KWA NINI MBU HAWEZI KUENEZA VIRUSI VYA UKIMWI??? SABABU NI HIZI HAPA!!
Mbu ni kiumbe ambacho kinaongoza kwa kusababisha vifo vingi duniani kupitia magonjwa ambayo huyaeneza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine mfano malaria, homa ya dengue na mengine mengi.
Lakini kwa bahati nzuri na jambo la kumshukuru mungu ni kwamba mbu hawezi kueneza virusi vya UKIMWI kutoka kwa mtu aliyeathirika kwenda kwa mtu asiyeathirika na UKIMWI.
KWA NINI MBU HAWEZI KUENEZA UKIMWI?
1.) Kwanza, mbu anatumia mirija miwili tofuti pindi anapomng'ata mtu, mrija mmoja anatumia kuingizia mate yake kwa mtu, na mwingine anatumia kunyonya damu kutoka kwa mtu aliyemng'ata.
Kwa maana hiyo, kinachoingia kwa mtu kutoka kwa mbu kwenda kwa mtu ni mate ya mbu tu na sio damu, na kinachotoka kwa binadamu kwenda kwa mbu ni damu tu.
Kazi ya mate ya mbu ni kuzuia damu isigande kipindi anainyonya kutoka kwa mtu.
Kama mbu akimng'ata mtu mwenye virusi vya UKIMWI, virusi hivyo vitaingia tumbo la mbu.
Ili mbu aweze kusababisha UKIMWI, virusi hivyo vinatakiwa viishi kwenye tumbo la mbu, halafu baadaye virudi mdomoni, viingie kwenye tezi zinazotengeneza mate, na baadaye viambatane na mate kuingia kwa mtu pindi mbu huyo atakapokuja kumng'ata mtu asiyeathirika na keneza virusi hivyo na kusababisha UKIMWI.
KWANINI SASA MBU HAWEZI KUENEZA UKIMWI WAKATI HATUA ZA UENEZWAJI ZIPO HAPO JUU.???
Kwa bahati nzuri, hizo hatua za uenezwaji wa virusi vya UKIMWI haziwezi kutokea.
KWANINI?
Vizuri, ili virusi viweze kuishi kwenye tumbo la mbu, vinahitaji vitu (seli) maalumu ambazo zinapatikana kwa binadamu tu, kwa maana hiyo mbu hana hizo seli na ndio maana virusi vya UKIMWI haviwezi kuishi kwenye tumbo la mbu, hivyo vitakufa na kuacha mate ya mbu yakiwa salama na hayana virusi,, hata mbu akimng'ata mtu mwingine, atampa mate ambayo hayana virusi vya UKIMWI.
2.) MBU ANA UWEZO MDOGO WA KUBEBA VIRUSI VYA UKIMWI.
Kama mbu angekuwa na uwezo wa kueneza ukimwi, ili mtu apate UKIMWI, anatakiwa ang'atwe na mbu milioni 10 wenye virusi vya UKIMWI, kwa mara moja, ambalo ni jambo gumu kutokea,.
ASANTENI,,
USISAHAU KUSHARE ILI WATU WANUFAIKE ZAIDI NA ELIMU HII..
No comments: