Header Ads

ZIFAHAMU AINA ZA MAUMIVU YA KICHWA NA SABABU ZAKE.



Maumivu ya kichwa ni tatizo ambalo huwapata watu wengi zaidi duniani. Tafiti zinaonesha karibu nusu ya watu wote duniani hupata matatizo ya maumivu ya kichwa kila mwaka.

Maumivu ya kichwa huweza kutokea katika namna tofauti ambapo yanaweza kuwa maumivu ya kichwa chote au sehemu ya kichwa, yanaweza kuwa makali sana au ya kawaida au yakawa ya muda mrefu au muda mfupi.


Maumivu ya kichwa yamegawanywa katika namna kuu mbili kutegemea na sababu iliyosababisha. Aina hizo ni;
  • Maumivu ya awali ya kichwa- haya ni aina ya maumivu ambayo husababishwa na mabadiliko ya kiutendaji ya mifumo mbalimbali ya kichwani ambayo yanaweza kuwa ni ya kifiziolojia au mabadiliko yatokanayo na ajali katika sehemu za kichwani. mabadiliko hayo yanaweza kuhusisha mishipa ya damu, misuli ya kichwani, mfumo wa neva wa kichwani na mabadiliko ya utendaji kazi wa kemikali mbalimbali katika ubongo. Mfano wa maumivu haya ni kipanda uso na kizunguzungu
  • Maumivu ya kichwa yanayosababishwa na matatizo mengine- maumivu haya hutokea pale tatizo lingine ndani ya mwili mfano ugonjwa linaposababisha kuamsha neva ambazo hupelekea kuhisi maumivu. Kuna sababbu nyingi ambazo huweza kupelekea maumivu ya kichwa, sababu hizo ni pamoja na;
*Kula vitu vya baridi kupita kawaida.
*Uvimbe katika ubongo
*Kuganda kwa damu maeneo ya kichwani.
*Kuvujia kwa damu katika maeneo mbalimbali ya kichwani hasa katika ubongo.
*Kuvuta hewa ya Carbon monoxide.
*Kupoteza maji mengi.
*Magonjwa ya macho
*Mafua
*Matumizi ya kupita kiwango ya madawa ya kutuliza maumivu
*Kushikwa na hasira.
*Kiharusi.

Maumivu ya kichwa hutokea kwa namna tofauti sana, Kwa vile basi aina ya maumivu ya kichwa hutegemea zaidi ni yanatokea kwa namna gani. Kujua aina ya maumivu ya kichwa ni vyema katika kuchagua tiba sahihi kwa vile maumivu ya kichwa hutibiwa kwa njia tofauti kulingana na aina ya maumivu yenyewe. Zifuatazo ni aina za maumivu ya kichwa kulingana na yanavyotokea;
  • Maumivu ya kichwa ya kuvuta(Tension Headache)
Haya ni maumivu ya kaida ya kichwa na huwatokea watu wengi. maumivu haya ya kichwa husababishwa na mabadiliko ya kawaida ya kifiziolojia katika sehemu ya kichwa. Maumivu haya mara nyingi huanza kama maumivu madogo na huanza kuongezeka kadri ya muda, na mara nyingi hutokea kipindi cha mchana. Sababu kuu za maumivu ya aina hii ni;Kuvaa vitu vinavyobana kichwani.Na maumivu haya huweza  kuhusisha kichwa chote au sehemu ya kichwa na heweza kusambaa hadi shingoni. Maumivu haya huweza kuwa  ya mara chache au yaweza kuwa sugu na huweza kudumu kwa dakika , masaa hadi siku.
  •  Maumivu ya kichwa ya Kipanda uso(Migraine)
Haya ni maumivu ya kichwa ambayo hutokea upande mmoja wa kichwa na mara nyingi sehemu ya mbele ya kichwa na maumivu haya huweza kusambaa hadi maeneo ya usoni. Maumivu haya huambatana na mtu kushindwa kufumbua macho(kutazama), Kichefuchefu,  na kupoteza fahamu. Maumivu hayahuweza kuwa makali kiasi cha kuhatarisha uwai wa mtu. Aina hii ya maumivu ya kichwa mara nyingi hudumu kati ya dakika, masaa  hadi siku 2 au  3, ni mara chache huweza kutokea zaidi ya siku 3.
  • Maumivu ya kichwa ya kujirudia(Rebound Headache).
Haya ni maumivu ya kichwa ambayo hujirudia, maumivu haya husababisha na matumizi ya dawa za kutuliza maumivu wakati chanzo cha maumivu ni ugonjwa hivyo maumivu haya hukata mara baada ya kunywa dawa na hurudi haraka mara tu baada ya nguvu ya dawa kuisha. Maumivu haya huambatana na maumivu ya shingo, kukosa usingizi na Kupoteza radha ya chakula .
  • Maumivu ya kichwa ya vipindi(Cluster headache).
Maumivu haya hutokea kwa nyakati tofauti kwa siku, huweza tokea hata zaidi ya mara nane kwa siku na mara nyingi hudumu kati ya dakika 7 hadi 10. Maumivu haya huwa ni makali na huchoma kama mshale, yanaweza kuwa ya upande mmoja na mara nyingi ni sehemu za kuzunguka jicho na sehemu iliyoathiriwa inaweza kuvimba.
  • Maumivu ya kichwa kugonga kama nyundo(Thunderclap headache)
Maumivu haya ni ya ghafla na ni makali kuliko aina yeyote ya maumivu ya kichwa. Maumivu haya hudumu kati ya dakika 5 na zaidi. Maumivu haya huwa ni hatari kwa uhai wa binadamu kwa vile sababu zake ni hatarishi zaidi. Sababu zake huweza kuwa Kuvujia kwa damu katika ubongo, kupasuka kwa mishipa ya damu ya kichwani, kuminyika kwa mishipa ya damu ya kichwani na ubongo, na uti wa mgongo. Mtu apatapo tatizo la maumivu ya namna hii ni vyema kuonana na daktari haraka iwezekanavyo vinginevyo yaweza pelekea hatari zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.