FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO, SABABU ZAKE, TIBA NA DALILI.
Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika na kulika kwa kuta za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Kuta ambazo hushambuliwa na vidonda ni
- kuta za tumbo
- kuta za sehemu ya chini ya koo la chakula.
- kuta za sehemu ya kwanza ya utumbo mwembamba.
kuna sababu kuu mbili ambazo hupelekea mtu kupata vidonda vya tumbo,
- Maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori, -bakteria huyu husambaa kwa njia ya maji na chakula, katika mwili wa binadamu hupenda kuishi tumboni na katika sehemu ya kwanza ya utumbo mwembamba. Akiwa hapo huzalisha vimeng'enya viitwavyo urease ambavyo hupunguza kiwango cha tindikali tumboni. kupungua kwa tindikali tumboni kunasababisha nyongo kuzalisha tindikali nyingi zaidi ya uwezo wa tumbo kuzimudu ambazo hupelekea tumbo kutoboka na kuchubuka.
- Kumeng'enywa na kulika kwa kuta za mfumo wa chakula-hii husababishwa kwa namna zifuatazo
Sababu nyingine zinazoweza sababisha vidonda vya tumbo ni pamoja na:
- Uvutaji wa sigara na Bangi
- Ulevi wa Pombe
- Msongo wa mawazo.
- Tiba za miale katika maeneo ya mfumo wa tumbo mfano x-ray.
- Kansa ya Tumbo
- Kuugua kwa muda mrefu magonjwa mengineyo.
Dalili za vidonda vya tumbo.>Maumivu ya tumbo toka maeneo ya chini ya tumbo mpaka kifuani.
>Kinyesi kinakuwa na rangi nyeusi au kijivu.
>Kutapika damu
>Kupungua uzito.
>Kichefuchefu na kutapika.
>Kupoteza hamu ya kula.
>Kiungulia.
Kama vidonda vya tumbo havitatibiwa kwa wakati huweza kusababisha madhara makubwa ambayo tiba yake itahitaji uangalizi mkubwa na unaweza kuwa na gharama kubwa sana. kama utaona dalili hizi basi ni vyema kumuona daktari kwa maana dalili hizi huashiria tatizo limekuwa kubwa zaidi, sababu hizo ni;
-Acha punguza kutumia pombe bila kiasi.>Kinyesi kinakuwa na rangi nyeusi au kijivu.
>Kutapika damu
>Kupungua uzito.
>Kichefuchefu na kutapika.
>Kupoteza hamu ya kula.
>Kiungulia.
Kama vidonda vya tumbo havitatibiwa kwa wakati huweza kusababisha madhara makubwa ambayo tiba yake itahitaji uangalizi mkubwa na unaweza kuwa na gharama kubwa sana. kama utaona dalili hizi basi ni vyema kumuona daktari kwa maana dalili hizi huashiria tatizo limekuwa kubwa zaidi, sababu hizo ni;
- kizunguzungu
- maumivu makali ya kichwa
- kinyesi cheusi ambacho kinaweza ambatana na damu.
- Badili baadhi ya mifumo yako ya maisha kama,
-Usichanganye pombe na aina yeyote ya dawa.
-Weka mazingira yako safi kuepuka maambukizi ya bacteria.
-Usitumie hovyo dawa za kupunguza maumivu bila ushauri wa kitaalamu.
-Pata chakula kwa wakati, epuka kukaa na njaa kwa muda mrefu.
-Kuwa na ratiba nzuri na inayoeleweka ya chakula, epuka kubadili ratiba ya chakula bila sababu za msingi.
ZINGATIA,
Kuna wakati unapojaribu kutibu vidonda vya tumbo inashindikana, huwa inatokea na hii husababishwa na sababu kuu zifuatazo
-----yawezekana una maambukizi ya bakteria zaidi ya mmoja.
-----Yawezekana una ugonjwa mwingine katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kama vile kansa.
Hivyo basi kama una tatizo la vidonda vya tumbo ni vyema uwahi hospitalini mapema upate tiba kabla haijafikia hatua mbaya.
No comments: