KIHARUSI(STROKE) UGONJWA UNAOONGOZA KWA KUSABABISHA VIFO DUNIANI! UFAHAMU ILI KUEPUKANA NAO.
Kiharusi ni ugonjwa unaosababishwa na damu kushindwa kufika ama kufika kwa kiwango kidogo sana katika seli za ubongo. Kushindwa kufika kwa damu katika seli za ubongo kunapelekea seli za ubongo kufa. Kufa kwa seli za ubongo kunasababisha ubongo kushindwa kufanya kazi na kwa vile ubongo hufanya
kazi ya kuratibu na kudhibiti muingiliano wa utendaji wa mifumo mbalimbali ya
mwili hvyo basi kiharusi kama kisipopatiwa uvumbuzi wa haraka husababisha kifo.
Kiharusi kinatajwa kuwa ndio ugonjwa unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi duniani kote. Kuna sababu tofauti ambazo zinaweza kupelekea mtu kupata kiharusi, baadhi ya sababu hizo ni pamoja na;
- Uzito uliopita kiwango
- Kiwango kikubwa cha Rehemu mwilini
- Msongo wa mawazo
- Uvutaji wa sigara
- Umri mkubwa watu walio na zaidi ya miaka 55 huwa katika hatari zaidi
- Kutokufanya mazoezi
- Matumizi ya madawa mbalimbali hasa ya kulevya.
- Kiharusi kinachosababishwa na kupasuka ama kuminyika kwa mishipa ya damu inayopeleka damu katika ubongo hivyo kiwango cha damu kinachotakiwa kufika katika ubongo kinapungua au kushindwa kufika kabisa. aina hii ya kiharusi huwapata watu wengi zaidi duniani, zaidi ya 85% ya matatizo yote ya kiharusi yanayoripotiwa duniani ni ya aina hii yaani yanasababishwa na kupasuka au kuminyika kwa mishipa ya damu inayopeleka damu katika ubongo. sababu kubwa inayopelekea mishipa ya damu kupasuka au kuminyika ni uwepo wa bonge la damu lililoganda ndani ya mishipa ya damu.Uwepo wa bonge la damu lililoganda katika mishipa ya damu ambalo ni matokeo ya mlundikano mkubwa wa mafuta katika mwili. Bonge hili la damu lililoganda husababisha kupungua kwa upana wa mshipa wa damu na kuzuia kiwango cha damu kupita kutoka upande mmoja kwenda mwingine(mishipa inayoathiriwa na tatizo hili ni ile ya ateri ambayo hupeleka damu maeneo mbalimbali ya mwili).
- Kiharusi kinachosababishwa na damu kuvuja kutoka katika mishipa ya damu na kuingia maeneo yaliyojirani na mishipa hiyo ambayo ni seli za ubongo. Damu hiyo ikifika katika uso wa kiwambo cha seli hubadilisha shinikizo lililopo kati ya mazingira ya nje ya seli na yale ya ndani, shinikizo hili husaidia usafirishwaji wa dutu mbalimbali zinazoingia na kutoka nje ya seli kwa hivyo mabadiliko yeyote ya shinikizo hili huleta madhara katika seli huku kubwa ikiwa ni seli kufa. Kuvuja kwa mishipa ya damu ya ubongo kunaweza sababishwa na kuongezeka kwa shinikizo la damu, dawa zinazopelekea damu kuwa nyepesi ambapo damu kuwa nyepesi inaongeza shinikizo na Udhaifu wa mishipa ya damu katika ubongo.
Kiharusi ni tatizo ambalo hutokea haraka na kwa kushtukiza, si rahisi kuzijua dalili za awali ambazo zinaweza kukujulisha kwamba utapata kiharusi. Zifuatazo ni dalili ambazo mtu huzipata mara tu ashambuliwapo na kiharusi;
- Kuchanganyikiwa ambako huathiri uwezo wa kuongea na kufikiri
- Maumivu ya ghafla ya kichwa ambayo huambatana na kupoteza fahamu.
- Kupatwa na ganzi miguuni, usoni, miguuni au upande wowote wa mwili.
- Kupoteza uwezo wa kuona na kutambua.
- KIzunguzungu na kushindwa kutembea.
- Kushindwa kudhibiti haja kubwa na ndogo
- Msongo wa mawazo.
- Maumivu makali y amikono na miguu yakiambatana na kushindwa kutembea.
- Kudhoofu mwili mzima au sehemu ya mwili.
- Kushindwa kudhibiti hisia.
- Upande mmoja wa uso kuwa mzito kuliko mwingine
- Mkono mmoja kuwa mzito na dhaifu kuliko mwingine
- Kuongea kwa shida au kupata kigugumizi cha ghafla.
No comments: