Header Ads

YAFAHAMU MAGONJWA HATARI ZAIDI DUNIANI! HUSABABISHA ZAIDI YA 50% YA VIFO VYOTE DUNIANI!?


Haya ni magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watu ulimwenguni, magonjwa haya huchangia takribani asilimia zaidi 50% ya vifo vyote vinavyotokea na kurekodiwa ulimwenguni kote.





Orodha hii imehusisha taarifa kutoka shirika la afya duniani (WHO). magonjwa hayo ni kama ifuatavyo;

01. Kiharusi cha moyo (Ischemic heart disease.)

Huu ni udonjwa unaoshambulia mishipa ya damu ya kwenye moyo ambapo mishipa ya damu ya kwenye moyo hupungua umbo na kuwa miembamba kupita kawaida hivyo kuzuia kiwango cha damu kufika baadhi ya maeneo ya moyo, hii hupelekea moyo kushindwa kufanya kazi hatimaye kifo.
Kwamujibu wa (WHO) ugonjwa huu husababisha takribani vifo zaidi ya milioni 7 ambayo ni asilimia zaidi ya 12 ya vifo vyote duniani. taarifa hizi ni zile za mwaka 2012 hadi 2015.

Tatizo hili husababishwa na sababu kuu zifuatazo;
  • Kiwango kikubwa cha rehemu mwilini.
  • Shinikizo la damu.
  • Uvutaji
  • Uzembe na uvivu wa mwili.
  • Kushindwa kumudu uzito.
  • Kutopata mlo kamili.
02. Kiharusi cha ubongo (stroke). 
 
Kiharusi ni tatizo linalotokea katika ubongo ambapo mishipa inayopeleka damu safi  ya ateri katika ubongo hupasuka, huvuja au kuwa miembamba kushindwa kuruhusu damu kupita. Matokeo yake ni ubongo kushindwa kufanya kazi na seli zake kufa hatimaye kifo.
Kwa mujibu wa  (WHO) kiharusi cha ubongo husababisha takribani zaidi ya vifo milioni 6 kila mwaka ambayo ni zaidi ya asilimia 10% ya vfo vyote.
Sababu za kiharusi ni sawa na zile zinazosababisha ischemic heart diseases.

03. Magonjwa sugu ya Mapafu.(Chronic obstructive pulmonary disease)

Magonjwa sugu yanayoshambulia mapafu kama Broncitis sugu(bronchitis ni tatizo la uvimbe katika milija ya bronkioli ambapo milija hiyo hupungua unene na kusababisha ugumu wa upuaji) na Emphysema( emphysema ni tatizo linalotoke katika vifuko vya hewa vilivyopo katika mapafu ambapo vifuko hivyo husinyaa na kushindwa kupokea hewa).
Ka mujibu wa (WHO) ugonjwa huu husababisha zaidi ya 5% ya vifo vyote ambavyo ni takribani ya vifo milioni 3 ya vifo vyote duniani.
Zaidi ya watu milioni 50 duniani kote wanaishi wana tatizo hili.
Sababu kubwa ya ugonjwa hoo ni;
  • Kuvuta hewa chafu.
  • Uvutaji wa tumbaku
04. Magonjwa yanayoshambulia sehemu ya chini ya mfumo wa upumuaji.
 (Lower Repiratory Infections)
Haya ni magonjwa yanayoshambulia zaidi maeneo ya ndani ya mfumo wa upumuaji pekee maeneo hayo ni milija ya bronchioli, Trachea na mapafu. mengi ya matatizo haya ni yale ambayo hukua na kuwa sugu. magonjwa hayo ni pamoja na  kisamayu(pneumonia),bronchitis na homa ya mafua.
Kwa mujibu wa (WHO) idadi ya vifo vya ugonjwa huu ni sawa na ule wa homa sugu ya mapafu kwa vile lower respiratory infections ni maambuizi ya awali ambayo huendelea na kuwa sugu. 

05. Saratani ya Mapafu, Bronchioli na Trachea(bomba la pumzi).
(Respiratory system cancer) 

Hii hujumuisha saratani zote za mfumo wa upumuaji ambazo ndizo zinatajwa kuwa saratani zinazoongoza kwa vifo vya watu duniani  ambapo inaripotiwa zaidi ya watu milioni 1.5 hupoteza maisha kwa saratani hizi ikiwa ni asilimia zaidi ya 2.5% ya vifo vinavyoripotiwa.
Sababu kuu zikiwa ni;
  • Hewa chafu
  • Sumu katika mazingira(gesi za sumu)
  • Uvutaji.
 06. Ukimwi.( HIV/AIDS)

Upungufu wa kinga mwilini  ambao husababishwa na virusi aina ya HIV. limeendelea kuwa ni tatizo kubwa katika ulimwengu kwa muda mrefu sana ingawa vifo vyake vikionekana kushuka kwa kiwango kidogo. tangu kugunduliwa UKIMWI umesababisha vifo takribani milioni 40 duniani kote. na inaripotiwa kuwa zaidi ya watu milioni 35 huishi na virusi vya ukimwi huku maambukizi mapya yakikadiliwa kuwa ni zaidi ya watu 5000 huambukizwa kila siku. idadi kubwa ya maambukizi ni katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara ambapo huchangia zaidi ya 70% ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
 Kwa kila mwaka zaidi ya watu milioni 1.5 hpoteza maisha kwa UKIMWI ambayo ni zaidi ya  2.5% ya vifo vyote duniani.

07. Magonjwa ya kuharisha(Diarrheal Diseases)

Kuharisha ni husababishwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ambapo maambukizi hayo huweza kusababishwa na kula vyakula visivyo salama au kunywa maji yasiyosalama.
Tatizo hili husababisha kupotea kwa maji mengi mwilini ambako kuaathiri utendaji kazi wa mwili mpaka kusababisha kifo.

 Inakadiliwa zaidi ya vifo milioni 1.5 hutokea duniani kote ambayo ni zaidi ya 2.5% ya vifo vyote. kuharisha inatajwa kuwa ni ugonjwa wa pili unaosababisha vifo kwa watoto  baada ya malaria na ugonjwa huu uko kwa kiwango kikubwa katika nchi zinazoendelea ambako kuna changamoto ya utoaji huduma ya maji safi.

08. Kisukali (Diabetes)

kisukari ni tatizo linaloathiri utendaji kazi wa homoni ya insulin ambayo hufanya kazi ya kurekebisha sukari ya mwili.kushindwa kufanya kazi kwa homoni hii ni hatari kwa afya ya binadamu kwa vile tatizo hili huweza kusababisha matatizo mengine mengi na makubwa mwilini. tatizo hili hutokea ama kwa ini kushindwa kuzalisha homoni hizi au homoni hizi kuzalishwa kwa kiwango kidogo kiasi cha kushindwa kumudu kazi.
Kisukari huchangia asilimia zaidi ya 2.6% ya vifo vyote kwa mwaka huku ikitajwa kuwa ni zaidi ya watu milioni 1.5.
Sababu kuu ya kusukari ni;
  • Kutopata mlo kamili.
  • Kushindwa kufanya mazoezi.
  • Uzito kupita kiasi.
  • Fetma(kitambi)
09. Matatizo yanayotokana na uzazi kwa wanawake.
                 (Preterm Birth Complications)

Matatizo yanayojitokeza kwa mama wajawazitoyanaripotiwa kusababisha zaidi ya vifo milioni 1 hasa kwa nchi zinazoendelea. ambayo ni zaidi ya asilimia 2% ya vifo vyote.
Matatizo haya husababishwa na ukosefu wa elimu kwa wanawake wengi ambapo kunawafanya kushindwa kutunza mimba katika namna inayofaa jambo ambalo hupelekea matatizo mengi wakati wa kujifungua ikiwemo upasuaji usio wa lazima, maambukizi ya magonjwa kama fistula na mengine mengi.

10. Kifua kikuu (Tuberculosis(TB))

Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya bacteria ambavyo husambaa kwa njia ya hewa zaidi ya watu 900000 waliripotiwa kupoteza maisha mwaka 2012 na idadi ya vifo imepingua kwa kiwango kikubwa kwa vile TB inatibika.

No comments:

Powered by Blogger.