Header Ads

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo



Ufafanuzi wa jumla wa tatizo la nguvu za kiume na tiba yake
Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka siku had I siku. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wengi wenye umri kuanzia miaka 35 na kuendelea ndio wanaosumbuliwa na tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili.

Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.

Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.

Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).

Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.

Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.

Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza wake.

Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.

Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.

Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume. Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.

Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.

Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke.

Sababu nyingine ambazo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na matatizo ya mhemko kama:

  • Wasiwasi
  • Hasira
  • Msongo wa mawazo (Stress)
  • Huzuni
  • Hofu na mashaka
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Ili uume usimame vizuri ni lazima:

Mfumo wako wa neva uwe na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.

Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa

Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.

Uume kshindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri. Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni:

  • Uzee
  • Kisukari
  • Kujichua/Punyeto
  • Uzinzi
  • Kukosa Elimu ya vyakula
  • Kutokujishughulisha na mazoezi
  • Shinikizo la juu la damu
  • Ugonjwa wa moyo
  • Uvutaji sigara/tumbaku
  • Utumiaji uliozidi wa kafeina.
  • Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
  • Madawa ya kulevya
  • Kupungua kwa homoni ya testerone
  • Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
  • Pombe
Nguvu za kiume na mzunguko wa damu: Kitu gani husababisha uume usimame?

Unaweza kujibu ni msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.

Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia. Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani.

Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.

Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja muhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele muhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.

Tiba yake.
Chakula bora ni tiba ya kwanza ya nguvu za kiume na mazoezi ya viungo pia kama tatizo litazidi unashauriwa kwenda hospitali kumuona dakari ili upatiwe matibabu ya kitaalamu.

Baadhi ya vyakula unavyoshauriwa kutumia ili kuondoa tatizo la nguvu za kiume.

1. Blueberry



Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubisho vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.

2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.

Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.

4. Karanga



Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

5. Vitunguu saumu


Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

6. Ndizi


Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).

Vyakula ni bora kuliko madawa makali

Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.

Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.

Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.

Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.

No comments:

Powered by Blogger.