Header Ads

AINA YA MATUNDA YANAYOSAIDIA KUPUNGUZA SHINIKIZO LA DAMU MWILINI


Tatizo la Shinikizo kubwa la damu ni kubwa hapa Tanzania na Dunia kwa ujumla. Idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka kila siku, juhudi zinapaswa kufanyika ili kuzuia na keupukana na Tatizo hili. Sababu kuu zinazochangia kuwepo kwa Tatizo hili ni pamoja na Mtindo mbaya wa maisha: ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na chumvi tele, kutofanya mazoezi, msongo wa mawazo (stress) pia huchangia kwa sehemu kubwa. Hivyo basi namna nzuri ya keupukana na Tatizo hili ni kubadili Mtindo wa maisha yaani kufanya mazoezi na kula chakula bora. Leo nimekuletea baadhi ya matunda yanayosaidia kupunguza Shinikizo kubwa la damu ili uboreshe mlo wako na kudumisha afya yako.
Tikiti maji (Water melon)
Matunda haya yana kemikali muhimu sana inayoitwa Lycopene inayosaidia kuufanya moyo uwe na Afya njema unaoweza kusukuma damu kwenda kwenye sehemu zote za mwili kwa uzuri zaidi,hivyo mzunguko Wa damu huwa ni mzuri na uwezekano Wa shinikizo la damu huwa ni mdogo. Pia yana virutubisho vingine kama vile; Beta carotene,vitamin C, na antioxidants. Yana madini ya Potassium kwa wingi hivyo hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu.
Ndizi mbivu (Banana)
Matunda haya ni muhimu sana kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu kwa sababu yana kiwango kidogo sana cha madini ya sodium (huongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu) ,pia yana kiwango kikubwa cha madini ya potassium; kwa kila gramu 100 za ndizi kuna miligramu 358 za madini ya potassium. Kupitia jarida kubwa la kisayansi (International Journal of Pharmacognosy) wanasayansi wamethibitisha kuwa ndizi hupunguza shinikizo kubwa la damu.
Embe (Mango)
Katika kila gramu 100 za embe kuma miligramu 168 za madini ya Potassium ambayo hupunguza shinikizo la damu kama ilivyoelezwa hapo mwanzo.Unaweza kula kama yalivyo au ukatengeneza juisi yake na kuitumia.Unapaswa kula maembe kwa kiasi .
Matunda aina ya Strawberries
Matunda haya yanapatikana hapa Tanzania na yana umuhimu mkubwa sana katika kupunguza uwezekano wa shinikizo kubwa la damu. Yana sifa ya kuwa antioxidants na anti-inflammatory,pia ya vitamin C kwa wingi na kemikali muhimu iitwayo omega 3 fatty acids. Pia juisi yake huwa na madini ya Kalsium yanayopunguza shinikizo kubwa la damu.

No comments:

Powered by Blogger.