Header Ads

*MUDA MUAFAKA WA MAMA MJAMZITO KUANZA KLINIKI*


Mwanamke anapopata ujauzito huwa na mawazo ni lini haswa anatakiwa aanze kuhudhuria kliniki ya afya ya uzazi haswa kliniki ya mama mjamzito, wengi wao hawafahamu haswa ni lini muda muafaka wa kuanza kuhudhuria kliniki na wengi wao huchelewa kuanza na kupata huduma ya kliniki kwa mama mjamzito.
Muda muafaka wa kuanza kliniki ya afya ya uzazi kwa mama mjamzito ni pale tu anapogundua kuwa ni mjamzito, lakini ni vyema hata kabla mwanamke hajashika ujauzito na amepanga yeye na mwenzi wake wanapaswa waanze kliniki mapema, ili waweze kupata huduma kabla ya ujauzito na inakuwa vyepesi kuendelea na huduma wakati wa ujauzito.
Kliniki ya afya ya uzazi si kliniki ya akina mama tu, hata akina baba huwahusu na inashauriwa mama mjamzito anapoanza kliniki anatakiwa aende na mume/mwenzi wake, mara tu mwanamke anapogundua kuwa ni mjamzito. Kuanza kliniki mapema mara tu mwanamke anapojigundua ni mjamzito kuna faida ukilinganisha na mama mjamzito anaechelewa kuanza kliniki mapema.
Kuwahi kuanza kliniki mapema kunasaidia kupata huduma stahiki mapema na kuchelewa kuanza kliniki mapema huweza sababisha kukosa baadhi ya huduma katika kipindi cha ujauzito.
*ASANTENI*

No comments:

Powered by Blogger.