Header Ads

JINSI YA KUJIKINGA NA FANGASI ZA SEHEMU ZA SIRI.



Fangasi zinaweza kuzuiliwa kwa kiasi kikubwa na ni endapo tu mtu mwenyewe ukiamua kujilinda.Fanya yafuatayo ili kujiepusha na fangasi

1) ACHA KUPIGA UKE DEKI: nawakumbusheni tena kinadada mnafikiri kwamba ili kujiweka msafi sehemu za siri ni lazima UINGIZE KIDOLE UKENI. Mimi nawaambia ukweli na naomba mnielewe kwamba UKE unajisafishaga wenyewe na huna haja kupiga deki kwani ukipiga deki utakua umeharibu ulinzi Wa uke wako na ukishaharibu ulinzi huo unakua rahisi kupata fangasi na ndo kwanza utanuka uke kama ulikua hujui.

2) Acha matumizi ya madawa kiholela hasa dawa za UTI,kikohozi ,tumbo nk ,dawa hizo ni kama flagly,amoksilini,cipro nk.matumizi holela ya dawa hizi husababisha uharibifu Wa ulinzi Wa uke ambapo kunawaachia mwanya fangasi kushamiri.

3) usivae nguo za ndani ambazo ni mbichi au hazijakauka vizuri. Nguo za ndani zianikwe nje na zipasiwe vizuri.

4) acha kutumia sexy toys ya aina yeyote 
5) Punguza unene.punguza kilo zako angalau kwa asilimia 10. 
6) Acha ngono zembe

7) acha kushea nguo za ndani

MUHIMU
KAMA UNAPATA FANGASI ZA MARA MARA NAKUOMBA PIMA YAFUATAYO
1) KISUKARI
2) HIV 
3) MAFIGO NK
Ikumbukwe pia fangasi wakati Wa ujauzito inaweza kusababisha mimba kutoka au kujifungua kabla ya muda.
Asanteni ; shirikisheni kina Dada wengine

No comments:

Powered by Blogger.