Fahamu zaidi namna mboga-mboga na matunda zinavyosaidia kuimalisha mwili.
Baadhi ya mboga-mboga na matunda yenye
rangi nyekundu, zambarau na hata kijani
kibichi na njano huwa na virutubisho kwa
wingi zaidi hasa madini na vitamini. Baadhi ya
virutubishi hivi huchangia sana kuongeza
damu. Mfano mmea wa choya (rosela) ambao
una rangi nyekundu, umeonekana kuwa na
madini chuma kwa wingi ambayo huchangia
kuongeza damu. Lakini haimaanishi kuwa,
kila chakula au kinywaji chenye rangi hizo huongeza damu.
Hata hivyo kuchanganya mboga na matunda
ya rangi mbalimbali huongeza ubora wa chakula unachokula. Hivyo ni vizuri kujaribu
kuchanganya rangi kadiri inavyowezekana.
Baadhi ya mboga-mboga au matunda
vinaweza kutumika kutengeneza supu au
v i n y w a j i .
Watu wengi hudhani kwamba vinywaji vya
rangi ya zambarau au nyekundu vyenye ladha
bandia ya matunda mfano “black curre n t ”
huongeza damu. Hii si kweli; vinywaji hivi mara nyingi hutengenezwa na maji, sukari,
rangi na ladha bandia, hivyo si vizuri kuvitumia na siyo bora kwa afya zetu.
No comments: