaume unatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, acha kuweka laptop kwenye mapaja, acha kuvuta sigara na kunywa pombe.
Wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara wanapata tatizo la kuwa na mbegu chache na mbegu kidogo sawa sawa na wavutaji wa bangi na watumia madawa mengine ya kulevya.
Pia ikiwa mwanaume anatumia dawa za kutibu saratani pia husababisha uzalishaji wa mbegu kuwa mdogo.
3. Tumia staili za tendo la ndoa ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa
Staili hizi huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume yaani XY kufika haraka na kufanya utungwaji wa mimba kuwa rahisi.
Unahitaji utumie staili ambazo zinawezesha mwingiliano mkubwa (deep penetration) na hii ni mhimu hasa kama wewe mwanaume una kibamia.
Wakati unapotumia staili za  mwingiliano mdogo (shallow penetration) husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi na hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike (XX) kutungisha ujauzito na hapo anatokea mtoto wa kike.
4. Hakikisha mwanamke anafika kileleni kwanza
Dawa mbadala zinazotumika kurejesha uke mkubwa au uliolegea
Wakati wa tendo la ndoa mwanaume hakikisha mkeo anafika kileleni kwanza kabla ya wewe.
Mwanamke anapofika kileleni huwa anatoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo huwa haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.
Sasa mwanaume utahitaji kuchelewa kufika kileleni lakini uonapo tu mama amefika kileelni basi na wewe ufike muda huo kabla hakujakauka. Namna rahisi kama wewe ni mtu wa kukojoa haraka ni kumnyonya kinembe mama kwa dakika kadhaa na hatachelewa kufika kileleni.
Hapa nguvu za kiume zinahitajika sana. Pia ni mhimu mwanaume uzifahamu dalili za mwanamke anapofika kileleni huwa anakuwaje.
5. Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya yai kushuka
Kabla ya siku yai kushuka (ovulation day) kawaida mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi kama kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya siku hii kupita.
Tumia kila mbinu kila elimu kuhakikisha unaifahamu siku hii yai linaposhuka kwani ndiyo siku pekee yenye uhakika wa kutungisha mtoto wa jinsia ya kiume.
6. Mwanamke aepuke vyakula na vinywaji vyenye asidi 

Kahawa
Mwanamke anatakiwa kwa kipindi kirefu ale vyakula na anywe vinywaji visivyo na asidi (tindikali).
Vitu vinavyoongeza asidi mwilini ni pamoja na vyakula vya kusisimua (spiced foods), vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, pombe, chai ya rangi, kahawa, baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, maziwa na bidhaa zingine zitokakanazo na maziwa n.k.
Vyakula visivyo na asidi nyingi ni pamoja na matunda, mboga za majani, maji ya kunywa, mbegu mbegu (za karanga, za ufuta, korosho, za maboga nk), apendelee kula uyoga pia.
Mwisho wa siku usiache kumuomba Mungu kwani yeye ndiye muweza wa yote.

29 comments:

  1. Pongezi doctor kwa elimu safi na ushauri mwanana kwa kweli hata Mimi ni mhanga katika hili, lakini kutokana na ushauri wako nitajitahidi kutekeleza yote lakini katika kusoma kwangu note sijaelewa neno kibamia ninaweza kupata msaada zaidi asante.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kibamia ni kuwa na maumbile madogo ya Uume.

      Delete
    2. Kibamia ni kuwa na maumbile madogo ya Uume.

      Delete
    3. Kibamia ni kuwa na maumbile madogo ya Uume.

      Delete
  2. Hahaha umetisha sana mzee kwahili nakupongeza

    ReplyDelete
  3. Asante sana doctor kwa somo zuri sana nimekuelewa. Naomba kuuliza kwa mtu ambaye mzunguko wake hauko constant hiyo siku ya 14 kabla ya kuona siku zake ataijuaje? Mfano mi October nilienda tr 19,November tr 13, December tr 7.Siku ya 14 ya mwezi ujao nitaijuaje. Asante

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapa hata mimi sijaelewa swali zuri kweli maana kuna wengine mzunguko hubadilika jinsi ya kuijua hiyo tarehe ndo tatizo atueleze na hapo.

      Delete
    2. Kinachobadikika nini kwako, yaani mzunguko sio stable au..? Mzunguko wako ni wa Siku ngapi, je ni wa Siku 25 au 26 au 27 au 28 ni.
      Chamsingi unatakiwa ujue mzunguko wako ni wa Siku ngapi. Ukijua mzunguko wako, unachotakiwa wewe ni kuhesabu Siku tangu unapoanza kubleed Siku ya kwanza, ikifika katikati ya mzunguko yai linakuwa tayari,.
      Kwahiyo Fanya sex kuanzia Siku moja kabla ya kufika katikati ya mzunguko mpaka Siku moja baadae.

      Delete
  4. Asante kwa elimu nzuri , nimejifunza mengi sana.

    ReplyDelete
  5. Asante Sana.. nimepata kitu nashukuru.

    ReplyDelete
  6. Thanks Papaa Kwa Elim Taam Doctor

    ReplyDelete
  7. Habari Daktari naweza Pata namba yako ya simu tafadhali

    ReplyDelete
  8. Nimeshindwa kujua mzunguko wa siku zangu kama ni siku 28 au 29...mwanzoni nilikua sijui ila nikaona nianze kuweka tarehe nione inakuaje...Nilichoshindwa kuelewa ni kwamba mwezi uliopita Feb niliingia siku zangu tarehe 23 jioni kama saa 12 ilikua Jumapili...Na mwezi huu ilikua nianze tarehe 22 kama ni siku 28 ila nilianza usiku wa kuamkia tarehe 23 saa 8 usiku yaan jumapili usiku.ina maana masaa hayahesabiwi maana nashindwa kutambua nitahesabuje..

    ReplyDelete
  9. Asante daktari Nimeshindwa kujua mzunguko wa siku zangu kama ni siku 28 au 29...mwanzoni nilikua sijui ila nikaona nianze kuweka tarehe nione inakuaje... Nilichoshindwa kuelewa ni kwamba mwezi uliopita Feb niliingia siku zangu tarehe 23 jioni kama saa 12 ilikua Jumapili... Na mwezi huu ilikua nianze tarehe 22 kama ni siku 28 ila nilianza usiku wa kuamkia tarehe 23 saa 8 usiku yaan jumapili usiku. Je Masaa pia yanahesabiwa? Na kama yanahesabiwa ina maana ni siku 28 au 29?

    ReplyDelete
  10. Hata mimi ninapenda sana mtoto wa kiume aisee dah

    ReplyDelete
  11. Dr asanteee Sasa wakat mwingine mzunguko unasogea Sana na mpk cku 35,,ntajuaje cku ya kupata mtoto wa kiume

    ReplyDelete
  12. Asante Dr.nimejaribu kufuatilia somo lako ni zuri nikaamua kudownload calender ya mzunguko lakini ikifika siku ya 14 calendar inanionyesha kidoti ambacho kinakuwa na doa jeupe ikifika siku ya 15 kidoa kinakuwa chekundu kote, Je siku sahihi ya ovulation ni ipi?

    ReplyDelete
  13. Asante kwa elimu,mwaka Jana nilisoma makala hii na kuitumia kwenye ndoa yangu na hatimaye mke wangu kajifungua mtoto wa kiume,haja yangu ilikuwa ni mtoto wangu wa kwanza awe mwanaume.Namshukuru Mungu kwanza na wewe pia .

    ReplyDelete
  14. Yaani mara nyingi huwa namtafuta mwenye maarifa km Niko nayo leo nimempata maana watu wengi na wengine wanaitwa wataalamu wa afya lkn hawajui kalenda ya hedhi iliyo sahihi yaani Ni waongo na wababaishaji. Nimefurahi leo ninachokiamini mm nimempata mwenye uelewa km wangu. Kilichoelezwa hapa ndicho kweli. Kwa mtu asiye na tatizo lolote yaani aliye sahihi kabisa hedhi yake Ni siku 7. Tatizo Ni kwamba hatupaswi kutumia zana isiyo kamili kufundishia Bali zana kamili ili kupata ukweli. Kumbuka sayansi Ni ukweli c bahat nasibu. C kwamba cku saba zote Ni maporomoko ya damu, no Bali hupungua kadri cku zibavoe ndelea hadi ya saba Ni ute wenye damu kwa mbali, ikifika 8 na zaidi huyo amuone daktari tena daktari sahihi. Baada ya saba hesabu cku 2 za maintanance hapa Ni free, then Kuna ovulation pia yai huanza kutoka kwenye oviduct cku ya kumi kuingia kwenye falopian tube kuelekea kwenye uterus na hufika kati ya cku ya 13, 14 na ya 15 huwepo. Lkn tangu cku ya kumi mimba huweza kutungwa hata km yai halijafika kwenye uterus likisharutubishwa kiinitete hicho huendelea na safar hadi mji wa mimba kikishindwa tunasema mimba nje ya kizazi na hapa uwezekano mkubwa Ni mtoto wa kike kwa sababu alizoeleza mtaalamu japokuwa inategemea pia uwezo na ubora wa mbegu za mwanaume pamoja na umbali yai lilikokuwa. Nimeenjoy nkajikuta nami naeleza yangu maana tangu nisome habari hizi mtandaoni cjawahi pata ninayenana naye uelewa hasa juu ya kalenda ya hedhi na ndiyo ninayoiamini kwani naitumia kwangu mwenyewe km zana ndo maana naiamini na kumwamini Sana mwl alonifundisha. C kila kinachoandikwa Ni sahihi Bali Ni mawazo ya watu na c kila wazo Ni ukweli Bali utakuwa ukweli kwa kufanya uchunguzi wa kweli na kupata majibu ya kweli ktk wazo Hilo. Nasikitika kwamba hata baadhi ya wataalamu wengi wa afya wanapotosha ktk hili yaani hawaijui kweli na wanatumia zana zenye udhaifu kueleza kweli niombe tutumie zana sahihi yaani mwanamke asiye na tatizo lolote mwenye mzunguko wa cku 7 za hedhi na anayekamilisha mzunguko wote kwa cku 28. Huyo ndo atakupa ukweli ktk hili c vinginevyo. Asante Sana mtaalamu umenikumbusha mengi na mengine nimeyatunza akilini tunaweza kushare idea kwa no 0625656376.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Je asiyekuwa na mzunguko wa siku28 ataingia hedhi siku 7 na je yai litatoka ktk oviduct Siku ya 10?

      Delete
  15. Naomba unisaidie kujua mzunguko wangu Kama ni wa siku 28 mwezi wa nne iliingia bleed tarehe tatu na na nikaipata Tena tarehe 27 mwezi wa nne mpaka tarehe moja naomba msaada

    ReplyDelete
  16. Maumivu yanayotokea siku chache baada ya kumalizika hedhi ni maumivu ya kusafiri kwa yai kuelekea ktk uteras au ni maumivu ya nini?

    ReplyDelete
  17. Nimeingia bleed tar 10 mwez huu nikamsliza tar 13 na mzunguko wangu Ni was siku 28 siku ya 14 hapa Ni ipi

    ReplyDelete
  18. Elimu iko poa Sana keep it up doctor

    ReplyDelete

Powered by Blogger.