Header Ads

UKWELI KUHUSU MAUMBILE MADOGO YA MWANAUME NA KUFIKA KILELENI

Ernst Grafenberg, Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake aliyegundua G-spot, sehemu ya kike inayoelezwa kuwa na msisimko wa kipekee kuliko nyingine  
Kwa Muhtasari
Afya ya uzazi inahitaji uume wa ukubwa wa kidole cha mwisho cha mkono ili kumfikisha mwenza kileleni



Kawaida katika jamii taarifa potofu huwa na nguvu kuliko ukweli uliothibitishwa kisayansi. Jambo hili ndilo limenilazimu kutoa tena taarifa ya ufahamu kuhusu uhusiano wa maumbile ya kiume na kumfikisha kileleni mwanamke katika tendo la ndoa.
Baadhi ya wanaume wamekuwa wakiishi kwa hofu na kutojiamini katika uhusiano wakihisi kuwa wana uume mdogo usioweza kuwaridhisha wenza wao.
Ieleweke kwamba sayansi ya maumbile ya binadamu na afya ya uzazi inathibitisha kuwa unahitaji tu uume wa ukubwa wa kidole cha mwisho cha mkono ili kumfikisha mwenza kileleni.
Hii ni kwa sababu wanawake wengi sehemu inayowapa msisimko wa kipekee kuliko mahali popote ipo ndani kidogo sawa na urefu wa kidole kidogo cha mwisho cha mkono.
Hofu ya wanaume inapanda kila siku kutokana na kuzagaa matangazo mitandaoni, matabibu wasio na sifa wanaojitangaza katika vipeperushi na magazeti kuwa wanazo dawa na vifaa vya kuongeza ukubwa wa uume.
Ukweli ni kuwa hakuna hata njia moja ambayo ni salama wala iliyoidhinishwa na Wizara ya Afya, hata zile za nje ya nchi si salama kwa watumiaji na hazileti matokeo mazuri.
Taarifa za kitafiti kwa njia zinazotumika kuongeza maumbile ya kiume zimeandikwa katika majarida ya Science Today, Men’s Health na British Journal of Urology International na kuelezwa njia hizo si salama.
Tafiti zinaonyesha asilimia 85 ya wanawake wanaridhika na urefu na upana wa maumbile ya uume wa wenza wao, ingawa wanaume wenyewe hawana uhakika wa jambo hilo.
Vilevile asilimia 45 ya wanaume wanaamini kuwa maumbile yao ni madogo. Japokuwa tafiti mbalimbali zilikuja na hitimisho kuwa wastani wa urefu wa uume kabla ya kusimama ni kati ya sentimeta 7 hadi 10 au inchi 2.8 hadi 3.9 na urefu unapimwa kuanzia katika shina la uume mpaka katika kichwa.
Wakati kipimo cha mzunguko wa uume hupimwa ukiwa tepetepe ni kati ya sentimeta 9 hadi 10 au inchi 3.5 mpaka 3.9.
Wakati urefu wa uume unapokuwa umesimama ni kati ya sentimeta 12 hadi 16 au ichi 4.7 mpaka 6.3 na mzunguko wa uume ukiwa umesimama ni kati ya sentimeta 12 au inchi 4.7.
Hata hivyo, tafiti zinaonyesha wanaume wenye unene uliopitiliza na umri mkubwa wengi wao wana uume mfupi ukiwa umesimama, lakini si sababu ya wao kushindwa kuwafikisha wenza wao kileleni.
Pia ifahamike kwamba maumbile ya uume yanatofautiana kati ya jamii moja na nyingine, bara moja na lingine. Mfano wanaume wanaotokea Bara la Asia wana maumbile madogo ukilinganisha na wanaume wa Bara la Afrika.
Pamoja na hilo, ifahamike kwamba wanawake wengi hawajali urefu na upana wa uume wa wenza wao. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kufika kileleni na kuridhika kwao si lazima kumuingilia, bali wanaweza kusisimuliwa kwa kutomaswa tu na kuridhika.
Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Ernst Grafenberg mwenye asili ya Ujerumani ndiye mgunduzi wa sehemu ya kike inayoelezwa kuwa na msisimko wa kipekee kuliko nyingine yoyote. Sehemu hiyo inajulikana kama G-spot ambayo ipo sentimeta 5.1 hadi 7.9 au nchi 2 mpaka 3 tu kuanzia nje ya uke kuingia ndani.
Hivyo unaweza kuwa na uume mdogo lakini ukamfikisha kileleni mwenza wako kwa sababu sehemu hiyo huweza kusisimuliwa hata na uume mdogo.
Kwa ugunduzi huu wa Grafenberg, mwanaume unayejihisi kuwa na maumbile madogo unapaswa kujiamini kwani kukata tamaa, hofu na mawazo makali hupunguza hamu ya tendo na hivyo kushindwa kulianza tendo lenyewe.
Ushauri, usitumie madawa ya mtaani kwani yana madhara na hayatibu tatizo badala yake fika mapema katika huduma za afya zinazotambulika na Serikali kwa ushauri zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.