Afya ya kinywa na meno kwa watoto
Afya ya kinywa na meno kwa watoto- dondoo kwa wazazi na walezi
Utangulizi
Afya bora ya kinywa na meno kwa mtoto ni muhimu
sana na ina uhususiano wa moja kwa moja na
afya yake kwa ujumla. Humuepusha mtoto kupata
maumivu, uwezekano wa uambukizo, kumfanya
aweze kutafuna vizuri ili kupata virutubisho muhimu
kwa ajili ya kujenga kinga dhidi ya magonjwa, na
kusaidia ukuaji. Afya nzuri ya kinywa na meno
pia itamfanya mtoto aweze kuhudhuria masomo
ipasavyo na hivyo kupata matokeo mazuri.
Umuhimu wa meno ya utoto
Wazazi /walezi wengi hujiuliza kwanini wahangaike
kutunza meno ya utoto ambayo yanatarajiwa
kung’oka na kuota ya ukubwa. Meno ya utoto ni
muhimu kutokana na sababu zifuatazo:
• Humsadia mototo kutafuna na hivyo
kumwezesha kupata virutubisho muhimu
• Hutunza nafasi kwa ajili ya meno ya ukubwa
na hivyo
• Hali ya afya ya meno ya utoto huathiri hali
ya afya ya meno ya ukubwani
• Husadia uumbaji wa maneno (kuongea)
Kama mzazi / mlezi unatakiwa kuwa mstari wa
mbele kutunza meno ya mtoto wako kwani, watoto
hupenda kujifunza kutokana na mfano wa wazazi.
Zifuatazo ni dondoo muhimu kwa wazazi/walezi
kwa ajili ya kutunza afya bora ya mtoto:
Umri wa kuzaliwa mpaka miezi 6
• Mnyonyeshe mtoto maziwa ya mama pekee
hadi umri wa miezi sita.
• Maziwa ya mama ni muhimu sana kwa
ukuaji na kinga dhidi ya magonjwa.
Umri wa miezi 7 hadi miezi 18
• Usimlaze mtoto akiwa na chuchu ya maziwa
au chuchu ya mama mdomoni ili kuzuia
ugonjwa wa kuoza kwa meno (rampant
caries)
• Mpatie mtoto maji badala ya juisi akiwa na
kiu.
• Iwapo utampa mtoto juisi ya boksi
unashauriwa kuongeza kiwango cha maji
sawa na kile cha juisi ili kupunguza kiasi
cha sukari kilichomo ndani ya juisi.
• Ukitengeneza juisi nyumbani kwa ajili ya
mtoto, jiepushe kuiongezea sukari.
• Jino la kwanza litakapoota, anza kusafisha
kinywa cha mtoto kutumia kitambaa laini
kilicholoweshwa kwenye maji safi au
mswaki laini bila dawa.
• Panga miadi ya kwanza ya kumwona
daktari wa meno (first appointment) wakati
mwanao hana maumivu au shida yoyote ili
kujenga mahusiano mazuri kati ya mtoto na
daktari
Umri wa miezi 18 hadi miaka 6
• Dhibiti ulaji wa vyakula vyenye sukari na
zingatia ulaji wa vyakula vinavyojenga afya
ya mtoto kama matunda, mboga mboga,
karanga, maziwa na samaki.
• Safisha meno ya mtoto kutumia maji safi
na mswaki laini na dawa ya meno (zingatia
kiwango cha dawa: kiasi cha mbegu ya
kunde) asubuhi na jioni kila siku.
• Mtoto asukutue mdomoni ili kupunguza
kiwango cha dawa itakayobaki.
• Chunguza mara kwa mara meno ya mtoto
ili kugundua dalili za mwanzo za ugonjwa
wa kuoza kwa meno (rangi kuwa nyeupe au
kahawia zaidi katika eneo husika baada ya
No comments: