Header Ads

KUPATA HEDHI MARA MBILI KATIKA MWEZI MMOJA (INTERMENSTRUAL BLEEDING,METRORHAGIA)



Hii ni ile hali ambayo mwanamke hupata hedhi au kutokwa na damu ukeni muda wowote katika mzunguko wake tofauti na tarehe au muda aliiouzoea.. na damu hii hutokea pasipokua ama kuhusiana na tendo la ndoa.. mfano kwa mwezi huu wa 6 mwanamke anaweza kupata hedhi tarehe 10/6 halafu akapata tena tarehe 25/6
Kuna wanawake wenye mzunguko ambao uko vizuri yaani haubadiliki badiliki na wanapata damu kidogo au matone kidogo tu katikati ya mzungukoCyclic midcycle intermenstrual bleeding) wake yaani wakati wa yai kutoka(ovulation);na kuna wengine hutokwa na damu nyepesi siku chache kabla ya kupata hedhi au baada ya kumaliza hedhi kwa siku kadhaa(Cyclic premenstrual or postmenstrual intermenstrual bleeding). hii ni hali ya kawaida ya kimwili tu kwani kunakua na mabadiliko kidogo ya vichocheo ama vichocheo vinabadilishana majukumu nyakati hizi.

VISABABISHI VYA KUPATA HEDHI MARA MBILI

Matumizi ya vidonge vya majira(Oral contraceptives)

Maambukizi ya shingo ya kizazi(Cervicitis)

Maambukizi ya ndani ya kizazi(Endometritis)

Saratani ya kizazi(Uterine cancer)

Saratani ya shingo ya kizazi(cervical cancer)

Saratani ya uke(vaginal cancer)

Saratani ya sura ya uke na mdomo wa uke(Vulva cancer)

Maambukizi ya Uke(Vaginitis)

Madonda ya magonjwa ya zinaa kwenye mfumo wa uzazi(Sexually transmitted ulcerations)

Uvimbe ndani ya kizazi,shingo ya kizazi,uke nk(Benign growths)

No comments:

Powered by Blogger.