Header Ads

Kuoza kwa meno


Kuoza kwa meno

Jump to navigationJump to search
Kuoza kwa meno
Mwainisho na taarifa za nje

Destruction of a tooth by dental caries. This type of decay is also known as root decay.
ICD-10K02.
ICD-9521.0
DiseasesDB29357
MedlinePlus001055
Kuoza kwa meno (caries ni neno la Kilatini kutoka "rottenness"[1]), pia hujulikana kama kuoza kwa jinokaviti, au caries, ni kuharibika kwa meno kutokana na shughuli za bakteria.[2] Kaviti inaweza kuwa na aina tofauti za rangi kutoka kijani kibichi hadi nyeusi.[3] Dalili zinaweza kujumuisha maumivu na ugumu wa kula chakula.[4][3] Matatizo yanaweza kujumuisha inflamesheni ya tishu zinazozunguka jinokupoteza jino, na maambukizi au usaha hutokea.[1][3]

Kisababishi[hariri | hariri chanzo]

Bakteria huharibu tishu ngumu ya meno (enamelidentini na sementamu) kwa kutengeneza asidi kutoka kwa mabaki ya chakula kwa sehemu ya jino.[5] Sukari nyepesikatika chakula ni chanzo cha nguvu ya kimsingi ya bakteria na kwa hivyo lishe ya juu iliyo na sukari nyepesi ni swala la hatari.[5] Ikiwa uharibifu wa madini ni mkubwa kuliko ujenzi kutoka kwa vyanzo kama vile mate, matokeo ni kuoza kwa meno.[5] Maswala ya hatari inajumuisha hali zinazoleta matokeo ya mate kidogo kama vile: ugonjwa wa kisukariSindromu ya sjogren na baadhi ya matibabu.[5] Matibabu yanayopunguza utoaji wa mate yanajumuisha antihistamines na dawa za kupunguza makali na mengine.[5] Kuoza kwa meno pia kunahusishwa na umasikini usafishaji wa mdomo, na kurudi hali ya hapo awali ufizi wa meno inayoleta athari kwa mizizi ya meno.[6][2]

Uzuiaji na matibabu[hariri | hariri chanzo]

Uzuiaji hujumuisha: usafishaji wa meno kila wakati, lishe iliyo na sukari ya chini na kiwango kidogo cha floridi.[5][4] Kupiga meno mswaki mara mbili kwa siku na kusafisha katikati ya meno mara moja kwa siku unapendekezwa na wengi.[2][7] Floridi inaweza kutokana na maji, chumvi au dawa ya meno na vyanzo vinginevyo.[4] Kutibu meno ya mama yaliyooza kunaweza kupunguza hatari kwa watoto wake kwa kupunguza idadi fulani ya bakteria.[5] Uchunguzi unaweza kuleta utambuzi wa mapema.[2] Kulingana na kiwango cha uharibifu, matibabu kadhaa yanaweza kutumika urejeshaji meno kwa hali yake ya kufanya kazi au jino linaweza kutolewa.[2] Hakuna mbinu inayojulikana kurudia hali ya awali viwango vikubwa vya jino.[8] Matibabu yaliyopo katika nchi zinazostawi ni duni kila mara.[4] Paracetamol (acetaminophen) au ibuprofen inaweza kutumiwa kutuliza maumivu.[2]

Epidemiologia[hariri | hariri chanzo]

Kote duniani, takribani watu bilioni 2.43 (asilimia 36 ya idadi ya watu)  wana meno yaliyooza ya kudumu.[9] Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa karibu watu wote wazima huwa na meno yaliyooza kwa wakati fulani.[4] Meno ya watoto wachanga huathiri karibu watu milioni 620 au asilimia 9 ya idadi ya watu.[9] Uozaji wa meno hutokea sana kwa watu wazima na watoto kwa miaka ya hivi karibuni.[10] Ugonjwa huu unapatikana sana katika nchi zinazostawi na kiasi kwa nchi zilizostawi kwa sababu ya matumizi ya sukari kiasi.[2]

No comments:

Powered by Blogger.