TATIZO LA KIUNGULIA HUSABABISHWA NA NINI? NA JE LINA TIBA? PATA KUFAHAMU HAPA.
Kiungulia ni tatizo katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ambalo husababishwa na kucheuliwa kwa mchanganyiko wa tindikali na chakula kutoka tumboni kuelekea katika koo la chakula(eneo kati ya umio na tumbo) mchanganyiko huu wenye tindikali huunguza maeneo haya na kusababisha maumivu makali katika koo la chakula.
Sayansi ya mfumo wa chakula.
Nyongo huzalisha tindikali iitwayo Hydrogen Chloride(HCl), tindikali hii ni kali sana na ina uwezo wa kumengenya hata chuma. tindikali hii huzalishwa na kusafirishwa tumboni ambako hutumika kumeng'enya chakula na kuangamiza vimelea ambavyo huweza kuwa hatari mwilini.
Tumbo limeundwa na ukuta madhubuti ambao unaweza kuvumilia hatari ambayo huweza kusababishwa na tindikali hii katika seli za kawaida za mwili kumbuka tindikali hii ni moja kati ya sababu zinazopelekea vidonda vya tumbo endapo ukuta wa tumbo utapoteza umathubuti wake.
Tindikali hii ni salama ikiwa katika tumbo pekee kwa vile sehemu nyingine za mfumo wa mmen'enyo wa chakula hazina ukuta unaoweza stahimili tindikali hii. Moja ya sehemu ya mfumo ambao hushambuliwa zaidi na tindikali hii ni koo la chakula ambalo halijaundwa na ukuta stahimilivu dhidi ya tindikali hii hivyo basi kufika kwa tindikali hii katika koo la chakula husababisha kuunguzwa kwa eneo hili na kupelekea maumivu makali ya kufanana na moto.
Kati ya tumbo na koo la chakula kuna mlango ambao hurekebisha upitaji wa vyakula kati ya tumbo na koo la chakula, hivyo kuathiriwa kwa mlango huu ndio hasa sababu kubwa ya kiungulia, mlango huu huweza kuathiriwa kwa naman nyingi ikiwemo msukumo mkubwa chakula kutoka tumboni au kusinyaa na kutanuka kwa misuli inayorkebisha ufungukaji wa mlango huo.
Kiungulia husababishwa na nini?
Tatizo la kiungulia huwapata watu aina zote bila kujali jinsia, rangi au umri kwa kuwa yapo mambo mengi ambayo hupelekea mtu kupata kiungulia. kujiweka katika mazingira haya mara kwa mara kunaweza kupelekea kiungulia kuwa ugonjwa ambao huweza kukushambulia mara kwa mara.
Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kiungulia lakini kubwa ni kutumia vitu ambavyo hupelekea kutengenezwa kwa tindikali nyingi zaidi mwilini, vitu hivyo ni pamoja na;
Nini Dalili kuu za kiungulia!
Zifuatazo ni dalili za kiungulia;
Ndio, kiungulia kinaweza kutibiwa lakini pia unaweza kujikinga na hatari ya kupata kiungulia kwa kufanya mambo yafuatayo;
Nini hatari ya kutokutibu kiungulia cha mara kwa mara?Sayansi ya mfumo wa chakula.

- Vyakula ambavyo husababishwa kutengenezwa kwa tindikali nyigi kupita kiwango. mfano maharage, viazi na mihogo.
- Matumizi makubwa ya chumvi
- ukosefu wa vyakula vyenye ufumwele.
- Matumizi ya pombe na kafeini
- Kitambi
- Kutojihusisha na mazoezi.
- Matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za pumu na usingizi.
Nini Dalili kuu za kiungulia!
Zifuatazo ni dalili za kiungulia;
- Maumivu wakati wa kumeza chakula.
- Kutapika
- Kichefuchefu
- Maumivu ya kifua na tumbo
- Muwasho katika koo la chakula
- Harufu mbaya ya kinywa.
- Kushikwa na nimonia.
Ndio, kiungulia kinaweza kutibiwa lakini pia unaweza kujikinga na hatari ya kupata kiungulia kwa kufanya mambo yafuatayo;
- Matumizi ya dawa, hii ni kwa watu tayari wanaosumbuliwa na kiungulia, kuna dawa za aina tofauti za kutibu kiungulia ambazo hutofautiana kulingana na aina ya mgonjwa. mfano wa dawa hizo ni omeprazole, rabeprazole,cimetidine, ranitidine pamoja na antiacids(Calcium carbonate, sodium bicarbonate, aluminum, and Magnesium hydroxide.)
- Epuka vyakula ambavyo husababisha kiungulia kama chocolate, soda na juice zenye tindikali
- Usile chakula kingi kupita kiasi.
- Epuka kuvaa vitu vinavyobana tumbo baada ya kula mfano mshipi(mkanda wa suruali au sketi)
- Usilale kwa muda wa masaa 2-3 mara tu baada ya kula.
Kutokutibu kiungulia ambacho hukushambulia mara kwa mara ni hatari kwa afya yako kwa vile huweza kusababisha magonjwa kama vile;
- Uvimbejoto sehemu za koo la chakula. uvimbe huu huharibu koo la chakula kwa vile huweza kusababisha vidonda na koo kupoteza uwezo wa kufanya kazi.
- Kutengenezwa kwa kovu katika koo la chakula ambako kunapelekea koo la chakula kupoteza uwezo wa kufanya kazi.
- Kubadilika kwa seli za koo la chakula kunakopelekea koo la chakula kupoteza asili yake. tatizo hili kitaalamu huitwa Barrett's esophagus.
Magonjwa yote hapo juu ndio sababu kubwa ambayo hupelekea mataizo ya saratani ya koo la chakula na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa ujumla.
No comments: