Header Ads

Ugonjwa wa Homa ya Uti wa Mgongo kwa Watoto

Tokeo la picha la madhara ya uti

Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ni nini?
Ugonjwa wa uti wa mgongo ni ugonjwa unaotokea iwapo utando unaofunika uti wa mgongo na ubongo umepatwa na maambukizi na kuvimba. Ugonjwa huu unakua kwa haraka na ni hatari sana.
Ugonjwa wa uti wa mgongo unasababishwa na bakteria au virusi:
  • Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria: Hii ni aina ya maambukizi iliyo hatari sana. Inaweza kuhatarisha maisha na kusababisha ulemavu kama ukiziwi au uharibifu wa ubongo. Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria ambao haujatibiwa unasababisha kuenea maambukizi haraka ndani ya damu (septicaemia), ambayo ni hatari sana.
  • Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na virusi una madhara madogo ukilinganisha na ule unaosababishwa na bakteria. Ingawa dalili kama mafua yanaweza kumsumbua mtoto lakini ana uwezo wa kupona bila matibabu ndani ya siku saba mpaka 10.
Jinsi homa ya uti wa mgongo inavyoenezwa?
Bakteria na virusi vinavyosababisha ugonjwa huu vinaishi ndani ya pua,koo na utumbo wa watu. Vyenyewe haviwezi kusababisha athari. Ugonjwa wa uti wa mgongo unakua pale virusi na bakteria vinaposhambulia na kuambukiza utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo.
Ni nadra sana kwa mtu aliye na ugonjwa huu kuambukiza. Ingawa watu wanaoishi nyumba moja na mtu mwenye ugonjwa huu uliosababishwa na bakteria wanapatiwa antibaiotiki kama tahadhari.
Mtoto wako anaweza kupata bakteria na virusi kwa:
  • Kuguswa au kupigwa busu.
  • Watu kupiga chafya na kukohoa karibu yake.
  • Kuchangia vyakula vya kula na kunywa na vitu vingine binafsi kama msawaki.
Unaweza kumlinda mwanao kwa kufuata usafi mzuri. Safisha mikono baada ya kukohoa, kupiga chafya au kupenga kamasi, au baada ya kutoka chooni au kubadilisha nepi.
Dalili na ishara za ugonjwa wa uti wa mgongo
Dalili za awali za ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria, ambao ni hatari sana ni ngumu kuonekana. Dalili zinaweza kuonekana kama za mafua au kuumwa tumbo ambazo ni kama kuwa na homa. Lakini dalili za ugonjwa huu zinatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine na zinaweza kuonekana katika utaratibu tofauti
Ukiona dalili zifuatazo mkimbize mtoto hositali haraka:
  • Mtoto ameota upele usiopotea, upele unaoanza kama vipele vidogo vyekundu vinavyokua kwa namba na ukubwa na kubadilika kuwa zambarau-nyeusi.
  • Mtoto kukakama na kushindwa kutulia,asiye na furaha.
  • Analia kwa sauti isiyo kawaida.
  • Ana baridi miguuni na mikononi.
  • Anatapika na kukataa kula.
  • Shingo na mwili kukakama.
  • Hapendi mwanga mkali.
  • Kuhema kwake kumebadilika,wakati mwingine haraka au taratibu kuliko kawaida.
  • Mgongo kuuma.
  • Tumbo kuvimba.
  • Mshtuko wa moyo.
Jinsi ugonjwa wa uti wa mgongo unavyotambuliwa?
Hospitalini daktari wa watoto atamkadiria mwanao haraka, akiangalia dalili na ishara za ugonjwa. Daktari atahitaji kuchukua sampluli ya damu ya mwanao au kimiminika kutoka kwenye uti wa mgongo kuangalia kama ana ugonjwa huu uliosababishwa na bakteria au virusi.
Daktari atachukua sampluli ya utando wa uti wa mgongo kwa kumchoma mtoto sindano nyembamba katika sehemu ya chini ya uti wa mgongo na kutoa kimiminika kutoka kwenye tishu zinazozunguka uti wa mgongo. Kimiminika hicho kinatumwa maabara kupimwa.
Inaweza kuchukua dakika 45 kwa daktari kuchukua kimiminika hicho kwenye uti wa mgongo wa mwanao. Inaweza kuhuzunisha kumuona mwanao akipitia utaratibu huo mkubwa wa kimatibabu. Ukiona unashindwa kuangalia toka nje kidogo atabaki katika mikono salama usiwe na wasiwasi.
Ikiwa daktari atahisi mwanao ana maambukizi yaliyosababishwa na bakteria atakupatia antibaiotiki za mwanao mapema bila kusubiria matokeo ya vipimo. Daktari anaweza kuomba mwanao afanyiwe kipimo cha “CT” kama kinapatikana hositalini kinachopiga picha za muonekano wa ndani wa ubongo kuangalia kama kama kuna uvimbe ndani ya ubongo.
Matibabu ya ugonjwa wa uti wa mgongo
Matibabu ya ugonjwa huu yanategemea na aina gani ya ugonjwa wa uti wa mgongo alionao mtoto:
Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na bakteria
Aina hii inahitaji matibabu ya haraka ya antibaiotiki ndani ya hospitali. Kama mtoto anaumwa sana, anaweza kuwekwa katika wodi za wagonjwa mautiuti.
Matibabu ya mwanao yanategemea na kiasi gani mwanao anaumwa na dalili gani anazo. Matibabu ya aina hii ya ugonjwa wa uti wa mgongo yanajumuisha:
  • Antibaiotiki zinazotolewa kwa njia ya drip katika mishipa ya mwanao kuhakikisha ana dozi ya mara kwa mara.
  • Vimiminika vitakvyomsaidia mtoto kuwa na maji ya kutosha mwilini
  • Hewa ya oksijeni
  • Matibabu ya “steroid” yanayosaidia kupunguza uvimbe kuzunguka ubongo.
Ugonjwa wa uti wa mgongo unaosababishwa na virusi
Maambukizi yanayosababishwa na virusi hayaitaji antibaiotiki, hivyo mwanao atahitaji kupumzika na kuangaliwa zaidi. Mtoto anaweza kuumwa kichwa, ananung’unika bila kuacha na kuchoka, na anakataa kula. Atapona ndani ya siku 10,kwa sasa hakikisha:
  • Anakunywa  maji mara kwa mara
  • Unampatia “paracetamol” za watoto kupunguza maumivu ya kichwa.
  • Hakikisha mazingira yanayomzunguka ni tulivu.
Watoto wachanga wanaweza kupata ugonjwa huu?
Ndio. Watoto waliozaliwa kabla ya wiki 37 wana uzito duni, wana hatari za kupata ugonjwa wa uti wa mgongo papo kwa hapo.
Ikiwa mama alikua na ugonjwa wa listeria akiwa na ujauzito na akampatia mtoto kupitia plasenta, inaongeza hatari za mtoto kuzaliwa na ugonjwa huu papo kwa hapo au kuupata baada ya kuzaliwa.0765203999

No comments:

Powered by Blogger.