Header Ads

HIZI NDIZO KANUNI 8 ZA AFYA BORA

Afya ni kitu muhimu na cha thamani katika maisha ya mwanadamu. Kwani mwanadamu akiwa na afya njema ataweza kukabiliana na majukumu yake ya kila siku. Kwakua na afya njema pia mwanadamu huweza kuwa na fikira mpya pamoja na mtazamo chanya katika swala la maendeleo. Afya njema humsaidia mwanadamu kujitunza mwenyewe na kutunza familia yake. Humsaidia kutimiza wajibu wake kwa jamii inayo mzunguka na hata kwa taifa zima. Kwakua na afya njema taifa litapata watu makini na viongozi bora ambao watashirikiana kwa pamoja kwa ajili ya kuinua uchumi na maendeleo yataifa.



Swali la kujiuliza:-Je, afya bora hupatikanaje? Zifwatazo ni kanuni nane za afya. Ambazo kama
mtu akiishi kwa kuzifwata atakuwa na afya bora.

1. Lishe bora.
Hapa ninamaanisha mlo mwanadamu anaopaswa
kula unatakiwa uwe mlo kamili wenye aina za
makundi yote ya chakula.

2. Mwanga wa jua.
Kila mwanadamu anapaswa kupata mwanga wa jua.
Jua la asubuhi nizuri katika miili yetu kwani
hurutubisha miili na kuipa virutubisho ngozi ya
mwanadamu.

3. Kiasi.
Kila kitu mwanadamu anachokifanya anatakiwa
kuwa na kiasi.

4. Hewa safi.
Mazingira yetu tunayoishi ni lazima yawe na hewa
safi. Miti na mimea ya asili itunzwe vizuri kwa ajili
ya kutoa hewa safi.

5. Mazoezi.
Kila mwanadamu anatakiwa afanye mazoezi ili
kuujenga na kuuweka mwili katika hali nzuri.
Mazoezi yanafaida kubwa katika miili yetu na hivyo
imetupasa kufanya mazoezi.

6. Maji safi.
Maji ni muhimu kwa afya zetu. Maji hayana
mbadala. Wapo watu huwa soda na juisi badala ya
maji. Pendekezo langu kunywa maji mengi kila siku
kwani "MAJI NI UHAI".

7. Pumziko.
Miili yetu inahitaji kupumzishwa. Katika kila masaa
24 nilazima angalau upate masaa kuanzia 5 hadi 8
kwa ajili ya kupumzisha na kutuliza akili yako. Na
katika siku saba za wiki kumbuka kupumzika katika
siku moja.

8. Kumtegemea Mungu.
Mungu ndiye Muumbaji wetu. Kumbuka
kumtegemea na kuweka matumaini yako kwake.
Tunaishi katika ulimwengu usio na matumaini lakini
Ukimtegemea Mungu utawezakuwa na matumaini
katika ulimwengu usio na matumaini.
Kumbuka AFya ni bora kuliko tiba.

No comments:

Powered by Blogger.