Header Ads

TATIZO LA MINYOO

Tokeo la picha la dalili za minyoo
Minyoo ni wadudu hatari ambao huingia tumboni mwa binadamu na kusababisha matatizo kadhaa ya kiafya. Ukubwa wa minyoo tumboni hutofautiana, kuna minyoo yenye urefu wa kuanzia inchi sita hadi inchi 26, ikitegemea imekaa kwa muda gani tumboni.
Kwa kawaida minyoo huingia tumboni kwa njia kuu mbili, ingawa zipo njia nyingine. Minyoo huingia tumboni kwa kula chakula kisicho salama au kwa njia ya ngozi, hasa kwa watu wanaopenda kutembea na kucheza bila viatu miguuni.
Watoto ndiyo wanao ambukizwa zaidi minyoo kwa njia ya ngozi kutokana na tabia yao ya kupenda kucheza bila viatu, tena wakiwa sehemu zisizo safi. Vile vile mtu anaweza kupata minyoo kwa kunywa maji yasiyo salama au kwa kuumwa na mbu, inzi na hata kwa njia ya kujamiana bila kinga.
Inakadiriwa kwamba karibu ya robo ya idadi ya watu duniani wameathiriwa na ugonjwa huu, na hasa umeenea sana katika maeneo ya kitropiki na maeneo yenye hali duni ya usafi.
DALILI ZAKE
Kama idadi ya minyoo ni ndogo, unaweza kutoona dalili za ugonjwa huu. Hata hivyo unaweza kuambatana na:-
+Homa
+kuharisha
+kuvimba tumbo
+kuvimba ini au wengu
+Kichomi cha mara kwa mara
+Kichefuchefu na kutapika minyoo ya duara
+Maumivu ya tumbo
+Kupungua uzito
+Utapiamlo
+Kuonekana dhaifu
+Kula sana,na kusikia njaa baada ya mda mfupi
+Ngozi kupauka
Matatizo mazito yanaweza kujitokeza kama minyoo itahamia sehemu nyingine za mwili kama mapafu, ini, na sehemu nyingine za mwili asa msokoto na kuoza kwa sehemu ya utumbo mdogoambayo hupelekea kifo.
MATIBABU..
Ni muhimu kuzingatia kanuni za usafi,ili kuzuia madhara makubwa ya tatizo ili...
-kwa mtu ambae unauhakika kuwa una minyoo, naweza kukusaidia kwa bidhaa zetu... 0672287991

No comments:

Powered by Blogger.