MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA
Namna Maumivu Wakati Wa Kukojoa Yanavyotokea
Maumivu haya hutokana na kuchubuka kwa njia ya mkojo. Maumivu huwa yanakuwa ya kuungua wakati mkojo unatoka. Yanaweza kuwa wakati wote unakojoa, mwanzoni au mwishoni mwa kukojoa.
Pia yanaweza kuambatana na dalili kama homa, kuokwa na usaha au uchafu sehemu za siri, kutokwa mkojo wenye damu damu na maumivu chini ya kitovu.
Maumivu haya hutegemea na chanzo cha ugonjwa unaoleta dalili hii. Baadhi ya sababu za maumivu wakati wa kukojoa ni:
Maambukizi ya Njia ya Mkojo (Urinary Tract Infection – UTI)
Ugonjwa huu huleta maumivu kama ya kuungua kwenye njia ya mokojo. Pia maumivu yanaweza kufika mpaka chini ya kitovu wakati wa kukojoa. Dalili nyingine zinazoweza kuambatana na hali hii ni homa, kukojoa mara kwa mara, kuhisi mkojo hauishi kwenye kibofu na maumivu ya mgongo.
Magonjwa ya Zinaa
Huleta maumivu wakati wa kukojoa hasa kwa wanaume, maumivu kama ya kuungua wakati mkojo unatoka. Dalili nyingine zinazoweza kuambatana na magonjwa haya ni kutoa uchafu kama usaha sehemu za siri, maumivu chini ya kitovu na homa.
Kichocho
Kichocho husababisha maumivu wakati wa kukojoa ikiambatana na kutoa mkojo wenye damu.
Magonjwa mengine yanayoweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa ni:
Saratani ya kibofu cha mkojo
Mawe ya figo
Kuumia wakati kufanya mapenzi
mawasiliano 0765203999
No comments: