Header Ads

FAHAMU KUHUSU HOMA YA INI, NI KITU GANI? INASABABISHWAJE? NINI MADHARA YAKE NA NAMNA GANI YA KUJIKINGA?


Homa ya ini ni ugonjwa unaotokana na uvimbe katika seli hai za ini. hali hii ya kutengenezwa au kutokea kwa uvimbe kunaweza sababishwa na sababu kuu tatu

  • Mitindo wa maisha wa mtu.
  • Maambukizo ya virusi visababishavyo homa ya ini.
  • Matatizo ya kibaiolojia ya mifumo ya mwili.
kutengenezwa au kutokea kwa uvimbe huu kunaweza pelekea kuundwa kwa kovu katika seli za ini, kuwepo kwa kovu katika seli hizi kunaweza sababisha matatizo makubwa ya kiafya kama vile kansa na ini kushindwa kufanya kazi.
Homa ya ini huweza kutokea kwa namna kuu mbili, yaani
  • Homa ya ini ya muda mfupi- hii hutokea na kudumu kwa muda mfupi sana. aina hii ya homa ya ini mara nyingi haina madhara makubwa kwa vile mwili unaweza pigana na hali hii na kulirudisha ini katika hali ya kawaida kabisa bila madhara yoyote.
  • Homa ya ini ya muda mrefu- hii huanza kama ya muda mfupi lakini mwili unashindwa kupambana na tatizo mpaka kupelekea tatizo kuwa sugu, katika aina hii ya homa ya ini, Ini linaweza kupona lakini itapelekea kuundwa kwa kovu katika sehemu athirika ya ini. kwa hali hii basi homa ya muda mrefu ya ini huambatana na madhara makubwa katika afya ya binadamu, ni aina hii ya homa ya ini ambayo hupelekea kansa ya ini.

HOMA YA INI HUSABABISHWA NA NINI?

Homa ya ini husababishwa na sababu kuu zifuatazo;
  • Mitindo wa maisha wa mtu- mitindo mbalimbali ya maisha kama uvutaji wa sigara na bangi, matumizi ya dawa bila kufuata utaratibu wa wataalamu ulevi pamoja na kutozingatia mlo kamili(kunakopelekea kuwa na kitambi) hii yote ni mitindo ya maisha ambayo inakuweka katika hatari ya kupata  homa ya ini.

  • Matatizo ya kibaiolojia ya mifumo ya mwili- Matatizo ya kibayolojia ambayo mtu anaweza kuyapata akiwa ameshazaliwa ama yale ambayo mtu anazaliwa nayo yanaweza kuwa sababu kuu ya kupata homa ya ini. Matatizo hayo ni pamoja na seli za ulinzi za mwili wako kushambulia seli nyingine ndani ya mwili wako, mapungufu katika ufanyaji kazi wa seli za mwili na matatizo ambayo hutokana na mabadiliko yasiyo sahihi katika chembe za urithi(vinasaba).  

  • Maambukizo ya virusi visababishavyo homa ya ini- njia kuu ambayo ugonjwa huu huenea ni kupitia virusi viitwavyo hepatitis, virusi hivi hushambulia seli hai za ini pekee ambapo hupelekea madhara makubwa katika ini. Mpaka sasa kuna aina nyingi za virusi hivi vya hepatitis ambao husababisha homa ya ini lakini utafiti  unaonyesha kuwa kati ya aina zote hizo ni aina 5 tu ndo zinaonyesha kusababisha madhara makubwa katika afya ya ini. Aina hizo ni;
         > Hepatitis A Virus (HAV)
         > Hepatitis B Virus (HBV)
         > Hepatitis C Virus (HCV)
         > Hepatitis D Virus (HDV)
         > Hepatitis E Virus (HEV).
Tutaziangazia aina hizi za virusi moja baada ya nyingine katika matoleo yayayo lakini hebu tuangalie dalili kuu za homa ya ini bila kujali aina ya njia ambayo imekusababisha kupata ugonjwa huu.
Dalili za homa ya ini ya muda mfupi;
  • Uchovu wa mwili.
  • kukosa hamu ya kula.
  • Homa.
  • Kuharisha.Maumivu ya misuli na maungio ya mwili.
  • Kichefuchefu.
  • Mumivu sehemu ya chini ya tumbo.
  • Kutapika.
  • Kupungua uzito.
Hizi ni dalili za ugonjwa wa homa ya ini katika hatua za awali kabisa ambapo kama mtu atatumia dawa ama kama kinga ya mwili ya mtu iko sawa zinaweza kuisha ndani ya mda mfupi sana bila madhara makubwa.
Lakini kama dalili hizi zitaendelea kwa muda mfupi bila kuisha au kutibiwa kuna uwezekano wa homa hii kuingia hatua nyingine ambayo ni ya muda mrefu, hapa mtu anaweza kuonyesha dalili zifuatazo.
  • Mtatizo ya mzunguko wa damu.
  • Mkojo hubadilika rangi na kuwa manjano yaliyokolea au kuwa mweusi.
  • Kizunguzungu.
  • Kuwashwa kwa mwili.
  • Uvimbe katika maeneo ya yumbo ambao hutokana na kuvimba na kujaa kwa nyongo(dalili hii huwapata sana wale ambao homa ya ini imesababsha na pombe)
  • Maumivu makali ya kichwa.
  • Haja kubwa angavu inayoambatana na ute mweupe kama usaha. 
  • Ngozi kuwa ya manjano pamoja na macho.
  • Vipele vyaweza kujitokeza.
HIzi ni baadhi ya dalili za jumla ambazo mgonjwa wa homa ya ini anaweza kuzionyesha kwa namna moja au nyingine.

No comments:

Powered by Blogger.