Header Ads

NJIA PEKEE RAHISI, NAFUU, YA ASILI, NA ISIYOSHINDWA KATIKA KUONDOA HARUFU MBAYA YA MDOMO


NJIA PEKEE RAHISI, NAFUU, YA ASILI, NA ISIYOSHINDWA KATIKA KUONDOA HARUFU MBAYA YA MDOMO
Harufu mbaya ya mdomo inasababishwa na bakteria.
Huu ni ugonjwa unaofahamika kitaalamu kama halitosis.
Ugonjwa huu unatokana na tabia isiyofaa ya kutotunza kinywa. Na endapo mdomo wako unatoa harufu mbaya sana basi ni dalili za tatizo kubwa zaidi.
Kutoa harufu mbaya mdomoni kunaweza kuwa kubaya zaidi kutokana na aina ya vyakula unavyokula na mwenendo mbovu wa lishe.
KILE UNACHOKULA KINAATHIRI HARUFU YA MDOMO
Kimsingi vyakula unavyokula hupondwapondwa kwa kuanzia mdomoni. Endapo unakula vyakula vyenye harufu kali, kama vile vitunguu maji na vitunguu saumu, harufu kali itabaki kinywani. Kupiga mswaki au kusukutua kwa dawa ya maji ya meno hakutaonda harufu hiyo. Harufu haitaondoka mpaka baada ya muda mrefu kidogo.
Vipande vya vyakula ulivyotafuna hujishikiza katikati ya meno na kwenye fizi. Hivi ndivyo hushambuliwa na bakteria na kusababisha kutoa harufu endapo hautakuwa na tabia ya kupiga mswaki au kusukutua mdomo kila baada ya mlo.
UNAKABILIANAJE NA TATIZO LA KUTOA HARUFU MDOMONI?
Wengine hutumia jojo au pipi.
Wengine hula ndizi asubuhi na mapema, hasa kwa wenye hangover ya pombe.
Wengine hutumia maji moto.
Na wengine hutumia bidhaa za viwandani kusukutua mdomo.
Lakini njia hizi zote hufanikisha jambo moja: huondoa harufu ya mdomo kwa muda tu.
Unaweza kuondoa harufu na hata kutibu mdomo wako kwa kutumia mchanganyiko wa asili unaopatikana nyumbani kwako. Tena kwa bei rahisi.
Hebu tuone unawezaje kujitengenezea tiba hii rahisi na maridhawa.
ASALI, MDALASINI, LIMAO
Vitu vitatu vikuu kukusaidia kuanza kunukia:
Asali halisi na mbichi ina sifa za kukabiliana na bakteria. Asali itaua bakteria wabaya wote ndani ya mdomo, tofauti na sukari ambayo huchochea kuzaliana kwa bakteria hao mdomoni.
Mdalasini huua bakeria wasababishao harufu mbaya. Kimsingi tunashauriwa kuwa na mazoea ya kutafuna mdalasini kila siku.
Na kwa hakika Muungano wa Kimataifa wa Utafiti wa Tiba ya Kinywa (International Association for Dental Research) uligundua kuwa watu waliotafuna mdalasini walibainika kupunguza maambukizi ya bakeria wabaya wa kinywa kwa asilimia 50.
Limao ina sifa ya kung’arisha meno. Ina ladha ya kupendeza, inayoburudisha, na husafisha kinywa kwa kuwaondoa bakteria waliojificha ndani kabisa ya fizi na meno.
Zingatia tu kwamba unapoandaa dawa ya kinywa usiweke limao nyingi kwa sababu inaweza kuharibu meno.
JINSI YA KUANDAA DAWA YA KUKABILIANA NA HARUFU YA MDOMO
Mchanganyiko:
• Juisi iliyotokana na limao 2 zilizovunwa hivi karibuni.
• Nusu kijiko (1/2) ya unga wa mdalasini.
• Nusu kijiko au kijiko kimoja cha baking soda (sodium bicarbonate)
• Kujiko 1 cha asali
• Kikombe kimoja cha maji moto kiasi
• Chupa safi au kikombe safi
MAELEKEZO
1. Changanya vyote hivi kwenye chupa safi au kikombe tupu kisha tikisha moaka vichanganyike sawia.
2. Baada ya kupiga mswaki sukutua kwa dakika chache mchanganyiko huu.
3. Usisukutue mchanganyiko huu zaidi ya mara moja kwa siku. Tumia asubuhi zaidi.
Furahia harufu nzuri na murua baada ya siku chache. Utaona mabadiliko.

No comments:

Powered by Blogger.