Header Ads

TATIZO LA KISUKARI, HAYA NI MADHARA YA KUSHINDWA KUTIBU KISUKARI KWA WAKATI..!


Yafuatayo ni madhara ambayo mgonjwa wa kisukari anaweze kuyapata endapo atachelewa ama kushindwa kupata tiba ya kisukari.

  • Matatizo ya macho.
Kushindwa kutibu kisukari kwa wakati kunawezasababisha matatizo makubwa ya macho ambayo huweza kupelekea mtu kushindwa kuona kabisa. matatizo hayo ni pamoja na mtoto wa jicho, Glaucoma na mengineyo.


  • Matatizo ya miguu.
Matatizo ya mikuu ambayo huweza sababisha miguu kushidwa kufanya kazi hadi kukatwa. mfano neuropathia, Donda ngugu na kulika kwa nyayo za miguu na vidole.



  • Matatizo ya ngozi.
Watu walio na kisukari huwa katika hatari zaidi ya kushambuliwana na magonjwa mbalimbali ya ngozi ikiwemo yale ya vimelea vya kuvu.





  • Mataizo ya moyo.
Matatizo ya moyo kama kupungua kwa damu inayofika kwenye moyo, uvimbe katika moyo, kiharusi, Shinikizo la damu na mengine mengi.





  • Kudhoofu kwa afya ya akili.
Kisukari kinaweza kusababisha matatizo mbalimbali ambayo huathiri akili ya mtu, matatizo hayo ni pamoja na wasiwasi, huzuni, woga na upweke.






  • Kupungua kwa kinga za mwili.
Mgonjwa wa kisukari hukabiriwa na kudhoofu kwa kinga za mwili jambo ambalo humfanya kuwa rahisi kushambuliwa na maradhi.






  • Uhanisi.
Kisukari huweza kusababisha mwanaume kushindwa kisimamisha uume wake na kupoteza uwezo na nguvu ya kujamiana.





  • Neuropathia.
Ni matatizo yanayoweza kuukumba mfumo wa neva na kusababisha mu kupoteza uwezo wa kuhisi na kuitikia miguso.





  • Kuchelewa kupona kwa vidonda na majeraha.


ZINGATIA,
Ni vyema kuonana na wataalamu wa afya na kuzingatia matibabu kadri itakavyopendekezwa na daktari wako. kumbuka kisukari hakina tiba ili kuishi salama ukiwa na kisukari ni vyema kufuata ushauri wa daktari na kubadili mtindo wa maisha yako ili kulinda afya yako.

No comments:

Powered by Blogger.