Header Ads

Homa ya matumbo

Homa ya matumbo

Homa ya matumbo (kwa Kiingereza typhoid fever) husababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella TyphiUgonjwa huu huambukizwa kwa mtukula au kunywa chakula au maji yaliyo na kinyesi cha mtu aliyambukizwa.[1] Bakteria hawa hutoboa na kunyonya chakula kwenye matumbo ya binadamu.




Dalili

  • Homa kali
  • Kutoka kwa jasho jingi
  • Kuharisha (bila ya kutoa damu)
  • Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.
Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.
Katika wiki ya kwanza:
  • Joto la mwili huongezeka
  • Kichwa huuma
  • Kukohoa
  • Damu kutoka kwa pua, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
  • Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea
Katika wiki ya pili:
  • Homa huongezeka
  • Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
  • Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
  • Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
  • Kutapika kwa mgonjwa
  • Ini la mgonjwa huvimba
  • Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.
Wiki ya tatu:
  • Matumbo hutoa damu.
  • Matumbo hutoboka
Wiki ya tatu ikimalizika, homa huanza`kutulia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.

Matibabu[hariri | hariri chanzo]

Mara nyingi, homa ya matumbo haiui binadamu. Dawa kama ampicillin, chloramphenicol, trimethoprim-sulfamethoxazole, amoxicillin and ciprofloxacin hutumika kutibu wagonjwa katika nchi zilizoendelea.

Hatua za kuzuia kupata homa hii[hariri | hariri chanzo]

Daktari akimpa mtu chanjomjini San Augustine County, Texas
  • Usafi wa mazingira na wa kinafsi ni hatua bora ya kujikinga kutokana na ugonjwa huu.
  • Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hiyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
  • Homa hii huweza kuenea kwenye mazingira ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kingo bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
  • Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majina Typhim Viiliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherix iliyotengenezwa na GlaxoSmithKline.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2004-2005, janga la homa ya matumbo lilizuka katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoathiri watu 42,000 na kuua watu 214 (kulingana na ripoti ya shirika la World Health Organization).

Waathiriwa maarufu[hariri | hariri chanzo]

  • Mary Mallon, aliyejulikana kama Typhoid Mary.
  • Louisa May Alcott, mwandishi wa Little Women.
  • Charles Darwin, mwanasayansi, aliathirika pindi alipoenda nchini Chile mnamo 1835.
  • Eugenia Tadolini, alikufa mjini Paris mnamo 1872.
  • William Wallace Lincoln, mtoto wa tatu wa Abraham Lincoln, ambaye ni rais wa 16 wa Marekani, pamoja na Mary Todd Lincoln, walifariki kutokana na maradhi haya mnamo 20 Februari 1862.
  • Wilbur Wright, alikufa mnamo 30 Mei 1912 baada ya kuugua homa hii.

No comments:

Powered by Blogger.