Header Ads

JE KISUKARI KINA TIBA? PATA KUFAHAMU HAPA!


Kisukari ni ugonjwa unaotokana na sukari ya mwili kuwa juu kupita kiwango kinachotakiwa.
Glucose ni zao la mwisho la mmeng'enyo wa chakula ambalo husharabiwa na seli za mwili kwa ajili ya kuzipatia seli nishati ya kufanya shughuli nyingine za mwili. zao hili ni aina ya sukari ambayo hupatikana katika vyakula tofauti ambavyo tunavitumia, kama vile vyakula vya wanga na protini vyote hivi hupelekea kutengenezwa kwa glucose na baada ya kutengenezwa glucose husafirishwa mwilini kote kupitia damu.Damu hufikisha sukari hii kila pande ya mwili na seli zote zenye uwezo wa kuiunguza sukari ili itoe nishati huipokea sukari hii kwa msaada wa homoni za insulini.

 Insulini inafanya kazi kwa namna mbili, moja husaidia kufunguka kwa milango ya seli ili glucose iingie ikaunguzwe itoe nishati na pia hufanya kazi ya kubadili glucose yeyote iliyozidi kwenda katika muundo glycogen(muundo ambao sukari yaweza hifadhiwa bila madhara).

 Kwa maana hii basi kiwango cha sukari mwilini hurekebishwa na homoni ya insulini, hitilafu yeyote itakayotokea na kudhoofu utendaji kazi wa insulini utasababisha sukari ya mwili kuwa juu na hapo tunasema mtu huyo ana kisukari.

Tatizo hili linaweza sababishwa kwa namna kuu mbili ambazo ni;
  • Mwili kushindwa kuzalisha homoni za insulini- homoni hii hufanya kazi ya kubadili sukari ya ziada mwilini kutoka hali ya hatari (glucose) kwenda katika hali ya usalama(glycogen) ili iweze kuhifadhiwa mwilini. Hivyo kukosekana kwa homoni hiyo kunasababisha sukari ya mwili katika damu kuwa juu kupita kawida.

  • Sababu ya pili ni pale mwili unatengeneza kiwango kidogo cha homoni ya insulini ambayo haikidhi haja au seli za mwili zinashindwa kutambua uwepo wa dutu za homoni ya insulini na hivyo kushindwa kufanyiwa kazi kwa sukari ya mwili na kupelekea sukari ya mwili katika damu kupanda. Asilimia zaidi ya 90 ya matatizo ya kisukari yanaripotiwa kusababishwa na sababu hii.
Je kisukari kina tiba ?

Jibu ni hapana!?

Kisukari bado hakijapata tiba!  Kwa mtu ambaye kisukari chake kimesababishwa na mwili wake kushindwa kuzalisha homoni za insulini yeye hutumia tiba maisha yake yote, mpaka sasa watu hawa hutumia homoni za insulini za  kutengenezwa maabara ambazo hufanya kazi kama zile za asili kwa hivyo ili maisha yake yaendelee ni lazima apate tiba hii na pia mpaka sasa tiba hii hufanywa kwa njia ya sindano.


Pia,

Kwa wale ambao kisukari chao kinasababishwa na kiwango kidogo cha homoni ya insulini ambayo haikidhi haja au seli za mwili zinashindwa kutambua uwepo wa dutu za homoni ya insulini bado hakuna tiba.

Lakini habari njema ni kwamba!!

Mgonjwa wa kisukari ambacho hutokana na sababu ya pili anaweza kupunguza na kuondokana na magonjwa nyemelezi ambayo husababishwa na kisukari bila
kutumia dawa kwa kuzingatia kanuni bora za mlo kamili na mazoezi.

No comments:

Powered by Blogger.