Header Ads

TATIZO LA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA NA SULUHISHO LAKE

Matokeo ya picha ya kukosa hamu ya tendo la ndoa
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi au kukosa nyege kwa lugha ya mitaani huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume lakini ni wanaume wanaokerwa zaidi na tatizo hili kulio wanawake. Wakati ambapo ni asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wenye tatizo hili, idadi ya wanawake ni mara mbili ya hii ya wanaume. Lakini wakati ni asilimia 23 ya wanaume wanaonyesha kuridhika kuishi na tatizo hili, asilimia 46 ya wanawake wapo radhi kabisa kuendelea kuishi na tatizo hili.
Si lazima kuendelea kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa sababu kuna mambo unayoweza kuyafanya ili kuondokana na hili tatizo.
Hali ya kupenda kufanya mapenzi au tendo la ndoa kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalibali yanayomtokea katika maisha yake.
Baadhi ya matukio yanayoathiri hamu ya mwanamke kufanya mapenzi ni pamoja na:
Kuanza na kwisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanamme,
Kupata ujauzito, na magonjwa.
Kama wewe mwanamke umepatwa na hali hii unaweza kukabiliana nayo kwa kubalisha jinsi unavyoishi, kufanya mambo kadhaa yatakayo badilisha hali hii au kutumia baadhi ya virutubishi ambavyo husaidia kuondoa tatizo hili.
Sababu Za Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa
Sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni nyingi lakini kwa ujumla karibu zote tunaweza kuzigawanya katika makundi manne:
1. Mahusiano Baina Ya Mwanamke Na Mwanamme Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga mapenzi kati yake na mwanamme. Hivyo, mahusiano mabovu yaweza kuwa ndicho chanzo cha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke. Mwanamke atakosa hamu ya kufanya mapenzi endapo hakutokuwa na mawasiliano baina yake na mumewe, kutakuwa na migogoro kati yake na mumewe isiyokwisha, kutakuwa na ukosefu wa mawasiliano kuhusu mahitaji yake ya kufanya mapenzi na jinsi ambavyo yeye angependa kufanyiwa kimapenzi na kama atahisi kuna ukosefu wa uaminifu katika ndoa au mahusiano yao.
2. Matatizo Katika Maisha Yako Matatizo mbalimbali katika maisha ya mwanamke humsababishia kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni pamoja na magonjwa, mabadiliko katika mwili wake na hata matumizi ya baadhi ya madawa:
Matatizo Katika Kufanya Tendo La ndoa . Kama mwanamke anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au kama mwanamke anakosa kufika kileleni, hali hii inaweza kusababisha akakosa kabisa hamu ya kufanya mapenzi.
Matatizo ya afya , Magonjwa mengi husababisha mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya magonjwa ni maumivu ya viungo vya mifupa (arthritis) , kansa, ugonjwa wa kisukari , high blood pressure, matatizo katika mishipa ya damu ya arteri na matatizo ya akili.
Matumizi ya madawa . Baadhi ya madawa yakitumiwa, huondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano wa dawa hizo ni madawa ya kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mtindo wa maisha . Matumizi ya pombe kuzidi kiwango, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya huathiri hamu ya kufanya mapenzi.
Upasuaji. Upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au katika maeneno ya viungo vya uzazi humbadilishia mwanamke mwonekano wake, huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na mwisho kuathiri hamu yake ya kufanya mapenzi.
Uchovu. Uchovu unaotokana na kulea watoto wadogo au vikongwe huweza kuathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi.
3. Mabadiliko Katika Mfumo Wa Homoni.
Kukoma Hedhi. Mabadilko ya viwango vya homoni katika mwili wa mwanamke yanaweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Kupungua kwa Estrogen katika mwili wa mwanamke katika kipindi cha kuelekea kukoma hedhi kunaweza kusababisha ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi. Upungufu wa homoni hiyo husababisha uyabisi wa wa viungo vya sehemu nyeti na kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Mwanamke pia huweza kuwa na upungufu wa homoni ya testosterone, homoni ambayo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake, hivyo mwanamke huyo akapungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Pamoja na kuwa wanawake wengi huendelea kupata hamu ya kufanya mapenzi baada ya kukoma hedhi, baadhi kupungukiwa na hamu hiyo baada ya mabadiliko haya ya viwango vya homoni katika miili yao.
Ujauzito na kunyonyesha. Mabadiliko katika mfumo wa homoni wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua na wakati wa kunyonyesha huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
4. Matatizo Ya Kisaikolojia
Matatizo ya kisaikolojia yana mchango katika kumfanya mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya mtatatizo hayo ni:
Waswasi na kuwa na msongo wa mawazo
Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
Kuwa na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa au kubakwa
Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi.
*SULUHISHO*
Hakuna dawa ya moja kwa moja toka hospitalini kwa sasa hivi kwa ajili ya kuondoa tatizo hili, hata hivyo wanawake wengi wanaweza kurudi kwenye hali zao za kawaida kwa kushirikiana na waume zao waelewa. ukisaidiana na mumeo. Unahitaji kuchunguza taratibu na kwa kina chanzo cha tatizo lako, na taratibu lifanyie kazi kwa msaada wa mume wako.
Katika nchi zilizoendelea, kila siku wamekuwa wakija na dawa na vifaa vipya vya kuondoa tatizo hili na vingi bado ni vya bei kubwa na/au vinapatikana kwa shida.
Vipo ambavyo vimeonyesha mafanikio makubwa, mifano ya vitu hivyo ni virutubisho asili
wasomaji wangu wengi wamefanikiwa na kunishukuru kwa kutumia virutubisho hivi (Tiba lishe) ambacho kinachosaidia kuongeza hamu. Kama bado bado unachangamoto hiyo nashauri utumie
virutubishi hivyo na
Endapo umepata tatizo kutambua virutubishi vizuri vya kutumia, wasiliana nasi kwa kutumia njia yo yote iliyo rahisi kwako kati ya hizi nilizoziorodhesha hapo chini.
Chakula Cha Kuongeza Hamu Ya Mapenzi
Utafiti umeonyesha pasi shaka kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya chakula tunachokula na afya ya viungo vya uzazi. Baadhi ya chakula na virutubishi vimehusishwa na hamu ya kufanya mapenzi (nyege). Virutubishi ndani ya chakula ambavyo vinasaidia hali hiyo ni antioxidants, vitamin C, vitamin E, potassium na zinc. Kirutubishi cha zinc ambacho hupatikana ndani ya vitunguu swaumu, mbegu za maboga, ufuta na mbegu za matikitimaji, kinaongeza mbegu kwa mwanamme (sperm count) hivyo humsaidia kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Chakula cho chote chenye virutubishi hivi kikiliwa, humfanya mlaji asikie hamu ya kufanya mapenzi au kwa maneno ya mtaani, chakula hiki kinasaidia kuongeza nyege. Baadhi ya chakula cha kuongeza hamu ni
Tikitimaji-Hili linachukuliwa kuwa ndilo tunda bora katika kuboresha afya ya mapenzi. Tunda hili lina asilimia 92 ya maji na asilimia 8 zinazobakia zina phytonutrient citrulline ambayo hugeuzwa kuwa arginine. Arginine ni amino acid ambayo hufanya mishipa ya damu kuwa kwenye hali ya ubora wake na kusadia damu kupita vizuri zaidi. Tikitimaji kwa hiyo husaidia damu ifike kwa kiwango kizuri zaidi kwenye sehemu ambazo hutakiwa kutanuka wakati mtu akipata hisia za kufanya tendo la ndoa ambazo ni viungo vya ndani ya kisimi cha mwanamke na ndani ya uume wa mwanamme.
Strawberries, matunda haya yana antioxidants kwa kusaidia afya ya moyo na mishipa ya damu (arteri) na vitamin C ambayo huongeza kiwango cha mbegu kwa mwanamme na mwanamke.
Avocadro-tunda hili lina vitamini E ambayo ni antioxidant. Ndani ya tunda hili kuna potassium na vitamini B6 ambavyo huboresha afya ya moyo na kusaidia mzunguko wa damu.
Viazi vitamu-hivi vina potassium ambayo husaidia kuondoa tatizo la high-blood pressure.
Hivyo kirutubisho hiki kimejumuisha vyakula hivyo vyote na hivyo mtumiaji wa bidhaa hii huweza kupata madini yote muhimu ambayo husaidia kuboresha afya ya tendo la ndoa na kurudisha hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa Mwanamke.
Unaweza kuvipata sehemu yoyote Tanzania.
Wasiliana nasi kwa  0765203999

No comments:

Powered by Blogger.