Header Ads

MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA

Matokeo ya picha ya tatizo la maumivu wakati wa kukojoa
Kupata maumivu wakati wa kukojoa ni tatizo ambalo husababishwa na magonjwa tofauti tofauti na huwapata watu wengi sana. Pia tatizo hii katika lugha za kitaalamu hujulikana kama dysuria. Shida kubwa ya kupata maumivu haya wakati wa kukojoa ni kutokana na mtu kupata maambukizi katika njia au mfumo wa mkojo ambayo hali hii hujulikana kitaalamu kama UTI yani Urinary Tract Infection ambayo huwapata watu wa rika zote lakini wanawake ndo huwa kwenye kiwango kikubwa sana. Ukiachana na maambukizi katika mfumo wa mkojo pia magonjwa ya zinaa kama kaswende, kisonono na mengineyo huweza kusababisha hali hii.
Dalili zake
  1. Homa
  2. Maumivu kwenye mbavu (hii huonesha kua maambukizi ni makali sana)
  3. Maumivu chini ya kitovu
  4. Mara nyingine kutokwa na mkojo wenye damu
Maumivu haya hutokana na njia ya mkojo kushambuliwa na wadudu kama bakteria ambao huaribu ukuta wa njia ya mkojo na kusababisha kama kijidonda hivi ambapo pindi unapokojoa mtu huhisi maumivu ni kwa sababu hii ya kuchubuka.
Vyanzo vya maumivu
  1. Magonjwa ya zinaa
Magonjwa haya yapo ya aina tofaouti tofauti kama kisonono, kaswende, klamidia ambayo nayo hufanya mtu kuhisi maumivu pindi anapokojoa na huathiri sana wanaume na dalili zake mara nyingi hufanana na zile za uchafu katika mfumo wa mkojo (UTI) na pia usaha hua unatoka sehemu za siri. Kujikinga na ugonjwa huu ni kutumia kinga (kondomu),kua na mwamifu na mpenzi mmoja
  1. Maambukizi katika njia ya mkojo ambayo hujulikana kama UTI
Katika maambukizi ya njia hii mgonjwa hupata dalili kama homa, maumivu chini ya kitovu, maumivu kwenye mwenye mbavu na chini kidogo ya mbavu hasa ukiwa unapitisha mkono (palpitation) na pindi unakojoa unahisi kama unaungua.
Njia za kupunguza makali ya ugonjwa huu ni kunywa maji mengi sana, pia kukojoa kabla ya kulala na baada ya tendo la ndoa hii husaidia sana kupunguza kujirudia rudia kwa ugonjwa huu.
  1. Kichocho
Kichocho ni hatari sana na ugonjwa huu pia husababisha maumivu wakati wa kukojoa na dalili zake pia huingiliana na magonjwa tajwa apo juu ila Zaidi mtu kukojoa mkojo wenye damu kabisa, hii ni kutokana na wadudu hawa kushambulia sana njia ya mkojo.mara nyingi wavuvi au watu wanaofanya kazi kwenye maji machafu ndo huwapata sana.


  1. Maambukizi ya ukeni
Hii ni kwa wanawake wenye maambukizi katika njia hii (uke) ambapo kitaalamu hujulikana kama vaginitis nao pia hupata dalili zinazofanana na hizi baadhi na pia hupata maumivu pindi wanapiokojoa.
Na magonjwa mengine mengi tuuu kama mawe kwenye figo n.k
Unashauriwa ukiona una dalili hizo zilizotajwa hapo au unapata maumivu wakati wa kukojoa ni kuchukua maamuzi na kufika katika kituo cha afya kilichopo karibu na wewe. Pia  kufanya vipimo ili kuweza kupata suluhisho na tatizo lako na sio kufanya maamuzi ya kujitibu mwenyewe.
Magonjwa mengi yanatibika kabisa cha msingi ni kuwahi tuu katika kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi ili kupewa tiba sahihi.
0765203999

No comments:

Powered by Blogger.