SARATANI YA MATITI, TATIZO LINALOWATESA WATU WENGI DUNIANI WANAWAKE KWA WANAUME! LIFAHAMU ILI KUEPUKANA NALO.
Saratani ya matiti ni tatizo linalowapata watu wengi zaidi duniani wanawake kwa wanaume huku saratani hii ikiwashambulia zaidi wanawake. Katika makala hii tutaangazia zaidi saratani ya matiti kwa wanawake.
Saratani ya matiti kwa wanawake iko kwa kiwango kikubwa kwa nchi zilizoendelea ukilinganisha na zile zinazoendelea, hii inasababidhwa na sababu nyingi na tofauti kama vile umri wa kuishi, chakula, makazi na mitindo ya maisha.
Sayansi ya titi la mwanamke.
Matiti ya mwanamke aliyebalehe linakuwa na tishu za mafuta ambazo zinazunguka karibu titi lote ambazo kazi yake kubwa ni ulinzi na kurekebisha jotoridi ndani ya titi, tishu zinazolipa titi umbo lake, seli za mfumo wa neva, tezi za kuzalisha maziwa ambazo zimeunganishwa na chuchu kupitia mifereji maalumu wa maziwa.
Saratani ya matiti husababishwa na nini?
Saratani ya matiti husababishwa na ongezek la seli zilizopo kwenye matiti , ambalo mwili unashindwa kuliratibu na hivyo ongezko hilo linakosa udhibiti. Ongezeko hili hupelekea kutengenezwa kwa seli nyingi kupita kiwango ambapo seli hizo hutengeneza uvimbe mgumu. Uvimbe huu unakuwa na madhara kwa vile unaathiri utendaji wa kawaida wa kazi za seli, na mbaya zaidi ni kwamba hali hii ya ongezeko la seli lisilo na udhibiti linaweza kusambaa kwa seli zilizo jirani au hata seli za mbali na matiti jambo linalopelekea sehemu zote zilizoathiriwa na hali hii kupoteza uwezo wa ufanyaji kazi wa kawaida.Tatizo hili hushambulia zaidi sehemu za milija ipitishayo maziwa ya mama kutoka katika tezi za kuzalisha maziwa kuelekea katika chuchu.
Zifuatazo ni dalili za kuwepo kwa saratani katika matiti(titi);
- Uwepo wa donge(uvimbe) katika titi.
- Maumivu sehemu za ubavu au maumivu amabayo hayahusiani na mzunguko wa hedhi( kwa kawaida wanawake wengine hupata maumivu hasa maeneo ya chuchu pindi waingiapo hedhi)
- Uvimbe katika chuchu ambao huambatana na kama muonekano wa vishimo vidogo.
- Chuchu huweza kutoa damu au ugilgili wa njano.
- Kubadilika kwa umbo la chuchu( kusinyaa au kubadili uelekeo)
- Kubadilika kwa muonekano wa titi.
- Ngozi za chuchu au titi lote huanza kujimenya.
Ni vigumu kufahamu moja kwa moja kwamba saratani inasababishwa na nini kwa sababu jambo fulani linaweza sababisha madhara kwa mtu mmoja na lisisababishe madhara kwa mwingine, kwa hivyo yafuatazo ni baadhi ya mambo ambayo huweza kusababisha saratani kwa namna moja au nyingine;
- Umri mkubwa kwa wanawake- takwimu zinaonyesha asilimia 80 ya matatizo ya saratani ya matiti yanayoripotiwa ni ya wanawake wenye umri zaidi ya miaka 50.
- Uvimbe katika titi(matiti).
- Wanawake wenye matiti yenye tishu zenye tungamo kubwa wako katika hatari zaidi ya kupata saratani ya titi.
- Wanawake wanaowahi kubalehe, takwimu zinaonesha wanawake wanaowahi kubalehe huwa na kiwango kikubwa cha homoni ya estrojeni, uwepo wa kiwango kikubwa cha estrojeni katika mwili kunaongeza uwezekano wa kupata saratani ya titi.
- Fetma(kitambi)- wanawake wenye vitambi na uzito mkubwa kupita wastani hushambuliwa zaidi na saratani ya matiti kwa sababu wanawake hawa huwa na kiwango kikubwa cha estrojeni.
- Kimo- wanawake warefu wako katika hatari ndogo ya kupata saratani ya matiti kulinganisha na wanawake wafupi.
- Ulevi- wanawake wanaokunywa pombe huwa katika hatari zaidi ya kupata saratani kulinganisha na wanawake wasiotumia pombe.
- Matumizi ya tiba za mionzi au kuwa karibu na mionzi kama vile X-ray na CT scan husababisha kwa kiwango kikubwa saratani za aina mbalimbali mwilini.
- Tiba zinazohusisha mabadiliko ya homone( kuongeza homoni au kubadili mfumo au tezi za homoni).
- Matumizi ya urembo na vipodozi kama vile matumizi ya matiti ya bandia.
Ndio, saratani ya matiti hutibika lakini hutegemea na mambo yafuatayo, aina ya saratani, ni hatua gani saratani imefikia(je imesambaa au ipo eneo la awali(matiti)), Hali ya afya ya jumla ya mgonjwa, umri wa mgonjwa na utayari wa mgonjwa.
Saratani ya matiti hutibiwa kwa njia zifuatazo;
- Matibabu ya kutumia mionzi mfano x-ray.
- Matibabu ya upasuaji ambayo uhusisha uondoaji wa uvimbe uliosababishwa na saratani
- Matibabu ya kutumia dawa maalumu za saratani mfano trastuzumab
- Tiba za kuthibiti utengenezwaji wa homoni ambazo huongeza athari za saratani ya titi, mfano wa homoni hizo ni estrojeni na progesteroni.
ZINGATIA
Ni vyema kufanya uchunguzi wa afya wa mara kwa mara ili kufahamu matatizo ya kiafya ambayo huwa ni magumu sana kuonyesha dalili hasa katika hatua za awali. Mfano wa matatizo haya ni tatizo hili la saratani. Pia zingatia sababu zinazoweza sababisha saratani na uweze kuziepuka.
No comments: