Header Ads

Ujue kwa Undani Ugonjwa wa KIFUA KIKUU (TUBERCULOSIS, TB)

Ni ugonjwa ambao unasaaishwa na bakteria/kimelea aitwae MYCOBACTERIUM TUBERCULOSIS(MTB). Huu ugonjwa unashika namba mbili duniani katika magonjwa yote yanayoambukiza kwa kupoteza Maisha ya watu.Namba moja kwa kuua watu ni HIV.Huyu bakteria huishi kwa binandamu tu kabla ya kumuingia mtu mwingine(natural reservoir).ikumbukwe watu wengi karibia theluthi moja ya watu wote duniani wameambukizwa TB sema sasa uwezo wake kusababisha madhara kwa awali unakua mdogo kutokana na uimara wa kinga ya mwili.kuna baadhi ya mambo ambao huweza kupelekea maambukizi ya TB yawe Makali na kuleta madhara mapema ,baadhi ya mambo hayo ni kama mtu aliepata TB awe pia na maambukizi mengine hasa ya HIV,au awe na magonjwa ya muda mrefu kama kisukari,saratani nk.kitakwimu katika kila mwaka watu wapatao MILIONI 6.3 hupata maambukizi mapya ya TB,vile vile watu wapato MILIONI 1.3 wenye TB pekee bila ya kua na HIV hupoteza Maisha kila mwaka,kwa wale wenye HIV na TB kwa pamoja idadi ya vifo ni vingi karibia mara mbili ya hao ambao hawana HIV.

NAMNA YA KUWEZA KUAMBUKIZWA TB
Njia pekee ya kuweza kupata maambukizi ya TB ni kupitia KUVUTA HEWA AMBOYO INA HAO BAKTERIA WA TB,hao bakteria hukaa au kuingia kwenye hewa pale mwathirika mwenye TB anapokohoa au kupiga chafya.ifahamikwe kwamba mtu yeyote anaweza kupata TB,iwe mwanaume,mwanamke,mtoto,mzee,mwanamke mjamzito nk

MAKUNDI YALIO KATIKA HATARI YA KUPATA TB
Sasa kuna baadhi ya makundi ya Fulani ya watu na maeneo Fulani ambayo yapo katika hatari kubwa ya kupata TB endapo akitokea mmojawapo awe na hayo maambukizi.
baadhi ya hayo maeneo ni:- KWENYE MISONGAMANO MIKUBWA YA WATU KAMA:-
MASOKONI.
MAKANISANI
MISIKITINI
KWENYE MIKUTANO YA HADHARA
KWENYE MAANDAMANO
KWENYE KUMBI ZA STAREHE
MASHULENI
VIWANJANI(MASHABIKI)
KAMBI ZA WANAJESHI
MAGEREZANI
KWENYE MADALADALA
MAKAHABA
MASHOGA
WAFUNGWA
WATUMIA MADAWA YA KULEVYA.


NAMNA TB INAVYOATHIRI MWILI(NATURAL HISTORY OF TB)
Pale mtu anapovuta matone ya hewa(aerosol) yenye vimelea vya TB,huyo kimelea huenda moja kwa moja hadi kwenye mapafu,akifika kwenye mapafu mambo makuu manne yanaweza kutokea,ambayo ni:-
Kinga ya mwili kupambana na kumuondoa huyo kimelea mara moja.
Kushambuliwa na kupata dalili zote za TB mwanzoni mwa maambukizi (primary disease).
Kimelea kudhoofishwa kidogo na kuhifadhiwa kwa muda bila kuleta madhara yeyote(latent infection).katika hatua hii ikumbukwe kwamba kimelea hajafa bali ametulia zake tu mpaka pale kinga ikidhoofika na ye ndo anaanza mashambulizi.
Kimelea alieficha kuamka tena na kuanza mashambulizi(reactivation)
Sasa ikumbukwe kwamba WATU WENGI TUPO KWENYE LATENT INFECTION na endapo kukitokea mtikisiko wowote wa kinga ya mwili basi mashambulizi ya huyu kimelea huanza upya.kwa kawaida huchukua muda wa hadi miaka 5 hadi 7 kwa mtu mwenye kimelea cha TB tu bila kua na maambukizi mengine kama HIV kupata TB na madhara yake yote.Uwepo wa TB na HIV kwa wakati mmoja hupelekea TB kushamiri kwa haraka na mwili kudhoofu haraka tofauti na mtu ambae ana TB tu bila ya HIV.
Sasa naenda kuelezea kwa kifupi haya mambo ambayo hutokea kwenye mwili punde tu kimelea cha TB kiingiapo
Hii hutokea tu kama mwathirika ana kinga imara ,vile vile hutegemea idadi ya vimelea alowavuta.kama kinga yako iko vizuri kwa maana huna HIV,KISUKARI,SARATANI NK na umevuta vimelea wachache basi mwili utatumia seli zake za kinga ili kupambana na kumuua huyu kimelea mara moja.na sababu hii ni mojawapo ya sababu ambayo inasemea kwanin watu wengi hawapati TB ili hali wapo maeneo hatarishi 


DALILI ZA KIFUA KIKUU(TB)
Kama wote tunavyofahamu TB inashambulia sana mapafu kwa asilimia kubwa,vilevile kuna TB ya sehemu zingine kama TB ya matezi(TB adenitis),TB ya uti wa mgongo( spine TB),TB ya Ngozi(lupus vulgaris),TB ya moyo na sehemu zake(TB pericarditis),TB ya ubongo(TB meningoencephalitis),TB ya tumbo na utumbo hasa hasa kwa wafugaji na wapenda maziwa nk
Ifahamike kwamba TB kwa asilimia nyingi huanzia kwenye mapafu, kama TB imekaa muda mrefu bila matibabu inasambaa na kushambulia sehemu zingine kama nlizotaja hapo juu.
Watu wenye upungufu wa kinga mwilini aidha HIV, kisukari,saratani nk wanakuaga na TB inayoshambulia maeneo mengi sana na wanakua katika nafasi kubwa ya kufa kwa sababu ya TB.
UKIWA NA DALILI HIZI JUA UNAEZA KUA NA TB NA CHUKUA HATUA MAPEMA 
1) KUKOHOA ZAIDI YA WIKI 2 (wakati mwingine kutoa makohozi yenye damu) 
2) KUTOKWA NA JASHO JINGI USIKU NA UNAKUA KAMA UMEMWAGIWA MAJI ZAIDI YA WIKI 2 
3) KUA JOTO KWA ZAIDI YA WIKI 2 
4) KUPUNGUA UZITO KUSIPOELEWEKA

Hizo hapo juu ndo dalili kuu za TB,kama wajiona una dalili mojawapo au kuna mtu unamfahamu anayo nenda au mshauri aende hospitali ili kupata matibabu.
TB INATIBIKA VIZURI SANA NA INAPONA VIZURI KAMA UKITUMIA DAWA INAVYOTAKIWA

No comments:

Powered by Blogger.