TATIZO LA MWANAUME KUSHINDWA KUSABABISHA MIMBA KWA MWANAMKE(UTASA)
Dr George
Habari za siku nyingi ndugu,jamaa,wapenzi na wafuatiliaji wa jukwaa hili la afya.Poleni kwa mihangaiko ya kila inapoitwa Leo,hatuna budi kumshukuru Muumba kwa kusema “Aksante Mungu”.
Kama ilivyo-ada leo tunaendelea na mfululizo wa masomo yetu hapa jukwaani.Leo tutakuwa tukizungumzia tatizo linalozikabiri ndoa nyingi ktk jamii yetu,tatizo la mwanaume kushindwa kusababisha mimba kwa mwanamke yaani Utasa.
UTASA NI NINI?
Utasa ni hali au tatizo linalompata mwanaume na kushindwa kusababisha utungwaji wa mimba kwa mwanamke baada ya kufanya mapenzi(bila njia yoyote ya uzazi wa mpango) kwa muda wa miezi kadhaa(6-12) kwa wastani wa mara mbili au tatu kwa wiki. Au
Ni hali ya mwanaume kushindwa kusababisha mimba kwa mwanamke kwa kipindi cha miezi 6-12 bila kutumia njia yoyote ya kuzuia utungwaji wa mimba.
Tatizo hili huweza kusababishwa na mbegu kuwa chache(low sperm count),mbegu kushindwa kuogelea vizuri ktk via vya uzazi vya mwanamke(azooasthenospermia),kuwa ktk umbo lisilo la kawaida,ukosefu wa vichochezi muhimu(testosterone) au kuwa na tatizo ktk mirija ya uzazi ya mwanaume(ejaculatory systems).
ZIPI NI AINA ZA UTASA?
Kuna aina mbili za utasa;
1.Primary male infertility;katika aina hii mgonjwa anashindwa kusababisha mimba na anakuwa hana historia ya kumbebesha mimba mwanamke.
2.Secondary male infertility;hii hutokea pale mwanaume anakuwa ktk historia ya maisha yake ameshawahi kusababisha mimba au kuwa na watoto ila tatizo linampata baadae.
NB:Kuna tofauti kati ya Hanisi(Erectile dysfunction) na Tasa(visichanganywe).Uhanisi ni hali ya mwanaume kushindwa kumudu kusimama kwa uume pale anapohitaji kufanya mapenzi au kuwa na hisia za kimapenzi.Ila ni tasa anaweza kuwa uume wake unasimama vizuri ila akashindwa kusababisha mimba
ZIPI SABABU ZA TATIZO HILI LA UTASA?
Utasa husababishwa na sababu zifuatazo;
- Maambukizi kwenye makende/mapumbu(testicular infections) kitaalamu tatizo hili huitwa Orchitis.Tatizo hili mara nyingi husababishwa na virusi wanaojulikana kama Mumps japo wadudu wengine kama bakteria huweza kusababisha.
- Makende kuwa ktk jotoridi la juu(overheating).Kwa kawaida mbegu za kiume huzalishwa katika jotoridi lisizozidi sentigredi 35(35 celcius centigrades) hivyo jotoridi likizidi maeneo ya kiwanda cha mbegu zakiume hupelekea kiwanda kupunguza uzalishaji wake.Watu walio ktk hatari hii ni watu wanaovaa nguo nyingi,nzito na zenye kubana na watu wanaoendesha magari(masafa marefu) na waendesha pikipiki pia(bodaboda).
- Kansa ya makende(testicular cancer).
- Matatizo ya mbegu za kiume kurudi nyuma/juu ndani ya kibofu badala ya kumwagika nje ya uume(retrograde ejaculation) na pia tatizo la manii kushindwa kutoka nje kutokana na kuzuiwa au kufungika kwa mirija ya kupitiza mbegu za uzazi(obstructed ejaculation).Mtu mwenye tatizo la retrograde ejaculation hupata mkojo unaokuwa na rangi nyeupe kama maziwa kutokana na mbegu za uzazi kuwa ktk kibofu cha mkojo.
- Makende kushindwa kushuka sehemu yake na kubakia tumboni wakati wa maendeleo ya mtoto tumboni kabla ya kuzaliwa (undescended testicles) kitaalamu Cryptoorchidism.Kwa kuwa makende yanakuwa ktk jotoridi kubwa hivyo kupelekea mbegu kushindwa kutengenezwa.Pia mtu mwenye tatizo hili yupo ktk hatari ya kupata kansa ya matende(testicular cancer).
- Matatizo ya kurithi(genetic abnormalities) mfano tatizo linalofahamika kitaalamu kama Klinefelter’s syndrome.
- Tatizo la kukosa au kuwa na kiwango cha chini cha kichochezi kinachoitwa Testosterone.Kichochezi hiki ndicho kinachosababisha mabadiliko ya hali na maumbile ya kiume(masculine).Pia kichochezi hiki kinapatikana kwa kiasi kidogo ktk mwili wa mwanamke lakini kwa mwanamke hutumika kumpatia hamu ya tendo la ndoa(Libido).
- Tatizo la mishipa ya damu inayotoa damu kwenye mapumbu(testicular vein) kutanuka na kujikunjakunja,kitaalamu tatizo hili linajulikana kama Varicose vein.Ktk tatizo hili damu hutuama na kupelekea kuongezeka kwa jotoridi(overheat) ktk kiwanda cha kutengenezea mbegu za kiume hivyo kupunguza uzalishaji wake.Tatizo kwa kiasi kikubwa hutokea upande wa kulia na kufanya pumbu la upande la kulia kuwa kubwa na lenye kuuma sana.
- Upasuaji unaohusisha makende(testicular surgery) mfano upasuaji wa kuondoa na kutibu tatizo la busha(kama ikifanyika vibaya).
- Mionzi(Radiations) kama X-ray n.k.Mionzi hubadilisha na kuathiri mfumo mzima wa utengenezaji wa mbegu za kiume kuliko kwa mwanamke,hivyo tujiepusha kuwa karibu na mionzi au kupigwa picha za x-rays zinazohusisha via vya uzazi mara nyingi labda iwe na ulazima sana kitaalamu.
- Matatizo ya kiafya kama upungufu wa wingi wa damu(anemia),kisukari cha kupanda(diabetes mellitus) na matatizo ya tezi shingo(thyroid diseases).
- Matumizi ya dawa kama Sulfasalazine n.k
- Matumizi ya muda mrefu wa acetaminophen/panadol wakati wa ujauzito hupelekea mtoto atakayezaliwa(kama ni wa kiume),kuzaliwa na tatizo na upungufu wa uzalishaji wa mbegu za kiume.
- Matumizi holela ya dawa za kuongeza nguvu michezoni(anabolic steroids) hupunguza uzalishaji wa mbegu za kiume.
- Matumizi ya mihadarati kama bangi,cocaine,sigara na ulevi wa kupindukia hupunguza uwezo wa kusababisha mimba kwa kupunguza kiwango cha mbegu za kiume.
NIFANYE NINI KUJUA KAMA NINA TATIZO HILI?
Naam!ni rahisi fika hospitalini mara tu utapoingiwa na mashaka au juhudi za kupata mtoto kushindikana.Ongozana na mwenza wako kuelekea hospitali ili kujua kama tatizo lipo upande upi(mume au mke).
Vifuatavyo ni vipimo vinavyoweza kutimika kufahamu kama kuna tatizo upande wa mwanaume
- Sperm analysis kujua kiwango cha mbegu za kiume(sperm count/concentration),rangi(colour),uwezo wa mbegu za kiume kuogelea kwenye mji wa mimba wa mwanamke(sperm motility) bila kusahau ubora wake(sperm quality)
- Blood test kipimo hiki hutumika kupima kiwango cha kichochezi kiitwacho(testesterone).
- Ultrasound(USS) Kipimo hiki kitasaidia kuangalia kama kuna tatizo lolote ktk via vya uzazi vya mwanaume hasa mirija ya kupitisha mbegu za kiume.
NINI TIBA YA TATIZO LA UTASA?
Utasa unaweza kutibika au kushindikana kutibika kutokana na sababu iliyopelekea tatizo hilo.Tiba inaweza kuwa kubadilisha mfumo wa kuishi kutokana na maelekezo ya daktari,dawa za kutumia na lishe au upasuaji(kutegemeana na upatikanaji wa vifaa tiba na wataalamu). Kwa mawasiliano no 0747-630067 / 0782-782720
No comments: