Header Ads

Dawa ya meno



Dawa ya meno

Jump to navigationJump to search
Dawa ya meno ikikamuliwa kutoka tyubu yake na kuwekwa juu ya mswaki wa kisasa ili kusambazwa katika meno yote.
Dawa ya kusugulia meno ni kemikali inayotumika pamoja na mswaki wa kisasa kusafishia meno yazidi kupendeza na kuwa na afya.
Inasaidia kuondoa harufu mbayautambo wa meno na mabaki ya chakula katikati yake, pamoja na kuacha aina ya kinga (hasa ya floridi, kwa Kiingereza "Flouride") dhidi ya maradhi ya meno na ya ufizi (nyama inayoambatana nayo) (kwa Kiingereza "gingivitis").[1]
Hata hivyo kwa kiasi kikubwa ufanisi wa usafi unategemea zaidi matumizi ya mswaki wenyewe kuliko ya dawa hiyo.
Badala ya dawa ya meno vinaweza kutumika chumvi na magadi.
Dawa ya meno hayatakiwi kumezwa kutokana na floridi iliyomo. Ikimezwa kidogo si hatari sana, lakini kama ni kiasi kikubwa ni lazima kuomba msaada wa daktari.[2]
Dawa ya meno iliyotengenezwa kwa kusaga mifupa au chaza ilianza kutumika katika Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale.[3]
Matumizi yake yalienezwa hasa katika karne ya 19.
Nchi mbalimbali zimekataza aina kadhaa za dawa ya meno kutoka China kwa sababu zina sumu aina ya diethylene glycol (kifupi diglycol au DEG).[4]

No comments:

Powered by Blogger.