Header Ads

Mambo 5 ya kushangaza yanaokusababisha kuongeza kilo


Watu wanadhani ni lazima mtu awe na ari ya kupambana na unene au auzito wa mwili, lakini utafiti wa afya unaonyesha kwamba sio hilo tu.
Haya ni mambo matano ya kusahngaza yanayokusababisha kuongeza uzito wa mwili kama yalivyofichuliwa na makala maaluma ya BBC yanayoangazia utafiti wa sayansi kuhusu unene wa kupindukia.
1. Bakteria ndani ya Utumbo
Wanasayansi wanaamini kwamba utofauti wa kilo za watu unatokana na bakteria za mwilini zaidi kwa wanaoishi ndani ya utumbo.
Kwa mfano kwa pacha wawili waliofanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya miaka 25 ambao mmoja ana kilo 41 kumshinda mwenzake, matokeo ya utafiti wa vinyesi vyao umedhihirisha kwamba kwa pacha aliye mwembamba alikuwa na bakteria za aina tofuati, huku mwenziwe ambaye ni mnene kumshinda ana aina fulani tu ya bakteria hizo ndani ya utumbo wake.
'Kila kunapozidi kuwa na aina tofuati ya bekteria ndipo mtu huwa mwembamba'. anasema Profesa Tim Spector kutoka Uingereza.
Iwapo wewe ni mnene sana , basi huenda huna aina nyingi za bakteria kama inavyostahili katika utumbo wako, anasema profesa huyo ambaye amegundua mtindo wa aina hiyo katika utafiti wa watu 5000.
Bakteria wanaopatikana katika utumbo wa mwanadamu

Kila unapokula lishe bora yenye afya, imedhihirika kuunda aina tofuati za bakteria hao wa ndani ya utumbo.
2. Jini tunazorithi
Je ni kwanini kuna watu wanakula lishe bora lakini bado hawapunguzi unene huku wengine hata hawataabiki kuhusu chakula wanaochokula au kufanya mazoezi na hawaongezi unene?
Wanasayansi katika chuo kikuu cha Cambridge wanaamini kati ya 40-70% ya athari ya uzito wa miili ya watu unatokanana utofuati wa jini ndani ya mwili.
3. Je ni saa ngapi?
Kuna ukweli katika msemo wa zamani: Kula kiamsha kinywa kama mfalme, chakula cha mchana kama Lodi na cha usiku kama masikini, lakini sio kwa sababu unazozifikiria.
Mtaalamu wa kuhusu masuala ya unene wa mwili Dkt James Brown anasema kila tunapokula kuchelewa , basi tuna nafasi kubwa ya kuongeza kilo mwilini.
Na sio kwasababu usiku ni muda wa mapumziko na hatuna shughuli nyingi, kama inavyoaminika na wengi, lakini ni kwasababu ya saa zetu za ndani ya miili.
Ni kwasababu hiyo unaona watu wanaofanya kazi kwa saa fulani au masaa marefu huenda wakakabiliwana changamoto maalum ya kukaa na njaa kupunguza uzito.
Inapofika usiku, miili yetu hupata shida kusaga chakula - mafuta na sukari kwahivyo unapokula chekula chenye mafuta kabla ya saa moja suiku huenda kukakusaidia kupunguza kilo au kukusaidia kukuzuia kuongeza kilo mwilini.
4. Kuudanganya ubongo wako
Kuna namna tofuati za kubadili namna tunavyokula chakula, na sio tu kutegemea kuhesabu kiwango cha kalori ndani ya chakula tunachokila.
Kwa mfano, kuondosha vishawishi ni bora zaidi kuliko kutegemea ari yako binafsi.
Kwa hivyo usiweke vitamu tamu jikoni kwako - badala yake weka bakuli la matunda.
Usikae na pakiti nzima ya biskuti huku ukiangalia TV, weka kiwango unachotaka kula kwenye sahani na usiongeze zaidi ya hapo.
Kuna mtindo wa kula bila ya kufikiria kuhusu unachokula, kwaivyo unapijimia chakula na kula kwa kiwango kidogo kidogo kunaweza kuzuia mtu kula kalori za ziada pasi kutambua.
5. Homoni
Kubadilika kwa hamu ya kula chakula kunadhibitiwa na homoni ndani ya mwili na imegunduliwa kwamba upasuaji wa kuufunga utumbo - maarufu bariatric surgery - kunasaidia kuunda homoni nyingi zinazotufanya kuhisi kushiba kuliko homoni zinazotufanya kuhisi njaa ambazo hupungua.
Lakini ni upasuaji mkubwa unaohusu kupunguza ukubwa wa tumbo kwa hadi 90% na hufanyiwa watu wenye BMI ya 35 au zaidi pekee.
Mgonjwa hudungwa mchanganyiko wa homoni 3 katika sindano kila siku kwa wiki nne.
"Mtu hahisi njaa sana, wanakula chakula kidogo, na wanpunguza kilo kati ya 2-8kg katika muda wa siku 28 ," anasema mtaalamu Dkt Tricia Tan.
Iwapo dawa hiyo ni salama kutumiwa, mpango ni kuhakikisha inatumika hadi mgonjwa anafikia uzito ulio sawa ki afya.

No comments:

Powered by Blogger.