Header Ads

HUDUMA YA KWANZA KWA ANAETAPIKA NA NINI KIFANYIKE KUZUIA KUTAPIKA PINDI UNAPOHISI KICHEFUCHEFU.


Habarini za muda huu, kama nilivyo waahidi kuwa kutakuwa na somo linalohusu kutapika, nini kifanyike pindi mtu anapotapika na nini kifanyike kuzuia kutapika.
KARIBUNI>>>>>
MAANA YA KUTAPIKA.
Kutapika ni kutoka kwa vitu vilivyopo tumboni aidha kwa kupenda au kutokupenda kupitia mdomo.
Kutapika sio ugonjwa bali ni dalili ya hali mbalimbali za kimwili.
VITU VINAVYOSABABIBISHA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA NI HIVI.
1.) Hatua za awali za ujauzito.
2.) Dawa za kutapika, kusafisha tumbo
3.) Msongo wa mawazo au uoga wa jambo fulani.
4.) Magonjwa ya mfuko wa nyongo,
5.) Sumu katika vyakula.
6.) Kula chakula kingi kupita kiasi (kuvimbiwa),
7.) Magonjwa ya moyo,
8.) Kujeruiwa kwa ubongo,
9.) Vidonda vya tumbo
10) Baadhi ya cancer
11.) Kunywa pombe kupita kiasi.
12.) Aleji ya maziwa kwa watoto wadogo.
KWA KUANGALIA MUDA ULIOPATIA KICHEFUCHEFU, UNAWEZA KUGUNDUA SABABU YA KUTAPIKA.
Mfano, kama kichefuchefu kitaonekana muda mfupi baada ya kula, basi apo yawezekana imesababishwa na sumu katika chakula, vidonda vya tumbo au kula kupita kiasi.
Kuna baadhi ya bakteria wanakaaga kwenye chakula lakini wanachelewaga kuonyesha dalili ya kichefuchefu mapema.
JE KUTAPIKA KUNA MADHARA YOYOTE???
Kutapika mara nyingi sio ugonjwa na wala hakuna madhara, ila inaweza ikawa ni dalili ya hali (ugonjwa) mbaya zaidi kwa mfano majeraha katika ubongo au kuvimba kwa ubongo.
NI WAKATI GANI NA HALI GANI YA KUTAPIKA ITANIFANYA NIMUONE DAKTARI???
Unapaswa kwenda kumuona daktari kama kuna yafuatayo:-
1.) Kama kichefuchefu kimedumu kwa muda wa siku kadhaa bila kuacha, kamwone daktari.
2.) Kama umefanya huduma ya kwanza na haijasaidia, au umekaukiwa maji mwilini, au umegundua kuwa una majeraha kwenye ubongo ambayo ndo yamesababisha kutapika.
3.) Kwa watu wazima, muone daktari kama unatapika kwa zaidi ya siku moja mfululizo, au kama kuna dalili ya kupungukiwa maji.
4.) Kwa mtoto mchanga au mwenye umri wa chini ya miaka 6, mpeleke kwa daktari kama anatapika kwa zaidi ya masaa kadhaa na kuna dalili ya kupungukiwa maji mwilini.
Kwa mtoto zaidi ya miaka 6, muone daktari kama atatapika kwa zaidi ya siku moja.
UNATAKIWA UMUONE DAKTARI HARAKA SANA KAMA HALI ZIFUTAZO ZITAAMBATANA NA KUTAPIKA.
1.) Damu katika matapishi.
2.) Maumivu makali ya kichwa na shingo.
3.) Maumivu makali ya tumbo.
4.) Kuharisha
5.) kupumua haraka haraka isivyo kawaida.
KIVIPI UNAWEZA KUTIBU KUTAPIKA??
1.) Kunywa maji masafi kwa wingi
2.) Usile vyakula vigumu mpaka pale utakapoacha kutapika
3.) Kama unatapika na kuharisha kwa zaidi ya siku moja (masaa 24), itabidi unywe oral dehydrating solutions (maoro) utapata kwa wataalamu hospitali au duka la dawa.
UNAWEZAJE KUZUIA KICHEFUCHEFU??
1.) Kula chakula kwa kiasi cha kawaida na sio chakula kingi kupita kiasi.
2.) Kula taratibu.
3.) Usile vyakula vigumu sana
4.) Kula vyakula vya uvuguvugu kama unapata kichefuchefu kutokana na harufu ya vyakula vya moto sana.
5.) Pumzika baada ya kula, kichwa kikiwa juu, na sio kulala.
6.) Kunywa maji baada ya kula na sio wakati wa kula.
UNAWEZAJE KUJIZUIA KUTAPIKA KIPINDI UNAHISI KICHEFUCHEFU?
Kama unaanza kuhisi kichefuchefu, unaweza ukujizuia kutapika kwa kufanya yafuatayo..
1.) Kunywa kiasi kidogo cha kinywaji kitamu kama soda au juice ya matunda isipokuwa matunda yenye asidi kama machungwa.
2.) Pumzika kwa kukaa, kuhangaika kutaongeza kichefu chefu na unaweza kutapika.
AHSANTENI, NA KARIBUNI KWA MASWALI NA MAONI PALE AMBAPO HUJAELEWA NA TUPO TAYARI KUKUJIBU AU KUKUSAIDIA.
USISAHAU KUSHARE ILI JAMII YOTE IPATE ELIMU HII.

No comments:

Powered by Blogger.