Header Ads

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL CANCER)

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko  katika shingo ya kizazi. Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani   inayoongoza kwa kusababisha vifo vya  wanawake katika nchi zinazoendelea. Repoti ya 2012 ya shirika la afya duniani 'WHO' imesema kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya kizazi barani Afrika, 50,000 walifariki dunia.Namba za matukio haya zinawakilisha waathirika  waliopata fursa ya utafiti jaboNINI KINACHOSABISHA SARATANI YA  SHINGO YA UZAZI ?Ripoti za utafiti wa  kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99%  ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus'  au HPV vilivyoko katika jamii  ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja  huambukizwa kwa njia ya  kujamiana.


BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA  HATARI  ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?
Kushiriki tendo ndoa katika  umri mdogo au chini ya miaka 18Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofautiUtumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system)Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama UkimwiUzazi wa mara kwa mara
BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni.Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoaMaumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area)Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudiaMkojo wenye matone ya damu
JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA ?Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema.PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST);Pap-Smear ni test ambayo hutumika  kuchunguza  mabadiliko ya chembe zilizoko katika mlango wa kizazi   ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo  na hivyo kuwahi kuyakabili  mapema.
UMRI WA KUPATA PAP TESTTest hii hushauriwa kwa wanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65  na chini ya umri wa miaka 21 endapo umeingia katika tendo la ndoa kwa kipindi cha kisichopungua miaka 3.KUPUNGUZA HATARI ZASARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?
Pap tests.  Waweza kupata Pap test mara 1 kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2- 3,hii itategemea ushauri wa daktari,umri,hali yako ya afya kwa ujumla,  na majibu uliyoyapata katika testi zilizotangulia na mfumo wako wa maisha.Pata  HPV vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa daktari)Kuwa na mpenzi mmoja. Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa.Tumia kinga (condoms). Hii husaidia  kupunguza maambukizi ya magojwa ya  zinaa.

No comments:

Powered by Blogger.