Header Ads

JE UNASUMBULIWA NA MAFUA AU VIDONDA MDOMONI? HIVI NDIVYO LIMAU INAWEZA KUKUSAIDIA!

imau ni moja kati ya matunda muhimu zaidi katika mwili kwa vile yana kemikali nyingi na zilizo muhimu zaidi mwilini  huku kubwa ikiwa ni kiwango kikubwa kabisa cha vitamini C ambacho limau linacho.






Vitamini C ni aina ya virutubisho ambavyo mwili huvihitaji kwa ajili ya ukuaji. Virutubisho hivi ni muhimu zaidi mwilini kwa sababu mwili hauna uwezo wa kuvihifadhi hivyo ni lazima ule vyakula vyenye virutubisho kwa wingi kadri uwezavyo, na moja vyakula vilivyo na virutubisho hivi kwa wingi ni Limau.

Mbali na kuwa na kiwango kikubwa cha vitamini C limau pia ina kemikali zifuatazo;

limonene
coumarins
bioflavonoids
mucilage
vitamins A na B
alpha pinene
Beta pinene
alpha terpinene.

Kwa pamoja kemikali hizi zinafanya limau kuwa na nguvu za kutibu magonjwa mengi kama ifuatavyo;
  • Vidonda vya sehemu mbalimbali za mwili.
  • Watu wenye ugonjwa wa kutokwa na damu puani na midomoni.
  • Matatizo ya Ngozi kuwa kavu.
  • Magonjwa ya kansa.
  • Matatizo ya mafua.
  • Kutukwa na damu katika ufizi
  • Limau ina asidi ambayo hufanya kazi kama antiseptiki(kemikali inayoweza kuzuia vimelea vya magonjwa kuzaliana) hivyo hutumika kama kinga ya magonjwa kwa kupaka katika ngozi.
  • Huimarisha mishipa ya damu hivyo kuepusha uwezekano wa magonjwa ya mzunguko wa moyo kama shambulizi la moyo.

Matumizi ya limau yanaonesha kuwa na msaada zaidi kwa watu wenye mafua na watu wenye matatizo ya vidonda vya mdomoni na kutokwa na damu katika ufizi. Kwa watu wenye matatizo haya wanashauriwa kutumia limao kwa kiwango kikubwa. Na pia hushauriwa sana kwa,

*Wazee kwa vile hupambana na sumu ziharakishazo uzee.
*Maumivu ya goti hasa wana riadhaa.
*Wavutaji wa sigara
*Watu wanaotumia tiba za mionzi kama x-rays.

Jinsi ya kutumia Limau kama tiba.

Sehemu ambazo hutumika kama tiba ni pamoja na maganda ya nje, maji ya limau(juisi), mafuta ya limau na maganda ya ndani.

Maganda ya nje na ya ndani husaidia katika kupambana na magonjwa ya mzunguko wa damu kwa vile yana kemikali za mafuta muhimu kama pinene ambazo husaidia kuimarisha mishipa ya damu.

Juisi ya limau hutumika kutibu vidonda, michubuko maumivu na mafua na ili kuleta matokeo mazuri ni vyema kama yatachanganywa na kitunguu saumu na mdarasini. Matumizi ya juisi hii ni vijiko 2 vya juisi unavichanganya na maji nusu kikombe cha chai halafu unakunywa mara 3 kwa siku.

Mfuta ya limau hupatikana katika maganda na yanaweza kuvunwa, mafuta hayo hutumiwa zaidi kutibu magonjwa ya nje ya mwili kama fangasi, vidonda, michubuko, maumivu ya magoti na mifupa na hutumika kwa kupaka.

ZINGATIA,
Matumizi ya mafuta ya limau si salama zaidi hasa sehemu za ndani za mwili hivyo kabla ya kutumia ni vyema kuonana na mtaalamu wa tiba kwa ushauri zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.