Header Ads

HIZI NDIZO NGUVU ZA KITUNGUU SAUMU KATIKA KUPAMBANA NA MAGOJWA!


Kitunguu saumu ni mmea ambao unatumiwa kwa matumizi mbalimbali lakini kubwa ni kutumika kama chakula. Kitunguu saumu kina faida nyingi za kiafya kwa vile kina virutubisho bora kwa ajiri ya ukuaji wa mwili. Mbali na kuwa na virutubisho vingi kitunguu saumu pia kina dutu/kemikali adhimu ambazo zina uwezo wa kupambana na vimelea vya maambukizi ya magonjwa na pia kemikali hizo zina uwezo wa kubadili au kuiga utendaji kazi wa dutu nyingine za mwili  jambo ambalo jambo linalofanya kitunguu saumu kuwa moja ya mitishamba bora zaidi katika kutibu matatizo mbalimbali ya afya.

Nguvu ya kutibu ya Kitunguu saumu inatokana na kuwa na kemikali tiba zifuatazo;
  • Allicin
  • Alliin
  • Alliinase
  • Scordinins
  • Selenium
  • Vitamins(A,B,C and E)
 Uwepo wa kemikali hizi katika kitunguu saumu kunafanya kitunguu saumu kuwa na uwezo wa kutibu matatizo yafuatayo.
  • Kutibu na kukukinga na magonjwa ya mfumo wa upumuaji- magonjwa kama mafua, maumivu ya kifua, kikohozi na asthma haya ni baadhi ya matatizo yanayoweza kutibiwa na kitunguu saumu.


  • Kutibu na kupunguza hatari ya magonjwa ya mzunguko wa damu- kitungu saumu kina kemikali ains ya diallyl trisulfide ambayo husaidia moyo kufanya kazi vizuri.


  • Kupunguza kiwango cha rehemu mwilini- utafiti uliofanywa na journal of nutritional biochemistry unaonesha matumizi ya kitunguu kwa muda usiopungua miezi 4 unaweza kusaidia kupunguza rehemu(mafuta hatari) ya mwili.

  • Kutibu na kuwakinga wanaume dhidi ya saratani ya tezi dume- utafiti uliofanywa na China-japan Friendship hospital na taarifa kuchapishwa katika jarida la asian pacific journal of cancer prevention wa mwaka 2013 unaonesha matumizi ya mimea iliyo na allium ikiwemo kitunguu saumu.kunapunguza hatari ya saratani ya tezi dume kwa wanaume.
  • Matatizo ya ini yanayotokana na ulevi uliokithiri- kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Biochimica et biophysica acta inaonesha matumizi ya kitunguu saumu husaidia kutibu matatizo ya ini hasa wale walioathiriwa na pombe.


  • Husaidia wanawake ambao huzaa kabla ya wakati- wanawake wanaopatwa na matatizo ya kuzaa kabla ya miezi tisa matumizi ya mara kwa mara ya kitunguu saumu hupunguza tatizo hili.


  • Huweza kupambana na vimelea vingi vya magonjwa- kemikali aina ya allium ndani ya kitungu saumu ina uwezo mkubwa wa kuangamiza vijidudu vya magonjwa vikiwemo vile vya bakteria.

  • Husaidia kuulinda mwili dhidi ya saratani hasa ya ubongo- kitunguu saumu kina kemikali za organo-sulfur ambazo huangamiza seli zisababishazo saratani.


  • Faida nyingine za kitungu saumu ni pamoja na hutumika kutibu kuvu(fangasi) zinazoathiri mwili, Vidonda, Magonjwa ya mfumo wa mkojo kama UTI.
Kitungu saumu hutumikaje kutibu?
Sehemu kuu zitumiwazo za kitunguu saumu ni majani na balbu zake(vipande vyake).na huweza kutumiwa kwa namna zifuatazo;
  • Kutumika kwa kutafuna vipande vyake- vipande vya kitunguu humenya na huliwa kwa kutafuna, tumia vipande walau 7-10 kwa wiki ni wastani mzuri kitiba.


  • Kutengeneza juisi ya kitunguu saumu - juisi inayopatikana hutumiwa zaidi kutibu mafua na hutumiwa kwa kijiko kimoja cha chai mara 3 kwa siku.



  • Lulu(maganda mepesi yanayong'aa kabla ya kuvikuta vipande) zina mafuta ambayo huvunwa na ndio yana kiwango kikubwa cha allium.
 Kitunguu saumu huweza kuchanganywa na asali, mchanganyo huu umeonyesha kuwa na matokeo chanya mara dufu ya pale utumiapo kitunguu pekee, pia mchanganyo huu unaonesha kusaidia wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume.

ZINGATIA.
Mutumizi ya kitunguu saumu kwa watoto chini ya miaka 12 na walishawahi ama wanatumia dawa nyingine za mzunguko wa damu ni hatari kwa afya hivyo basi ni vyema kumuona daktari au mtaalamu wa afya ili upate elimu ya matumizi sahihi.

1 comment:

  1. Ahsante sana kwa elimu hii ni muhimu sana. Ila tu nauliza kuna uwezekano wa kuandaa na kupack juice yake kwenye chupa ili iwe rahisi kuwapa wengine ambao hawana access na vitunguu hivi. Kama inawezekana nielekeze.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.