Header Ads

Vifahamu Vyakula vya kuepukwa na Wajawazito

Siku mbili zilizopita tuliweza kuona vyakula ambavyo mama mjamzito anapaswa kuvitumia lakini wiki hii tutaweza kuona vyakula ambavyo mama mjamzito anatakiwa kuviepuka.



Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu,akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora Na sahihi Kwa kiumbe kilichomo tumboni Ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka.

Kwa siku la leo, tunaangalia arodha ya vyakula vilivyokatazwa. Mama mjamzito haruhusiwi kuvila vyakula vifuatavyo Kwa faida ya kiumbe kilichomo tumboni Na Kwa faida yake mwenyewe.

NYAMA MBICHI
Epuka kula samaki au nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri utajiepusha Na uwezekano wa kula bacteria na vijidudu vingine hatari kwa afya ya mtoto tumboni. Mjamzito anapokula nyama, anatakiwa kuhakikisha imeiva sawasawa.



SOSEJI NA SANDWICHI
Mjamzito haruhusiwi kula soseji, sandwichi za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama. Inaaminika kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea vyakula kama hivyo, huwa vimewekewa vihifadhi vyakula (preservatives) ambavyo vinaweza visiwe vizuri kwa afya ya mtoto.


SAMAKI WENYE ZEBAKI (MERCURY)
Wajawazito wamekatazwa kula samaki wenye kiasi kingi cha madini ya zebaki. Ulaji wa zebaki kwa wajawazito umehusishwa  na uzaaji wa watoto taahira. Mfano  wa samaki hao ni pamoja na papa, chuchunge na dagaa wakubwa.

MAYAI MABICHI
Ulaji wa mayai mabichi au vyakula vilivyochanganywa  na mayai mabichi, mjamzito haruhusiwi kuvila. Kuna baadhi ya ice cream na mayonaizi hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi. Mjamzito amekatazwa kuvila vyakula hivyo.


MAINI
Maini yana kiwango kikubwa cha madini aina ya chuma. Hata hivyo, yana kiasi kikubwa cha vitamin A ambacho huweza kuwa na madhara kwa mtoto kikizidi.

MAZIWA MABICHI
Maziwa mabichi huweza kuwa  na bacteria ajulikanae kama ‘listeria’ ambaye huweza kusababisha kuharibika kwa mimba. Unapokunywa maziwa, hakikisha yamechemshwa au kama ni ya paketi hakikisha ni yale yaliyoandikwa pasteurized na unpasteurized.

POMBE

Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa unywaji wa pombe kiasi kidogo wakati wa ujauzito hauna madhara kwa maana hiyo matumizi ya pombe hayaruhusiwi kabisa wakati wa ujawazito, hata kama ni kidogo. Unywaji wa pombe wakati wa ujauzito huweza kuathiri ukuaji mzuri wa mtoto. Kutegemeana na kiasi atakachokunywa mjamzito, pombe inaweza kumsababishia mtoto ugonjwa hatari utokanao na pombe (fetal Alcohol Syndrome).

1 comment:

Powered by Blogger.