Aina kumi za dawa ambazo hazipatani na pombe kabisa
Kumekua na kesi mbalimbali za vifo sababu ya watu kumeza dawa kisha kujisahau na kunywa pombe. Hii ni changamoto kubwa sana kwenye sekta ya afya kawaida dawa yeyote anayopewa binadamu kutibu kitu fulani ni sumu na ikichanganywa na baadhi ya kemikali kama pombe huweza kudhuru na kuua kabisa hivyo leo naenda kuzungumzia dawa kadhaa amabazo ukiona umezimeza usiguse pombe kabisa.
Dawa za kutibu bacteria[antibiotics];
hizi ni dawa ambazo hutumika mara kwa mara kwenye jamii kutibu magonjwa mbalimbali kama vidonda, kikohozi, kifua kikuu, madonda ya tumbo na kadhalika.matumizi ya dawa hizi na pombe huweza kuua. mfano fragile. isoniazid,grisiofulvin. lakini pia na baadhi ya dawa za malaria kama quinine na dawa za ya mseto ya malaria ni hatari zikitumika na pombe.
Dawa za kuzuia damu kuganda[ant cougulant];
Kuna dawa amabazo hupewa kwa wajawazito mara nyingi kulainisha damu ili isigande....sasa matumizi ya pombe hufanya dawa hizi kushindwa kufanya kazi na kusabisha damu kuganda hivyo kuziba mishipa ya damu ana kuleta kifo..mfano warfin
Dawa ya kupunguza mgandamizo wa mawazo[ant depressant];
Pombe huingilia kazi ya dawa izi na kufanya dawa hizo ziongezeke kwenye damu kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyopangwa. hii humfanya mgonjwa alegee sana mfano amitriptyline.
Dawa za kutibu kisukari[ant diabetic];
Dawa za kisukari hutengenezwa kwa ajili ya kushusha kiasi kikubwa cha sukari mwilini, sasa matumizi ya dawa hizi na pombe husababisha hali moja kitaalamu kama lactic acidosis... dalili ya hali hii ni maumivu ya misuli,tumbo kuuma na kusikia usingizi.hali hii isipodhibitiwa hospitali huua.mfano metformin vidonge.
Dawa za mafua na aleji;[ant histamine]
Hizi dawa hutolewa kutibu mafua, miwasho ya ngozi na kikohozi lakini dawa hizi pia husababisha usingizi na uchovu kila zikitumika.pombe huongeza uzingizi huu na uchovu mara duvu na kufanya mtu ashindwe kazi. mfano promethazine maarufu kama fenigani na chlropherinamine maleate maarufu kama piriton.
Dawa za magonjwa ya akili;
Dawa za akili kama chlopromazine hutolewa kwa wagonjwa wa akili kupunguza dalili a magonjwa haya kwa kuwapa usingizi...sasa matumizi ya pombe huongeza usingizi huu maradufu na kuwafanya washindwe kupumua hivyo huweza kuleta kifo.
Dawa za kutibu madonda ya tumbo;
Mara nyingi madonda hutibiwi na mchahnganyiko wa dawa tatu kitaalamu kama triple therapy, sasa moja ya mchanganyiko huo kama cimetidine, metronidazole,scenidazole au tinidazole hazitakiwi kuchanganywa na pombe kabisa sababu ya madhara ambayo zimeonyesha.
Dawa za moyo;
Hichi ni kikundi kikubwa cha dawa ambacho hutumika kutibu matatizo ya moyo. matumizi ya dawa hizi wakati mwingine huingilia mfumo wa kazi wa mwili na kusababisha kizunguzungu na kuanguka wakati wa kusimama mfano methyldopa, hydralazine na isosorbine mononitrate na dinitrate lakini pia matumizi ya pombe hupunguza uwezo wa dawa ya presha kitaalamu kama propanalol na kuzuia uwezo wake wa kufanya kazi.
Dawa za maumivu makali;
kuna dawa za maumivu kali sana ambazo hutolewa kwa wagonjwa wenye maumivu makali kama ya kansa, uzazi na maumivu ya ajali. pombe huongeza wingi wa dawa hizi kwenye mfumo wa damu na kusababisha overdose yaani dawa kua nyingi mwilini pale inapomezwa na pombe hata kama ulimeza dozo sahihi.mfano morphine,pethidine, codeine,meperidine...hali hii huleta kifo mara nyingi kwani wasanii wakubwa kama michael jackson na prince waliuawa na hali hizi.
Dawa za usingizi;
Dawa za usingizi kama valium hutumika kwa wagonjwa wenye kushindwa kupata usingizi na wakati mwingine kwenye chumba cha upasuaji. dawa hizi huleta usingizi mkali...matumizi ya dawa hizi na pombe huongeza usingizi huu, hupunguza mapigo ya moyo, hupunguza uwezo wa kupumua, kupoteza fahamu na kifo lakini pia dawa za kifafa kama phenytoin hupunguzwa uwezo wake na pombe na kushindwa kuzuia uwezo wake wa kuzuia degedege za kifafa.
Mwisho;
Kutaja dawa hizi haimaanishi kwamba dawa zote ambazo sijataja hapa zinafaa kunywa na pombe, hapana..kuna dawa bado zinafanyiwa utafiti kama zina madhara zikitumika na pombe lakini pia ni vizuri kujenga tabia ya kutokunywa pombe kabisa kama uko kwenye dozi ya ugonjwa wowote na hata kama una ugonjwa ambao unataka kumeza vidonge maisha yote kama kisukari, presha, ukimwi, kifafa na kadhalika basi ni vizuri ukaacha pombe kabisa.
No comments: