Header Ads

JINSI YA KUKABILIANA NA FANGASI WA MIGUUNI

Tokeo la picha la dawa ya fangasi miguuni

MARA nyingi ngozi ya miguuni hasa katika ngozi ngumu ya nyayo na katikati ya vidole, ndizo zinazopatwa sana na vimelea wa fangasi ambao husumbua watu wengi.  

Uwapo wa unyevunyevu, joto na giza huwa ni mazalia mazuri ya fangasi wa miguuni. Wanaume ambao wako katika hatari ya kupata fangasi za miguuni ni wale wenye dosari ya nyayo ya miguu kuwa na kiasi kikubwa cha tezi zinazotoa jasho nyayoni.

Vilevile wenye kinga dhaifu, wanaougua kisukari, wanaoishi maeneo yenye joto kali na wale wanaovaa viatu muda mwingi. Maambukizi haya yanaweza kuwa chanzo cha kupata fangasi maeneo mengine ikiwamo sehemu za siri, viganja vya mikono na mwili mzima.

Uwapo wa fangasi miguuni unaweza pia kumhatarisha mwathirika kuvamiwa na bakteria juu ya ngozi ambao wakipenya kwa ndani ya ngozi huleta madhara. Vimelea wa fangasi ni mojawapo wa vimelea wanaoweza kusambaa na kumpata mwanadamu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kugusana na vitu vilivyotumiwa na mwenye vimelea wa fangasi.

Katika maisha ya kila siku mara nyingine watu huweza kuvaliana soksi na viatu; hii ni mojawapo ya njia zinazoweza kueneza maambukizi ya fangasi wa miguuni kwa wanaoishi mazingira ya pamojaDALILI
Dalili kubwa ya fangasi ni muwasho unaokulazimisha kujikuna na kujihisi raha au utulivu unapojikuna, harufu nzito ya kuoza katika miguu hasa uvuapo viatu, kumomonyoka ama kulika kwa ngozi yenye fangasi miguuni. Pia kuvuja kwa majimaji yenye kuteleza na harufu nzito, maumivu au kuhisi kuchomachoma baada ya kuchubuka na pia mara nyingine kuhisi kuwaka moto.

Ugunduzi wa fangasi wa ngozi ya miguu ni rahisi, huhitajiki kwenda maabara, wahudumu wa afya wanaweza kugundua kwa kupata historia ya dalili na kutazama kwa macho. Mara nyingine unaweza usihitaji kupewa dawa za kukabiliana na fangasi wa miguu, elimu ya afya inaweza kukubadili tabia na ukadhibiti fangasi wa ngozi ya miguuni bila dawa japokuwa dawa hasa za poda au cream zipo.

NJIA YA KUKABILI FANGASI
Moja ya njia rahisi za kukabiliana na kujikinga na fangasi ni kubadili mienendo ya kimaisha ikiwamo kupenda kuwa msafi wa kimwili pamoja na kufua nguo zinazovaliwa ikiwamo soksi ambazo wengine huzivaa kwa muda mrefu bila kuzifua.

Tumia soksi zenye asilimia nyingi ya pamba ili kuweza kunyonya jasho la miguuni, kutumia kitambaa safi au taulo dogo kwa ajili ya kukaushia maji baada ya kuoga au unapotoka kazini, matembezini na mchezoni. Mara tu baada ya kutoka katika shughuli zako vua viatu vya kufunika na tumia viatu vya wazi, kausha kwa kitambaa kikavu maeneo ya miguuni katika upenyo wa vidoleni.DALILI
Dalili kubwa ya fangasi ni muwasho unaokulazimisha kujikuna na kujihisi raha au utulivu unapojikuna, harufu nzito ya kuoza katika miguu hasa uvuapo viatu, kumomonyoka ama kulika kwa ngozi yenye fangasi miguuni. Pia kuvuja kwa majimaji yenye kuteleza na harufu nzito, maumivu au kuhisi kuchomachoma baada ya kuchubuka na pia mara nyingine kuhisi kuwaka moto.

Ugunduzi wa fangasi wa ngozi ya miguu ni rahisi, huhitajiki kwenda maabara, wahudumu wa afya wanaweza kugundua kwa kupata historia ya dalili na kutazama kwa macho. Mara nyingine unaweza usihitaji kupewa dawa za kukabiliana na fangasi wa miguu, elimu ya afya inaweza kukubadili tabia na ukadhibiti fangasi wa ngozi ya miguuni bila dawa japokuwa dawa hasa za poda au cream zipo.

NJIA YA KUKABILI FANGASI
Moja ya njia rahisi za kukabiliana na kujikinga na fangasi ni kubadili mienendo ya kimaisha ikiwamo kupenda kuwa msafi wa kimwili pamoja na kufua nguo zinazovaliwa ikiwamo soksi ambazo wengine huzivaa kwa muda mrefu bila kuzifua.

Tumia soksi zenye asilimia nyingi ya pamba ili kuweza kunyonya jasho la miguuni, kutumia kitambaa safi au taulo dogo kwa ajili ya kukaushia maji baada ya kuoga au unapotoka kazini, matembezini na mchezoni. Mara tu baada ya kutoka katika shughuli zako vua viatu vya kufunika na tumia viatu vya wazi, kausha kwa kitambaa kikavu maeneo ya miguuni katika upenyo wa vidoleni.0765203999

No comments:

Powered by Blogger.