Header Ads

UMUHIMU WA MAJI KATIKA KUTUNZA NA KUREFUSHA NYWELE ZAKO.

Maji ni muhimu kwa viumbe wote duniani, bila maji hakuna shughuli zozote ambazo zinaweza kuendelea katika mazingira yetu. Kwa maana hii ndio maana utasikia usemi ya kwamba “maji ni uhai.”.



Ni kewli kabisa maji ni uhai kwa vile yana kazi nyingi zaidi za nje na ndani ya mwili wa binadamu, kazi ambazo ndizo hufanikisha maisha kuendelea. Moja ya kazi kubwa kabisa ya maji mwilini ni kusaidia seli za mwili kufanya shughuli zake za kutengeneza na kuvunja dutu mbalimbali za mwili ikiwemo vyakula.
Michanganyo ya kikemikali ambayo huishia kutengenezwa au kuvunjwa kwa dutu mbalimbali za mwili zote hufanyika katika hali ya unyevu. Kwa hivyo bila maji hakuna uhai.

Nywele kama sehemu mojawapo ya mwili huhitaji virutubisho malimbali ikiwemo maji. Idadi kubwa ya watu duniani(hususa ni watu weusi) wana nyele za msokoto(kipilipili), kumekuwa na mitazamo ya kwamba nywele hizi haziwezi kukua na kurefuka kama jamii nyingine za nywele.

Je dhana hii ni ya kweli?

Hapana, dhana hii si ya kweli na nywele za msokoto zinaweza kukua na kuwa ndefu kama jamii nyingine za nywele ingawa kuna changamoto nyingi ambazo huwakabili watu wenye nywele hizi katika kuzikuza na kuzitunza. Kuna mambo mengi ambayo watu wenye nywele hizi za msokoto huyafanya wakidhani ni sahihi na yatasaidia kutunza na kurefusha nywele zao badala yake huishia kuharibikiwa na nywele zao na kuendelea kuamini ya kuwa nywele za msokoto haziwezi kurefuka kamwe.

Kama ilivyoelezwa hapo awali maji kama sehemu ya virutubisho vya mwili huhitajika na sehemu nyingi za mwili ikiwemo nywele. Maji huhitajika Zaidi na nywele kwa ukuaji kwa vile yana fanya kazi zifuatazo.
  •   Kuziweka nywele katika hali ya unyevu, kukatika au kunyofoka kwa nywele ni matokeo ya nywele kuwa kavu. Nywele za msokoto huhitaji maji mengi ili kuwa na unyevu. Unaweza kufanya hivyo kwa kunywa n kuziosha nywele zako kwa maji safi na salama.
  •   Maji husaidia kuweka mazingira rafiki ya unywevu katika shina la nywele hivyo kuwezesha utengenezwaji wa virutubisho muhimu kama protein kupatikana na kutengenezwa kwa urahisi Zaidi.

Mambo ya kuzingatia ili uweze kutumia maji kwa ajili ya afya ya nywele kwa mafanikio.

  •    Usitumie mafuta pekee kupaka katika nywele, paka mafuta baada ya kuosha nywele na maji safi na ya kutosha. Kwa kuwa mafuta huzuia maji kufyonzwa katika nywele. Utumiapo mafuta katika nywele  baada ya kuosha na maji yatasaidia kutunza maji yasipotee kwa muda mrefu hivyo kuziacha nywele katika hali ya unyevu.
  • Usitumie vifaa vyenye joto au kemikali kukaushia nywele zako kwa sababu vifaa hivi hufyonza maji mengi na kuziacha nywele zikiwa kavu na zenye kukatika kiurahisi Zaidi.
  •   Usioshe nywele zako maa kwa mara weka kawaida ya kuziosha kwa hadi mara 3 kwa wiki.
  •   Tumia njia iitwayo “GREENHOUSE EFFECT”. 
Jinsi ya kutumia njia hii.
  • Osha nywele zako na maji mengi yaliyo safi mpaka zilowe kabisa.
  • Futa maji kwa kutumia kitambaa safi na kisha zibane nywele zako kwa namna unayopenda.
  • Tumia kofia ya plastiki kuzifunga au kofia ya Rambo.
  • Unaweza kuziacha kwa muda wa hadi masaa 12 ukiwa umezifunga kwenye kofia ya plastiki. Inashauriwa ufanye wakati wa kulala na uzifunike usiku mzima.
  • Na baada ya masaa 12 unaweza kutoa kofia yako na kuzikausha vizuri kwani tayari zitakuwa zimenyonya maji ya kutosha.

No comments:

Powered by Blogger.