Header Ads

Hatari ya Kukabwa Koo Mtoto (Choking)


Mojawapo ya hatari nyingine kwa watoto ni kukabwa koo la hewa. Sio tu kwamba bado hawajawa na uwezo kamili wa kumeza, ila pia wanatumia mdomo wao kuweka vitu mbali mbali mdomoni wakidadisi. Hii inamaanisha kuokota kitu chochote wanachokutana nacho na kujaribu kukila.
Utaweza kushangaa ni kiasi gani cha watoto wanapelekwa kwenye vituo vya afya na kukutwa na vitu mbali mbali kwenye choo. Vitu kama shilingi, mawe madogo, gololi na vitu vidogo vidog ambavyo usingependa mtoto wako ameze.
Ni vyema kufanya kazi ya kuweka vitu vidogo vidogo ambavyo mtoto wako anaweza akaviingiza mdomoni na kumeza mbali nae. Kwa kawaida wataalamu wanasema kama kitu kinaweza kikaingia na kuenea kwenye mdomo wa mtoto wako basi kitu hicho si salama kwa kuchezea.
Habari njema ni kwamba kama mtoto wako alikula kitu tofauti na akakitoa kwenye choo chake, unaweza ukawa na amani kwamba mtoto yupo salama (labda tu kitu kile kiwe na ncha kali, ambapo unashauriwa kumuona daktari mara moja). Vile vitu ambavyo vilishindwa kutoka kwa njia ya choo cha mtoto vinaleta wasiwasi. Na vile vitu ambavyo vinaweza kukuletea madhara ndani kama betri ndogo za saa. Betri hizi zenye Lithium zina umbo dogo ambalo ni rahisi kwa watoto kumeza, ijapokuwa zina rangi na umbo la kuvutia zinaweza zikaleta madhara makubwa sana ndani, hata kusababisha kifo. Hivyo ni vyema kuziweka betri hizi mbali na sehemu ambayo mtoto hawezi kufikia. Pia mpeleke mtoto hospitali haraka kama unahisi amemeza betri hii au yeyote inayofanana.

No comments:

Powered by Blogger.