Header Ads

FAHAMU CHUNUSI NI NINI, NA HUSABABISWA NA NINI??


Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao husababishwa na uwepo na utendaji kazi wa tezi ya mafuta iliyopo kwenye ngozi chini ya shina la vinyweleo. Tatizo hili la
chunusi huwa ni la kawaida kwa mtu aliyebalehe kwa vile ni katika kipindi hiki ndipo tezi hii ya mafuta iliyopo katika ngozi huanza kufanya kazi.




Chunusi huweza kujitokeza katika maeneo mengi, lakini maeneo ambayo hushambuliwa zaidi na chunusi ni maeneo ya paji la uso,mgongoni, kifuani, mabegani na shingoni.

Chunusi husababishwa na nini?

Kabla ya kufahamu ni jinsi gani chunusi hutokea ni vyema kujua kwa ufupi sayansi ya ngozi kimuundo,

  Ngozi ya binadamu ina vitundu vidogo ambavyo huonekana kama ni vishina vya vinyweleo, vishimo hivyo huelekea sehemu ya ndani ya ngozi mpaka karibu na tezi za mafuta, kati ya vishimo hivyo na tezi za mafuta kuna mifereji ambayo inaunganisha vishimo hivyo pamoja na tezi za mafuta. Kazi ya tezi hizi za mafuta ni kuzalisha kimiminika mfano wa mafuta(sebum) ambayo hufanya kazi kama gundi kwa kukusanya seli zote zilizokufa ndani ya ngozi na kuzitoa nje ya ngozi kupitia vishimo vinavyojitokeza nje ya ngozi.

Sababu za kutokea kwa chunusi.
Hakuna sababu za uhakika za kwanini chunusi hutokea lakini kwa sasa wataalamu wa afya wanaamini kuna sababu kuu mbili zinazosababisha chunusi mbazo ni;
  • Kuongezeka kwa homoni ya androgen.
Homoni hii huzalishwa mara tu baada ya mtu kubalehe, kuongezeka kwa homoni hii mwilini kunasababisha kupevuka na kuongezeka kwa tezi ya mafuta ya ngozi hivyo kuongeza uzalishaji wa sebum. Kiwango kikubwa cha sebum kinasababishwa kuharibika kwa kuta za vishimo vya vinyweleo na mifereji yake na hivyo kiwango kikubwa cha sebum kinashindwa kutolewa jambo ambalo hukaribisha vimelea kama bacteria katika vishimo hivyo.
Uwepo wa bakteria katika vishimo unasababisha kutengenezwa kwa uvimbe kama sehemu ya njia za mwili katika kupambana na vimelea. Uvimbe unaotokea unaweza kuwa wa kawaida au kuwa mkubwa kupita kiasi hii inategemea sana na aina ya bakteria waliovamia eneo husika.
    • Sababu nyingine zinazoweza sababisha kuharibika kwa vishimo hivi ni matumizi ya mafuta mazito ya kupaka, mafuta mazito huziba vishimo hivi na hivyo kusababisha mlundikano wa uchafu katika vishimo hivyo. Mlundikano huu wa uchafu unaweza kukaribisha vimelea au unaweza tengeneza uvimbe.
  • Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito- mama mjamzito hukumbata na mabadiliko makubwa ya homoni mwilini mwake , mabadiliko haya ya homoni huweza kusababisha uzalishwaji mkubwa wa sebum ambao hupelekea chunusi.
  • Pia wataalamu wa afya wanataja kuwa tatizo la chunusi laweza kuwa ni la kurithi, kwa maana matatizo yanaweza kuwa ni katika chembe za urithi(vinasaba) katika familia fulani.

No comments:

Powered by Blogger.