Header Ads

Mbinu za Kuifanya Nyumba Yako Salama kwa Mtoto


Bafuni: kamwe usimuache mwanao ndani bafuni au kwenye maji mwenyewe. Kumbuka inachukua dakika chache mtoto kuzama na kufariki ndani ya maji, kuliko vile unafikiria. Hakikisha vitasa vya chooni na bafuni vinafungwa vizuri ili kufanya ugumu mwanao kufungua. Kila mara hakikisha sakafu ya chooni na bafuni ni kavu.
Samani nzito: kama meza, kiti, kabati. Hakikisha samani hizi zimewekwa katika hali ya usalama ili kuepuka kuhatarisha usalama wa mtoto.
Kabati: kawaida kabati hatuweki vitu salama. Dawa za kusafishia choo na bauni au vyombo jikoni, sabuni za unga na maji na bidhaa nyingine amabazo ni hatari kwa afya ya mtoto. Hakikisha unaondoa bidhaa na vyombo hatari kwenye makabati amabyo mwanao anaweza kufikia au kumbuka kufunga makabati hayo na funguo.
Ngazi: ikiwa nyumba yako ina ngazi, hakikisha kuweka geti dogo litakalomzuia mtoto kuzifikia ngazi na kudondoka.

No comments:

Powered by Blogger.