Header Ads

Vyakula vinavyopunguza kichefuchefu kwa wajawazito

Miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito, (first trimester) ni muda wa mabadiliko mbalimbali kimwili na kisaikolojia kutotokana na homoni za uzazi kuzalishwa kwa wingi zaidi. Mabadiliko haya hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, na pia kwa mwanamke mmoja kwa nyakati tofauti (ujauzito tofauti).
Kichefuchefu ni dalili nzuri kwa wajawazito maana huonyesha hormone za mimba zipo juu, hormorne husaidia maendeleo mazuri na ukuaji wa mtoto aliye tumboni. Kipindi hiki cha ujauzito, mwili wa mama unatengeneza hormone inayoitwa human chorionic gonadotrophin(hcg) kwa kiwango kikubwa. Kuumwa kwa mama huuanza kupungua ujauzito unapofikisha kati ya wiki 12 na 14.



Wanawake 8 kati ya 10 hupitia hii hali, hivyo ni hali ya kawaida sana kwa wanawake wengi. Ni kitu ambacho huja na kuondoka bila madhara makubwa. Lakini kama mama mjamzito anatapika kupita kiasi hadi anaishiwa nguvu, chakula na maji mwilini basi anahitaji kupata uangalizi wa wataalamu wa afya au daktari.

Ni vigumu sana kuzuia kabisa hii hali kwa mama mjamzito mana ni mabadiliko ya mwili kuweza kupokea kiumbe kijacho, lakini unaweza kupunguza kiasi tatizo na madhara yake kwa homa za asubuhi.

Njia za kuzuia homa za asubuhi (morning sickness)


1. Kula kidogo mara nyingi zaidi kwa sikuNi vizuri kula kidogo kidogo mara nyingi kuliko kula chakula kingi kwa milo mitatu kwa siku. Kula mara nyingi husaidia kuongeza sukari mwilini sababu hali ya uchovu na ugonjwa huweza kusababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu. Sukari ndio chanzo cha nguvu mwilini. Chakula cha mara kwa mara humpa mama kiasi cha nguvu za kutosha kwake na kwa mtoto kwa muda wote. 

2. Andaa potato chips
Chumvi iliyomo kwenye viazi husaidia kukausha mate ambayo huwafanya baadhi ya wajawazito kuhisi kutapika mara kwa mara. Pia, wanga uliomo kwenye viazi husaidia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.

3. Tumia limao au ndimu
Limao au ndimu vina uchachu ambao husaidia kukata hali ya kichefuchefu. Kata limao na nusa, harufu ya limao itasaidia kupunguza hii hali ya kutapika. Pia unaweza ukakamulia limao kwenye chai au maji ukanywa. Unaweza pia kunusa maganda au majani ya limao maana husaidia pia kupunguza hali ya kichefuchefu.

4. Kula vyakula venye protini na vitamin B6
Vyakula venye protini kwa wingi na vile vyenye vitamin B6 humfanya mama apunguze hali ya kichefuchefu. Inashauriwa mama mjamzito aepuke kula vyakula venye viungo vingi, mafuta au vilivyokaangwa kwa muda mrefu sana. Vyakula hivi huweza kuzidisha hali ya kichefuchefu na kutapika balada ya kuiondoa.

5. TangawiziTangawizi hupunguza hali ya kichefuchefu, hivyo unaweza kuitumia kwenye chai. Kuwa makini, tumia tangawizi kiasi na usiweke nyingi.

6. Pata kifungua kinywa kabla ya kutoka kitandani
Mama mjamzito anashauriwa apate kifungua kinywa akiwa bado kitandani. Hali ya kuamka na tumboni hakuna kitu huweza kuwa chanzo cha kuhisi kichefuchefu na kutapika. Sasa ni vizuri ukapata kifungua kinywa ukiwa bado umepumzika. Kula mkate mkavu, cereals kavu au kitafunwa chochote kikavu, kula taratibu.

7. Pumzika muda mrefu inavyowezekanaNafahamu si rahisi kwa wajawazito wote kupata muda wa kupumzika manaa wengine ndo watendaji wakuu nyumbani, lakini inapopatikana nafasi ya kupumzika ni vizuri mama apumzike. Stress au uchovu unaweza kusababisha mama kuzidi kujisikia vibaya na hali ya kuumwa ikawa palepale. 

8. Epuka sehemu zenye joto
Usikae sehemu zenye joto, pendelea kukaa sehemu zenye kivuli, hewa na upepo mzuri. Hewa ni kitu muhimu sana kwenye kumfanya mama ajihisi vizuri. Pia mama aepuke sehemu zenye mikusanyiko ya watu na hewa nzito.

9. Kunywa maji mengi
Kunywa maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion). Ni vizuri kunywa lita 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai au juice za matunda zisizo na sukari ya kuongeza au kemikali za viwandani.

10. Usile na kunywa wakati mmoja
Kunywa vinywaji, hasa vyenye sukari, nusu saa kabla au baada ya mlo kamili na bora. Epuka kunywa vinywaji wakati wa chakula. Uwepo wa sukari huweza kuleta kichefu chefu na kumfanya mama atapike

11. Kunywa pregnancy multivitamin Wakati mwengine ni vizuri kumuona daktari ili kupata maelekezo ya dawa ambazo ni salama kuzitumia kupunguza hali ya kutapika. Pia kama kuna uwezekano wa kupata dawa zinazoweza kurudisha virutubisho muhimu mwilini, ikiwa ni pamoja na folic acid na vitamin D. Ila usitumie dawa bila ushauri wa daktari.

12. Preggie pops Hizi ni pipi ambazo hushauriwa kwa wamama wajawazito. Hazina madhara yoyote kwenye ujauzito lakini ni vizuri pia kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia. Pipi hizi humsaidia mama kupunguza kichefu chefu na hazina madawa. Zinapatikana kwenye ladha mbalimbali.

No comments:

Powered by Blogger.