Header Ads

KUTOKWA NA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDH

Matokeo ya picha ya hedhi

Hili ni taitizo ambalo huwakumba wanawake wengi katika nyakati tofautitofauti.
Mwanamke hutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi pia inaweza kudumu kwa wiki moja na zaidi.
Hali hii isipopatiwa ufumbuzi huweza kuleta madhara makubwa sana kwa mwanamke ambayo hupelekea vifo.
Katika hali fulani sababu ya kutokwa na damu nyingi inaweza isijulikane.
.
.
Zipo sababu kuu zinazosababisha hali hii.Sababu hizo huweza kutofautiana kati ya Mtu mmoja mpaka mwingine kutokana na kiwango cha lishe na virutubisho alivyonavyo mama huyo.
Zifuatazo ni sababu kuu ambazo huchangia tatizo hilo.
1.Kutokuwepo kwa usawa wa vichocheo (Hormonal imbalance )
Vichocheo vya oestrogen na progesterone hutakiwa kuwa katika usawa ili viweze kufanya kazi yake ipasavyo.
Matumizi ya vichocheo katika kupanga uzazi(vijiti/contraceptive pills) huweza kubadili Hali ya vichocheo na kusababisha hali hiyo kutokea,
Kama hali hii itatokea ukuta wa mfuko wa mimba hutoa damu nyingi isiyokawaida.
2. Matatizo ya ovari .
Ovari ni sehemu muhimu sana katika katika kuandaa na kukuza yai na badae kutolewa likiwa kamili kuingia katika mirija ya fallopia tayari kwa safari kuelekea mfuko wa kizazi.
Kama ovari zitashindwa kutoa mayai basi tatizo huwa ni upingufu wa kichocheo kiitwacho progesterone hivyo yai haliwezi kutoka kwenye ovari na hali hii husababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.
3. Uvimbe kwenye shemu ya kizazi (Fibroids )
Fibroids siyo saratani bali huwa ni uvimbe wa kawaida ambao hubaki sehemu moja (benign), ambayo hutokea katika umri wa uzazi.
Na hii husababishwa na vichocheo kutokuwa katika usawa na huweza kusababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.
4. Vimbe ndogondogo kwenye kizazi .
Huwa ni vimbe ndogo sana katika mfuko wa uzazi.
Hutokea kwa wanawake katika umri wa kuzaa kutokana na vichocheo kuongezeka.
5. Magonjwa ya kurithi.
Matatizo ya damu kutoganda kutokana na hii husababishwa na ukosefu wa vigandishi vya damu.
6. Matatizo ya kiafya.
Maambukizi katika njia ya kizazi kama Pelvic Inflammatory Diseases(PIDs)
Je nani yuko hatarini kukumbwa na hali hii ?
Makundi yafuatayo yako katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili..
1. Wale waliovunja ungo hasa mwaka mmoja wa kwanza huwa hatarini kupata changamoto hii
2.Wanawake wanaokaribia ukomo wa hedhi kati ya miaka 40-50 wako hatarini katika mabadiliko ya vichocheo.
ZIJUE DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO HILI (Menorrhagia )
1.Kutumia pads moja ama zaidi kila saa kwa mfululizo wa masaa kadhaa.
2. Uhitaji wa kuamka usiku kubadili pad.
3.Damu kutoka nyingi zaidi ya siku nne wakati wa hedhi.
4.Kutoa mabonge ya damu wakati wa hedhi zaidi ya siku moja.
5.Kutoshiriki shughuli za kila siku kutokana na damu nyingi kutoka
6.Dalili za kuishiwa damu, kama kuchoka, ama kupumua kwa shida.
.
.
MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA ENDAPO HATUA MADHUBUTI HAZITACHUKULIWA .
1.Upungufu wa iron ambayo ni madini muhimu katika damu ambapo husaidia katika kubeba hewa ya oksijeni, kukosekana ama kupungua kwake maisha huwa hatarini.
2. Maumivu makali wakati wa hedhi ambayo wakati mwingine huhitaji kutumia dawa za kutuliza maumivu.
Mwili wa mwanamke huhitaji uangalizi wa hali ya juu.
Uonapo dalili ama viashiria hivyo basi tambua changamoto hii ipo karibu nawe hivyo ni vyema kuitafutia ufumbuzi mapema sana.
Suluhisho.
Tumia virutubisho sahihi vyenye kuweza kukupa madini muhimu katika mwili wako.
. Fanya mazoezi mara kwa mara kwani husaidia katika kuimarisha utendaji kazi mzuri wa mwili wako.
Lakini pia tumia tiba lishe ili kuweza kuimarisha homoni ambazo zitakusaidia kuondokana na changamoto ya homorne imbalance.
Ukizingatia na kutumia Lishe bora na virutubisho bora basi utaweza kuimarisha Afya yako na kuondokana na changamoto hiyo.
Kwa Maelezo zaidi/Maswali au ushauri
Wasiliana nasi
Namba:0765203999

No comments:

Powered by Blogger.