Header Ads

UKOMO WA HEDHI KWA MWANAMKE NA CHANGAMOTO ZAKE.

Matokeo ya picha ya ukomo wa hedhi"
Ukomo wa hedhi kwa mwanamke ni kipindi ambacho vichocheo vya uzazi hupungua kiasi kwamba hushindwa kufanya mwendelezo wa hedhi kwa mwanamke.
Mara nyingi uanzaji wa kipindi hiki hutofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine kutokana na sababu mbalimbali wapo ambao huanza mapema zaidi na wapo ambao huchelewa.
Wengine pia huanza kwa kukoma koma na wengine huanza kwa kukoma ghafla.
Kabla ya kipindi hiki mwanamke hupitia katika hali ambazo huonekana kuwa na matatizo kiafya.
Kabla ya kufikia ukomo wa hedhi mwanamke huanza kwa kuonyesha viashiria vifuatavyo.
1.Hedhi isiyo na muda maalumu, yaani haieleweki.
2.Uke kuwa mkavu
3. Kutoka na jasho wakati wa usiku na kuhisi joto sana.
Hali hiyo humfanya mtu kuishiwa nguvu
4. Matatizo ya usingizi
5.Kuongezeka uzito,hii ni kutokana na mwili kuanza kuzalisha mafuta mengi hivyo hupelekea kuongezeka kwa uzito sana.
6. Ngozi kuwa mkavu
7. Hali ya kuisi kama vichomi.
Viashiria hivyo huonesha dhahiri kuwa mtu huyu anaenda kupata hiyo hali na kutakiwa kuwa makini.
Mabadiliko hayo mara nyingi hupelekea mwanamke kuwa na hasira mara kwa mara
8. Kupoteza umakini katika utendaji wao wa kazi pia husahau sahau mara kwa mara.
9. Kushuka kwa utendaji kazi wa moyo ,hivyo mtu mwenye changamoto hii huwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo ya mda mrefu.
10: Maunivu ya mgongo,kiuno n.k
SABABU ZAKE:
Hali hii husababishwa na mambo mengi.
1. Kushuka kwa vichocheo vya uzazi.
Kati ya miaka 30 na 40 wanawake wengi huwa katika hali ya kupata viashiria hivyo.
Hapa mwanamke hutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, au wakati mwingine yaweza kuwa kidogo.
2.Tiba ya cancer kwa dawa na mionzi
Baadhi ya dawa hizo huwa na vichocheo ambavyo huvuruga mfumo mzima.
3.Ovari kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
MADHARA AMBAYO YAWEZA KUTOKEA
1. Magonjwa ya moyo, kutokana na kupungua kwa oestrogen
2. Mifupa kuwa laini
3 Kushindwa kuzuia mkojo
4.Kukosa hamu ya tendo
SULUHISHO LAKE:
Katika kuondoa matatizo hayo muunganiko wa chakula ndiyo umeonekana kuondoa matatizo hayo kwa kiwango cha juu,
Wapo wanawake wengi ambao wamefanikiwa kupita katika hatua hiyo pasipo kupata changamoto yoyote au matatizo yoyote kama hayo yalotajwa hapo kwa kutumia lishe bora yenye kuupa mwili virutubisho sahihi.
Kupitia lishe hizo na virutubisho hivyo mwili huwezi kupunguza kiwango kikubwa cha uzalishaji mafuta na hivyo kuondoa Changamoto ya mafuta kuganda katika mishipa hivyo moyo hufanya kazu yake vyema.
Lakini pia mwili upatapo virutubisho bora huupa uwezo mwili kubalance homoni hivyo vichocheo vya mwili huwa sawa na hii husaidia kuupa mwili afya bora na kuondokana na tatizo la maumivu ya kiuno,mgongo nk.
Pia kufanya mazoezi,mwili upatapo mazoezi vizuri husaidia kujenga afya bora na kuupa ubongo kufanya kazi vyema hivyo huimarisha kumbukumbu vyema.
Pengine na wewe unapata hayo matatizo
Au upo katika changamoto hiyo na unahitaji kuondokana nayo au huhitaji kuipitia changamoto hiyo.
Wasiliana nasi kwa maswali na pia maoni
Au namna ya kuondokana na changamoto hizo. 0765203999

No comments:

Powered by Blogger.