Header Ads

MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI.

Tokeo la picha la maumivu makali wakati wa hedhi

MAUMIVU WAKATI WA HEDHI HII NI HALI YA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI, INAHUSISHA VIUNGO VYA UZAZI NA MWILI KWA UJUMLA AMBAPO KITAALAMU INAITWA “ GYNECOLOGICAL MEDICAL CONDITION”. TATIZO HILI LINAPOTOKEA MWANAMKE HUATHIRI SHUGHULI ZAKE ZA KILA SIKU. KWA KAWAIDA MWANAMKE ANAPOANZA MZUNGUKO WA DAMU ZAKE ZA HEDHI HUPATA MAUMIVU KIDOGO NA HILI NI KUTOKANA NA HALI YA KUKAMUA AU KUMINYA KIZAZI ILI KUTOA DAMU ILIYOPO NDANI. MAUMUVU HAYA HUWA MAKALI, AU SIO MAKALI SANA. WAKATI MWINGINE HALI HII HUAMBATANA KICHEFU CHEFU, KUHISI MOTO TUMBONI AU MAUMIVU MAKALI YANAYOKUJA NA KUPOTEA.
VILE VILE HALI HII HUSABABISHA DAMU VYINGI KUTOKANA NA KUPOTEZA AU KUTOKA KIDOGOKIDOGO KWA DAMU NDEFU. MAUMIVU YA WAKATI WA HEDHI YAMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAKUU MAWILI, KWANZA NI MAUMIVU YAITWAYO “PRIMAY DYSMENORRHEA” NI MAUMIVU YANAYOWAPATA WASICHANA NA WADOGO AMBAO HAWAJAWAHI KUPATA UJAUZITO AU KUZAA. AINA NYINGINE NI SECONDARY DYSNORRHEA, HII INASABABISHWA NA MAGONJWA YA MFUMO WA UZAZI, AU ENDAPO KUNA KASORO AU ISIYOKUWA YA KAWAIDA NDANI YA KIZAZI AU KWA NJE YA KIZAZI.
CHANZO CHA TATIZO MAUMIVU WAKATI WA HEDHI HUSABABISHWA NA HALI IITWAYO “ ENDOMETRIOSIS” AMBAPO LILE TABAKA LA NDANI YA KIZAZI HUWA NJE YA KIZAZI, VYANZO VINGINE NI UWEPO WA MATABAKA YA KIZAZI AU UVIMBE KATIKA VIFUKO VYA MAYAI NA MATATIZO KATIKA NYONGA, WENGINE WANAOPATA HALI HII NI WALE WANAOTUMIA NJIA YA UZAZI WA MPANGO YA KITANZI. VYANZO HIVI TULIVYOELEZA VINAWAPATA WANAWAKE WATU WAZIMA AU WANAWAKE WALIO KATIKA UMRI WA KUZAA. PAMOJA NA KWAMBA YALE MAUMIVU YA PRIMARY DYSMENORRHEA HUWAPATA ZAIDI WASICHANA WADOGO, LAKINI PIA SABABU HIZI TULIZOZIONA ZINAWEZA KUKUSABABISHIA KUMTOKEA HATA MSICHANA AMBAYE HAJAWAHI KUZAA.
DALILI ZA MAUMIVU HAYA HUWA CHINI YA KITOVU KUANZIA USAWA WA KITOVU, PIA MAUMIVU HUSAMBAA KUSHOTO AU KULIA NA KUELEKEA MAPAJANI HADI KIUNONI. MAUMIVU HUAMBATANA NA KICHEFU CHEFU, KUTAPIKA NA WAKATI MWINGINE KUHARISHA NA WENGINE KUFUNGA KUPATA HAJA KUBWA, MAUMIVU YA KICHWA NA KIZUNGUZUNGU, MAUMIVU HUWA MAKALI NA WENGINE HUZIMIA. MAUMIVU HUANZA TARATIBU MARA TU BAADA YA KUMALIZA KIPINDI CHA UPEVUSHAJI MAYAI NA HUONGEZEKA KIPINDI CHA DAMU NA KUISHA PALE ANAPO MALIZA DAMU YA HEDHI. ATHARI ZA TATIZO MAUMIVU WAKATI WA HEDHI HUMKWAMISHA MTU ASISHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA KIJAMII, MWANAFUNZI HUSHINDWA KUUDHURIA KIKAMILIFU MASOMO.
TATIZO PIA HULETA GHARAMA KWA MGONJWA NA FAMILIA KATIKA SUALA ZIMA LA MATIBABU. ATHARI YA TATIZO NI UGMBA. MWANAMKE MWENYE MAGONJWA KATIKA MFUMO WA UZAZI AMBAYO YANASABABISHA MAUMIVU ANAWEZA KUTOPATA UJAUZITO NA HATA BAADAYE KUFANYIWA UPASUAJI WA KUONDOA KIZAZI. ANAWEZA KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA NA PIA MAUMIVU YA TUMBO CHINI YA KITOVU YANAWEZA KUWA ENDELEVU, YAANI YAKAWA HAPO SIKU ZOTE KWA HIYO KILA SIKU AKAWA ANALALAMIKA MAUMIVU YA TUMBO CHINI YA KITOVU ENDELEVU ATAPATA MAAMBUKIZI BASI ATATOKWA NA UCHAFU AU MAJIMAJI UKENI AMBAKO HUTOA HARUFU AU MUWASHO. KWA MAALEZO ZAIDI TAFADHALI USISITE KUWASILIANA NASI,
KAMA WEWE UNASUMBULIWA NA TATIZO HILI, AMA NDUGU,JAMAA, MPENZI AU RAFIKI YAKO NA TAFADHALI WASILIANA NASI KWA NAMBA0765203999 UPATE USHAURI SAHIHI WA MOJA KWA MOJA NAMNA YA KUJIKINGA USISUBIRI TATIZO LIKAKOMAA NA UKAPATA UGUMBA AU KUTOWEZA KUZAA KABISA.

No comments:

Powered by Blogger.